Elections 2010 Tendwa atabiri viti 100 vya ubunge kwenda upinzan

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,349
6,476
Hivi huku sio kuvunja maadili ya kazi yake? Kwa nini asitabiri hivyo 100 kuwa ni vya CCM? Huku sio kupigia kampeni CCM? Yaani na yeye anaungana na kazi ya Sheikh Yahya!!? Basis ya utabiri wake ni nini?

Source: Mwananchi 1/9/10
 
Katika gazeti la mwananchi leo msajili wa vyama vya siasa John Tendwa amesema anatabiri upinzani kupata viti kati ya 80 hadi 100 vya ubunge kama watacheza karata zao vizuri.Sababu hizo ni:
1.Mwamko wa wananchi ndani ya Vyama.
2.Kura za maoni ndani ya Vyama.
3.Mabadiliko ya mfumo ndani ya CCM ambayo yamesababisha baadhi ya makada wake kuondoka kama Mpandazoe.
4.Mazingira huru ya demokrasia.

Hii yaweza kuwa ndoto kubwa ya mchana ambayo tutaijua wazi mwezi Novemba.Hivi kabla ya kuiota,Tendwa anajua kwamba muda si mrefu katika chaguzi za serikali za mitaa CCM imeshinda kwa karibu asilimia 80%??????

Najua yuko macho,alikuwa tu amepitiwa kidogo.
 
Katika gazeti la mwananchi leo msajili wa vyama vya siasa John Tendwa amesema anatabiri upinzani kupata viti kati ya 80 hadi 100 vya ubunge kama watacheza karata zao vizuri.Sababu hizo ni:
1.Mwamko wa wananchi ndani ya Vyama.
2.Kura za maoni ndani ya Vyama.
3.Mabadiliko ya mfumo ndani ya CCM ambayo yamesababisha baadhi ya makada wake kuondoka kama Mpandazoe.
4.Mazingira huru ya demokrasia.

Hii yaweza kuwa ndoto kubwa ya mchana ambayo tutaijua wazi mwezi Novemba.Hivi kabla ya kuiota,Tendwa anajua kwamba muda si mrefu katika chaguzi za serikali za mitaa CCM imeshinda kwa karibu asilimia 80%??????

Najua yuko macho,alikuwa tu amepitiwa kidogo.
Wewe na Tendwa nani mweye data za mienendo ya vyama, acha kupayuka kama imekunywa mataputapu leta data vinginevyo nyamaza no research no right to speak.
 
Tanzania nchi inaelekea wapi?

Msajili wa vyama vya siasa, mtu anayetakiwa kuwa na the highest integrity na neutrality, anaendekeza speculation na utabiri kama Sheikh Yahya Hussein ?

Anajiweka katika position ya wana CCM kukosa imani naye kwa sababu wanaweza kusema ana bias ya upinzani, na wapinzani kutokuwa na imani naye kwa sababu wanaweza kusema ana bias ya CCM (kashaanza kusema pingamizi la Slaa halina uzito kabla hata ya vikao rasmi) na watu neutral kama sisi kuona simply hana neutrality inayotakiwa na ofisi yake.
 
Tanzania nchi inaelekea wapi?

Msajili wa vyama vya siasa, mtu anayetakiwa kuwa na the highest integrity na neutrality, anaendekeza speculation na utabiri kama Sheikh Yahya Hussein ?
Neutrality doesn't mean no right to speak hayo ni maoni yake binafsi na si ya Ofisi ya Msajili.
 
Neutrality doesn't mean no right to speak hayo ni maoni yake binafsi na si ya Ofisi ya Msajili.

Ukiwa ofisa wa ofisi fulani zenye influence kubwa katika siasa, maoni yako binafsi yanayoingiliana na kazi yako unayaacha kichwani mwako, ama sivyo yanaingilia neutality yako na kuku disqualify kwa kazi yako.

Hii probably ni plot ya CCM kuwafanya wapinzani wajisikie comfortable na Tendwa, probably imepitiwa na kupigwa OK na Makamba na Kikwete. Wanajua mchezo wa kuuma na kupuliza, wanajua wanataka kuwauma vikali katika pingamizi la Slaa kwa hiyo wanaanza kwa kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa, halafu watatupilia mbali pingamizi la Slaa bila kulijadili sana, halafu watapuliza tena na some bullshyt kama hizi prediction.

Ndiyo mambo yanavyoenda, lakini waaapi, mashabiki wa upinzani walio shallow wanaopenda upinzani usifiwe tu bila hata kujiuliza kwa nini huyu kada wa CCM asifie upinzani against neutrality principles watadaka ndoano na kuimeza moja kwa moja.

Ulishaona wapi referee anatangaza utabiri wa matokeo ya mpira kabla mpira haujaanza, ukiona hivyo utasema "maoni yake tu hayo"? si utashtuka?

Hivi Tendwa angesema CCM itashinda kwa asilimia 98 napo ungesema "maoni yake tu"? Au mkuki mtamu kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu?
 
Hivi Tendwa angesema CCM itashinda kwa asilimia 98 napo ungesema "maoni yake tu"? Au mkuki mtamu kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu?
Kwa nini unani judge mapema au unanionaje, hata kama akisema CCM watashinda kwa kishindo nitasema hivyo hivyo ni maoni yake.
 
Tendwa, tangu lini umegeuka mtabiri? Nijuavyo kazi yako ni kusimamia demokrasia katika uwanja wa siasa za vyama vingi.. kwani hawawezi kupata 200, au hata 10, au 300. Kwa nini 100 pekee????
 
Kwa nini unani judge mapema au unanionaje, hata kama akisema CCM watashinda kwa kishindo nitasema hivyo hivyo ni maoni yake.

