Elections 2010 Tendwa atabiri viti 100 vya ubunge kwenda upinzan

Tendwa, tangu lini umegeuka mtabiri? Nijuavyo kazi yako ni kusimamia demokrasia katika uwanja wa siasa za vyama vingi.. kwani hawawezi kupata 200, au hata 10, au 300. Kwa nini 100 pekee????

maana ya huu utabiri ni kuwa upinzani hauwezi kushinda uchaguzi mwaka huuu
upinzani utapata viti 100 ambavyo ni less than half of the total seats, hii ni dhairi yuko bias kwa ccm
 
maana ya huu utabiri ni kuwa upinzani hauwezi kushinda uchaguzi mwaka huuu
upinzani utapata viti 100 ambavyo ni less than half of the total seats, hii ni dhairi yuko bias kwa ccm

Hapa ndipo ndoto ya Dr Slaa ya kubadilisha katiba ndipo inapokuwa ya msingi kuliko ahadi zooote zinazotolewa na thithiemu, wala hawazungumzii tatizo la kiutendaji la wakuu wa taasisi kama PCCB, NEC, Mahakama, Msajili wa Vyama, etc kuwa miliki ya mtu mmoja. Bahati mbaya mtu huyo ni dhaifu kama JK.
 
Mwitaaaa:That's something to do with the law,nahisi unatamani kuwa jaji mkuu wa Tanzania!!Lol
 
Mwitaaaa:That's something to do with the law,nahisi unatamani kuwa jaji mkuu wa Tanzania!!Lol

jk_203.jpg
 

Mkuu Masanilo,

Picha hii inasikitisha, inatia huruma na inaleta maswali mengi zaidi. Mkuu wa Kaya kalegea kabisaaaa kama mgonjwa mahututi, sijui hata kama alikuwa anajitambua, na hiyo ni within a fraction of a minute.
 
Mkuu Masanilo,

Picha hii inasikitisha, inatia huruma na inaleta maswali mengi zaidi. Mkuu wa Kaya kalegea kabisaaaa kama mgonjwa mahututi, sijui hata kama alikuwa anajitambua, na hiyo ni within a fraction of a minute.

Unapoteza kabisa fahamu zote kwa muda! Jamaa mgonjwa hebu google hii "petit mal epilepsy" condition ya muungwana.
 
Walio usingizini ni wale wanaoshangilia "utabiri" wa Tendwa bila kujua kwamba Tendwa ni kama mnyama mkali mwenye sauti nyororo anayeimba nyimbo nje ya mlango wao, huku akitokwa na mate ya uchu wa nyama pindi wakifungua mlango.

Can't anybody smell a rat here? Tendwa aende out of his way kutabiri ushindi wa upinzani ? What's in it for him, anataka kuanzisha biashara ya upinzani baada ya kuacha usajili ?

Kweli kabisa haiwezekani mtu ambaye tumemwona juzi juzi tu hapa anakandamiza upinzani leo hii aanze kutabiri ushindi. Liko kubwa zaidi, anataka tumwamini atakaposema pingamizi la Slaa kwa Kikwete halina mshiko, tumwone kama vile alivyoweza kubashiri haya basi pengine ni kweli hili. Kwani kuna gumu zaidi katika siasa za mwaka huu kama pingamizi hili likipita? Ni nani anaweza akabashiri maana yake (implications) za kukubaliwa pingamizi hili? Si uchaguzi au utaahirishwa au utaendelea na hao wachache, na je CCM na kiburi chao watafanya nini, huoni kuna shida kubwa; Tendwa anafahamu kilicho mbele yake ni maamuzi makubwa, anapenda sasa kuonekana upande wa upinzani, ni unafiki!

Kiranga - you are damnly right!
 
Unajua tatizo lako wewe Nostradamus ni apologist wa CCM, ulikuja hapa kwa gia ya ooh wananchi nao ni chanzo cha matatizo yetu, mara kujifanya motivational speaker mara tuendeshe mijadala. Lakini I have read your posts btn words and concluded that you are nothing but a CCM apologist. Unaweza kusema nimeenda personal au kuleta name calling. Yes I had to do it kwa sababu unapoteza mida ya watu hapa and I think it is high time watu wakakutambua. Jidhihirishe kama wenzako akina MS.
 
