Elections 2010 Tendwa aionya CCM kuacha kutumia nyenzo za Ikulu

Kama sijasahau, hii sheria ya uchaguzi ilimdhalilisha hata Kikwete mwenyewe kwa kusaini bila kujua vimeongeza vifungu vingine nje ya vilivyopitishwa na bunge!
Ni kheri huyo Tendwa angesema ameamua kutupilia mbali hilo pingamizi kwa sababu aliyesaini sheria za uchaguzi alikuwa hajui vizuri hizo sheria zitatumikaje!
 
wameishatoa maelezo kuwa sheria haijavunjwa

sasa nyie mnataka nini? na yule mke wa watu vipi?
Mke wa mtu na sheria ya uchaguzi wapi na wapi? some ignorance's are genetically determined, cant be changed by learning.
 
Kumbuka 16 June 2010, Fikiria Jana na tungoje 31 Oktoba 2010. Wahusika wakuu katika tarehe zote hizo ni wanasheria.

Tutegemee nini 31 Oktoba???????

Pamoja na kwamba wengi wetu hatukutegemea Tendwa aamue swala la pingamizi kwa haki lakini tulitegemea atoe ufafanuzi kwa nini ameamua kutupilia mbali pingamizi la Chadema. Lakini Tendwa alijua akiigia katika ufafanuzi wanasheria wenzake watambana na ushabiki wake utawekwa juani. Mwishowe aliishia kulalama kwamba pingamizi hili limezusha chuki na mengineyo. Ni masikitiko sana kwamba wanasheria wakubwa nchini wamegeuka kuwa wasimazii wa kupotosha haki kwa malengo finyu ya kuogopa watawala. Kuanzia Rufaa ya Mgombea binafsi na sasa hili la uchaguzi. Huko Kenya ni Bwana Kivuitu ( mwanasheria) alisababisha vurugu katika uchaguzi wa 2007. Wanasheria walichachamaa kweli kweli. Wako wapi wanasheria wetu nchini?
 
Personally they have met my expectations. I was not expecting something different kulingana na mambo ya hovyohovyo yanayoendelea hapa nchini. Kuna class fulani ya watu ambayo wako juu ya sheria yeyote. Kwa mfano issues za EPA, Richmond, kesi ya Zombe, issue ya RADA, kesi ya chenge ni mifano michache kati ya mingi inayoonyesha kuwa sheria haiko applicable kwa watu fulani fulani. YANA MWISHO
 
Wewe usitegemee maajabu mpaka Makamba kufikia atua ya 'kubwatuka'in fact nikawaida yake kwani twamjua jinsi alivyokilaza, ila kwa hili jambo ni jambo ambalo si tu Tendwa analiamua kwa faida ya 'bosi wake' ila pia maamuzi hayo yametolewa na wenye nchi akiwemo makamba mwenyewe...nadhani jambo lilo jema kwa wakati huu nikuwaadhibu katika upigaji kura na kama kuna jambo la kufanya kama wananchi kwa sasa ndio wakati wake tusikubali kuyumbishwa tena...leo imetokea kwa Chadema kesho itakutokea wewe au mimi .......
 
Pamoja na kwamba wengi wetu hatukutegemea Tendwa aamue swala la pingamizi kwa haki lakini tulitegemea atoe ufafanuzi kwa nini ameamua kutupilia mbali pingamizi la Chadema. Lakini Tendwa alijua akiigia katika ufafanuzi wanasheria wenzake watambana na ushabiki wake utawekwa juani. Mwishowe aliishia kulalama kwamba pingamizi hili limezusha chuki na mengineyo. Ni masikitiko sana kwamba wanasheria wakubwa nchini wamegeuka kuwa wasimazii wa kupotosha haki kwa malengo finyu ya kuogopa watawala. Kuanzia Rufaa ya Mgombea binafsi na sasa hili la uchaguzi. Huko Kenya ni Bwana Kivuitu ( mwanasheria) alisababisha vurugu katika uchaguzi wa 2007. Wanasheria walichachamaa kweli kweli. Wako wapi wanasheria wetu nchini?

Akina samweli kivuitu wapo wengi sana Tanzania, ni ajabu kuelezea chuki, bugudha na mengineyo ambayo sio msingi wa lalamiko la chadema. Usiri ni wa nini, je kulikuwa na ulazima wa kuufanya uamuzi huo wa siri?
 
Majibu aliyoyatoa Tendwa just a layman angeweza kuyatoa.
Na iyo ya kuilaumu CCM kutumia yale mabango kaiongela kimzaa mzaa si awapige barua?
Haoni kwamba CCM wanaamsha chuki ie wapinzani dhidi ya serikali yao kwa kuwa biase na kuibeba CCM kwa mgongo wa wavuja jasho wa Tanzania ie embezzlement
 
Kama mtu anaweza kudharau mahakama na kuhukumiwa,,wanaibuka wananchi wenye hasira,,, mahakama inaamua kufutilia mbali hukumu unategemea nini?
 
Jamani nasikitika sana kusoma kuhusu maamuzi ya Tendwa,

kimsingi tangu Ndugu John Mnyika anawasilisha hoja, niliiangalia kwa umakini sana ukizingatia alizyo panga hoja. Mambo yote yalijitosheleza ila sikua na matarajio tofauti na yalio tolewa jana kwa maana hiyo ninawapa pole wenzangu waliotarajia vinginevyo!