Unaelewa maana ya hii alama (?).

Apparently kwako wewe referee kuwa neutral si issue kubwa, ukishindwa game utalalamika umeonewa ?
 
Kiranga amka usingizini.

Walio usingizini ni wale wanaoshangilia "utabiri" wa Tendwa bila kujua kwamba Tendwa ni kama mnyama mkali mwenye sauti nyororo anayeimba nyimbo nje ya mlango wao, huku akitokwa na mate ya uchu wa nyama pindi wakifungua mlango.

Can't anybody smell a rat here? Tendwa aende out of his way kutabiri ushindi wa upinzani ? What's in it for him, anataka kuanzisha biashara ya upinzani baada ya kuacha usajili ?
 
Tendwa atabiri viti 100 vya ubunge kwenda upinzani

Tuesday, 31 August 2010 22:25

Na Ramadhan Semtawa

WAKATI joto la uchaguzi likizidi kupanda, Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tenda ametabiri kuwa vya vya upinzani vinaweza kupata viti 80 hadi 100 kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano kama watacheza karata zao vizuri. Msajili ametoa kauli hiyo wakati upinzani ukionekana kuzidi kukua baada ya wabunge kadhaa wa chama tawala kuhamia vyama vya upinzani kutokana na kutokubaliana na mchakato wa kura za maoni na matokeo yake, huku baadhi ya vyama vikijiimarisha kwenye majimbo kwa kuweka wanachama wenye nguvu, wakiwemo viongozi wao wakuu.

Wanachama wengi walioihama CCM na kuhamia upinzani wamesimamishwa kwenye majimbo waliyokuwa wakiyashikilia zamani kupambana na chama tawala, wakati Chadema na TLP zikisimamisha wenyeviti wao kugombea ubunge.

Akizungumza na Mwananchi ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana kuhusu mwelekeo wa uchaguzi huo, Tendwa alisema mtazamo wake unatokana na sababu kuu nne ambazo anaamini zitaongeza idadi ya wapinzani bungeni kama wakicheza vizuri karata zao.

"Wapinzani wanaweza kupata viti kati ya 80 hadi 100 kama wataweza kujipanga vema. Temperature (joto) ya kisiasa iko juu sana kwa sasa," alisema msajili huyo.

Tendwa aliitaja sababu ya kwanza kuwa ni mwamko mkubwa ambao ameuona kwa Watanzania katika kushiriki kwenye mchakato wa kuchagua viongozi, hali ambayo alisema imepandisha joto la kisiasa.

"Mwamko wa Watanzania ni mkubwa sana," alifafanua Tendwa.

Mkuu huyo wa ofisi hiyo yenye dhamana ya malezi na kuangalia mwenendo wa vyama vya siasa nchini, alitaja sababu nyingine kuwa ni kuwepo kwa mwamko pia kuanzia ndani ya vyama vyenyewe vya siasa.

Alisema yapo mabadiliko ndani ya vyama ambayo yameongeza joto la kisiasa kutokana na mwamko mpya ambao awali haukuwepo kutokana na mazingira ya mfumo na wakati.
"Unaangalia pia public (umma) inasema nini. Ukiangalia ndani ya vyama kuna watu ambao hawakuwa wametarajiwa kuong'olewa, lakini wameangushwa kwenye kura za maoni wakati wa mchakato wa wabunge," alifafanua.

"Kura za maoni ndani ya vyama zimeonyesha public inasema nini. Kuna mwamko mkubwa kwa wapigakura ambao tumeona si ndani ya chama tawala pekee ambako kuna majina yasiyotarajiwa yaliangushwa, bali hata ndani ya vyama vya upinzani kulikuwa na mwamko mkubwa."

Wabunge wengi vigogo ndani ya CCM, akiwemo mwanasiasa mkongwe John Malecela, waliangushwa kwenye kura za maoni ndani ya CCM, sambamba na mawaziri watano.

Visiwani Zanzibar, zaidi ya wawakilishi 10 wanaomaliza muda wao walianguka kwenye kura za maoni za CUF, huku Chadema ikikumbwa na mapambano kwenye baadhi ya majimbo na uchaguzi wa wabunge wa viti maalum kiasi cha uongozi kuamua kusitisha mchakato huo.

"Umeona uchaguzi wa wabunge wa viti maalum wa Chadema umeahirishwa; hii yote ni mwamko kwa wapigakura kuanzia ndani ya vyama," alisema Tendwa.

Tendwa alisema sababu ya tatu ni kuwepo mabadiliko ndani ya chama tawala ambayo yamesababisha baadhi ya makada kwenda vyama vya upinzani kwa wingi.Alieleza kuwa zamani haikuwa rahisi kuona makada kutoka chama hicho tawala wakikihama na kukimbilia upinzani kama ilivyo sasa hivi.

Chanzo:Mwananchi
 
Hivi huku sio kuvunja maadili ya kazi yake? Kwa nini asitabiri hivyo 100 kuwa ni vya CCM? Huku sio kupigia kampeni CCM? Yaani na yeye anaungana na kazi ya Sheikh Yahya!!? Basis ya utabiri wake ni nini?

Source: Mwananchi 1/9/10

Hii issue ipo katika thread nyingine hapa. Na kuhusu ukiukwaji wa maadili nimeongelea hapa

https://www.jamiiforums.com/uchaguzi-tanzania-2010/71839-ndoto-ya-tendwa-na-viti-mia.html

https://www.jamiiforums.com/uchaguz...-ndoto-ya-tendwa-na-viti-mia.html#post1058570
 
Back
Top Bottom