Tindwa ni mtu aliye katika mission, kwa hiyo ili afanikishe malengo yake/waliomtuma, lazima aseme kauli kama hiyo kulainisha mambo atakapo gueka nyuzi 90, hamna cha viti mia... wala nini
 
Masanilo:Google "Stress",I swear mwaka huu zimekujaa sana bro,CCM wanashinda kwa sera,ugonjwa si hata jambo la kutumia kufanyia kampeni.Wananchi watawachapa fimbo kwa kura.Subiri uone mambo kaka.
 
tumeucha.jpg
Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu ofisi yake kupokea rasmi malalamiko ya chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema yanayodai mgombea urais kupitia CCM kukiuka sheria ya ghalama za uchaguzi . Picha na Said Powa

Na Ramadhan Semtawa

WAKATI joto la uchaguzi likizidi kupanda, Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tenda ametabiri kuwa vya vya upinzani vinaweza kupata viti 80 hadi 100 kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano kama watacheza karata zao vizuri. Msajili ametoa kauli hiyo wakati upinzani ukionekana kuzidi kukua baada ya wabunge kadhaa wa chama tawala kuhamia vyama vya upinzani kutokana na kutokubaliana na mchakato wa kura za maoni na matokeo yake, huku baadhi ya vyama vikijiimarisha kwenye majimbo kwa kuweka wanachama wenye nguvu, wakiwemo viongozi wao wakuu.

Wanachama wengi walioihama CCM na kuhamia upinzani wamesimamishwa kwenye majimbo waliyokuwa wakiyashikilia zamani kupambana na chama tawala, wakati Chadema na TLP zikisimamisha wenyeviti wao kugombea ubunge.

Akizungumza na Mwananchi ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana kuhusu mwelekeo wa uchaguzi huo, Tendwa alisema mtazamo wake unatokana na sababu kuu nne ambazo anaamini zitaongeza idadi ya wapinzani bungeni kama wakicheza vizuri karata zao.

"Wapinzani wanaweza kupata viti kati ya 80 hadi 100 kama wataweza kujipanga vema. Temperature (joto) ya kisiasa iko juu sana kwa sasa," alisema msajili huyo.

Tendwa aliitaja sababu ya kwanza kuwa ni mwamko mkubwa ambao ameuona kwa Watanzania katika kushiriki kwenye mchakato wa kuchagua viongozi, hali ambayo alisema imepandisha joto la kisiasa.

"Mwamko wa Watanzania ni mkubwa sana," alifafanua Tendwa.

Mkuu huyo wa ofisi hiyo yenye dhamana ya malezi na kuangalia mwenendo wa vyama vya siasa nchini, alitaja sababu nyingine kuwa ni kuwepo kwa mwamko pia kuanzia ndani ya vyama vyenyewe vya siasa.

Alisema yapo mabadiliko ndani ya vyama ambayo yameongeza joto la kisiasa kutokana na mwamko mpya ambao awali haukuwepo kutokana na mazingira ya mfumo na wakati."Unaangalia pia public (umma) inasema nini. Ukiangalia ndani ya vyama kuna watu ambao hawakuwa wametarajiwa kuong'olewa, lakini wameangushwa kwenye kura za maoni wakati wa mchakato wa wabunge," alifafanua.

"Kura za maoni ndani ya vyama zimeonyesha public inasema nini. Kuna mwamko mkubwa kwa wapigakura ambao tumeona si ndani ya chama tawala pekee ambako kuna majina yasiyotarajiwa yaliangushwa, bali hata ndani ya vyama vya upinzani kulikuwa na mwamko mkubwa."

Wabunge wengi vigogo ndani ya CCM, akiwemo mwanasiasa mkongwe John Malecela, waliangushwa kwenye kura za maoni ndani ya CCM, sambamba na mawaziri watano.

Visiwani Zanzibar, zaidi ya wawakilishi 10 wanaomaliza muda wao walianguka kwenye kura za maoni za CUF, huku Chadema ikikumbwa na mapambano kwenye baadhi ya majimbo na uchaguzi wa wabunge wa viti maalum kiasi cha uongozi kuamua kusitisha mchakato huo.