Kingine niwapongeze wana CHADEMA kwa jitihada kwani dunia nzima inge wadai baadae na vizazi vijavyo vinge wadai CHADEMA kuhusiana na swala hili! Wametekeleza wajibu wao wa kisheria na sisi tunaoishi leo tumeona jitihada sema tu mfumo wetu haujaupokea demokrasia ya kweli. Sheria zinatungwa kuwadhibiti wanyonge wakati inawapendelea wenye madaraka!

Tahadhari! Makamba, Kikwete and CCM kwa ujuma wajue kwamba kuna kizazi kinakuja makini kuliko walivyo sasa hivi!
 
Kama sijasahau, hii sheria ya uchaguzi ilimdhalilisha hata Kikwete mwenyewe kwa kusaini bila kujua vimeongeza vifungu vingine nje ya vilivyopitishwa na bunge!
Ni kheri huyo Tendwa angesema ameamua kutupilia mbali hilo pingamizi kwa sababu aliyesaini sheria za uchaguzi alikuwa hajui vizuri hizo sheria zitatumikaje!



Mkuu, huwezi kuvunja sheria halafu eti ukajitetea kuwa ulikuwa hujui kama ulivunja sheria. Hiyo kitu haipo...
 
Hoja ilivyowasilishwa na CHADEMA, then jinsi ilivyomalizwa na Tendwa ni picha tosha kwa mwenye macho kuona ni jinsi tunavyotawaliwa, tena pengine bila ridhaa yetu...! Sasa ni wakati wa kukumbuka kuwa "MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA, NA AKIAMBIWA NI TUSI". Hata hivyo, inasikitisha pale CCM wanapowaomba Watanzania ridhaa ya kuwatawala, huku CHADEMA wakiwaomba ridhaa ya kuwaongoza, then Watanzania wanatoa ridhaa ya kutawaliwa badala ya ile ya kuongozwa....!

Maamuzi yaliyotolewa na Tendwa ni taswira ya jinsi CCM ilivyojipanga kuitawala nchi hii hata bila ridhaa yao.....! Tunafahamu fika kuwa "ballot is stronger than bullet", lakini huku kwetu hii haiapply...! Tunaambiwa kuwa "nobody above the law", lakini pia it is an inverse in Tanzania....!
 
Sijasema mahali popote kuwa nilitaka anifurahishe mimi, na wala sijasema amfurahishe mtu yeyote, nimesema atueleze na kutufafanualia kifungu hicho cha sheria kinasema nini maana ndio fani yake halafu atuambie ni kwa namna gani jambo alilofanya Kikwete limekivunja ama halijavunja hicho kifungu cha hiyo sheria. Hakuna nililosema zaidi ya hapo, sasa hapa ......ly! uliyosema nitakuwa mimi au ni wewe? Umepewa akili na fikra za kufikiri lakini unakimbilia kuongelea mambo bila kuangalia kwa undani nini maana yake. Ni watu ka ninyi msiotaka kufikiri ndio mnarudisha nyuma maendeleo ya hii nchi tunayoipenda. Ushauri wa bure, soma, tafakari halafu andika. Umasikini wa kufikiri ni mbaya kuliko aina yoyote ya umasikini hata kama umejaa hela za ufisadi. Ni kansa inayomaliza Taifa hili, ni kansa iliyowakamata wengi, ni kansa inayomaliza heshima ya wanasheria maana hawajielewi hata wako wapi. Ni kansa inayomfanya mru atoe majibu mepesi hata kama yanahusu jambo linalohitaji umakini wa hali ya juu. Ni kansa inayomfanya mtu aseme " amelitupilia mbali pingamizi" bila kueleza kwa kigezo na misingi ipi.

Achana na huyo jamaa (Marigwe), ndiyo walewale akina MS kwa majina tofauti!!!
 
habari waungwana wa jamii topic yangu hi hii

Tunakujia Malaria Sugu -- kawaida yako ni kuanzapost zako na small letter. Hii ni ID ya ngapi umeisajili humu JF tangu upate kipondo siku ile na kupigwa marufuku?
 
Tayari ccm imeshinda! Upinzani wanachelewa sana kulalamika! Wafanye kampeni! Watamlaumu tendwa bureee! Hivi mabango yale ya kikwete ndi yanafanya chadema waweweseke? Kipi cha kutisha!
 
mimi nashangaa sana hivi watu mnaona chadema ndio chama bora cha upinzani tanzania? ile ni kampuni yenye sura ya kichama tu! miaka yote mitano chadema hawana mpango wa kuimarisha chama wakiona uchaguzi ndio kelele kibao,ooh tutashinda sie! oooh sisi ndio wenye demokrasia sie! wapi? hawana lolote kuishabikia chadema ni kutoelewa uchambuzi wa siasa! huwezilinganisha chadema na cuf hata kidogo,Cuf sasa wamefanikisha serikali ya mseto! haya hao chadema wana nini!!!!????????? ukabila wachaga kibaoooo na vibarua akina slaaa na wachache kufuta sooooo! mimi naona bora ccm kuliko vyama ambayo hata kujipanga hawajui na wapo kimasilahiii!!!
 
Tendwa anajikosha kwa madudu ya kutupa pingamizi


Exactly, na ni plain truth kwamba hawezi eti 'kuionya' CCM....kwani yeye yupo chama gani kwanza? mwajiri wake ni nani? a lot of conflicting interests hapa!
 
Back
Top Bottom