Elections 2010 Tendwa na pingamizi la chadema dhidi ya kikwete

wishega

Member
Sep 6, 2010
7
0
Awali yote napend kuwaslimia ndugu zangu wa Jamii Forum,Leo napenda kuzungimzia pingamizi la CHADEMA dhidi ya mgombea urais wa CCM kuhusu kukiuka mkataba wa Sheria ya gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010.

Hivi kuna mtu alitegemea kuwa msajili wa vyama vya siasa angefanya maamuzi ambayo yangeonyesha dhahiri kuwa CCM imekiuka mkataba huo? Msajili wa vyama vya siasa ni ametuliwa na rais je inawezekanaje akatoa maamuzi ambayo hayatomtoa kimasomaso rais?

Rais wa Uganda ndugu Yoweri Kaguta Museveni aliwahi kusema kama rais ikiwa bado upo madarakani huwezi kushindwa uchaguzi wakati mamlaka zenye kutangaza ushindi zimetokana na uteuzi wako,alisema maneno haya alipokuwa akitoa maoni yake juu ya uhindi wa Rais Kibaki ambaye alimlazimisha aliyekuwa mwenyekiti Tume ya Taifa ya Uchaguzi wa Kenya wakayi huo Jaji SAmuel Kivuitu amtangaze mshindi. Katika hili nataka kusema kwamba maranyingi wateule wa rais hufanya maamuzi ya kuwafavor waliowateua.
 
Back
Top Bottom