"Umeona uchaguzi wa wabunge wa viti maalum wa Chadema umeahirishwa; hii yote ni mwamko kwa wapigakura kuanzia ndani ya vyama," alisema Tendwa.

Tendwa alisema sababu ya tatu ni kuwepo mabadiliko ndani ya chama tawala ambayo yamesababisha baadhi ya makada kwenda vyama vya upinzani kwa wingi.Alieleza kuwa zamani haikuwa rahisi kuona makada kutoka chama hicho tawala wakikihama na kukimbilia upinzani kama ilivyo sasa hivi.

"Hiki si kitu ambacho ni cha kawaida sana. Hivi sasa kuna makada wa CCM wanaamua kwenda upinzani. Zamani hii haikuwa rahisi sana au kwa kiasi kama cha safari hii," alisema.

Waziri wa zamani, Arcado Ntagazwa, mbunge wa siku nyingi wa Maswa, John Shibuda, mbunge wa kwanza wa Jimbo la Njombe Magharibi, Thomas Nyimbo na mbunge wa zamani wa Mlalo, Charles Kagonji ni miongoni mwa vigogo waliohamia Chadema baada ya kumalizika kwa kura za maoni wakifuatwa na wanachama wanaowaunga mkono.

Mbunge wa zamani wa Kishapu, Fred Mpendazoe aliihama CCM kabla ya Mkutano wa Tisa wa Bunge kumalizika na kujiunga na chama kipya cha CCJ kabla ya kutua Chadema.

Wengine ni Sijapata Nkayamba na Omary Likwelilo maarufu kama Dunia ambao wamehamia CUF pia wakiwa na wanachama wengine wanaowaunga mkono.

"Hayo yote ni changamoto na ishara kwamba kunaweza kuwepo na mabadiliko makubwa katika ukuaji wa demokrasia. Hilo linaonyesha kuwa wananchi wana uhuru na haki ya kujiunga na chama chochote cha siasa," alisema.

Tendwa alitaja sababu ya nne kuwa ni kuwepo mazingira huru ya kidemokrasi ambayo yanafanya vyama vya upinzani na tawala kufanya kampeni zao kwa uhuru, haki na usawa.
Alidai kuwa hakuna ukandamizaji wowote wa haki za vyama kwa kuwa viko huru kunadi sera zao, bila kuingiliwa wala kusumbuliwa na upande wowote uwe wa chama tawala au upande wa vyombo vya dola.

"Nchi ina mazingira mazuri mno ya kidemokrasia; hakuna chama kinazuiwa kunadi sera zake. Vyama vina uhuru mpana kunadi sera zao kwa wapigakura na hakuna mtu anaweza kuwasumbua."
Aliongeza kwamba mwaka 2005 alitabiri kuwa upinzani ungepata viti vingi, lakini hilo halikuwezekana kwa sababu muda wa kampeni uliongezeka baada ya kufariki kwa mgombea mwenza wa Chadema.

Akiwa Hoteli ya Hill Top mkoani Kigoma, Tendwa aliitisha mkutano na waandishi baada ya ziara yake katika maeneo mbalimbali nchini na kueleza kuwa upinzani ungeweza kupata viti hadi 60 lakini uchaguzi huo uliahirishwa kutokana na kifo mgombea huyo.

Viti vya majimbo vinatarajiwa kufikia 245 wakati vya viti maalum na uteuzi vikifanya jumla ya wabunge wote kufikia 315.

Source. Tendwa atabiri viti 100 vya ubunge kwenda upinzani
 
Jamani Utabiri sii lazima utumie bao, mtu yeyote anaweza kutabiri kisayansi na ikakubalika kutokana na statistical patterns.
Kwa hiyo alichofanya Tendwa ni kutazama Upinzani ulivyojipanga hadi sasa na kuzungumzia ushindani uliopo. Hata JK mwenyewe rais na mgombea anaweza kukiri kwamba safari hii kuna uwezekano mkubwa wa Upinzani kuzoa viti bungeni.
 
Back
Top Bottom