Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Tendwa aionya CCM kuacha kutumia nyenzo za Ikulu
BARAZA la Ushauri wa Vyama vya Siasa nchini, limekishukia CCM na kukitaka kutotumia picha zilizopigwa Ikulu katika kampeni zake.Onyo hilo lilitolewa jana na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.Tendwa, alisema hayo muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano ulivyovishirikisha vyama Baraza la Ushauri wa Vyama vya Siasa nchini.
Picha za kampeni za CCM zinazoonyesha Ikulu zisitumike, ukitumia hizo picha halafu chini yake ukasema chagua chama fulani, hiyo itakuwa siyo demokrasia kwa sababu hata aliyepiga hizo picha ni mfanyakazi wa Ikulu, alisema Tendwa.
Kwa mujibu wa Tendwa, picha hizo pia zinawashawishi wananchi kuipigia kura chama hicho na kuwa vyama vingine haviwezi kuzipata kutokana na kutoweza kupiga picha katika eneo hilo.
Mbali na kuitaka CCM iache kutumia picha zilizopigwa Ikulu, Tendwa alikita chama hicho pia kuacha kuvifanyia vurugu vyama vingine vya siasa.
Alisema CCM inawatumia vijana wa UVCCM, kufanya vurugu katika kampeni za vyama vingine vya siasa ikiwamo kuchana mabango ya wagombea na kutoa bendera za vyama hivyo.
Alikitaka chama hicho kuacha tabia hiyo mara moja.
Lakini Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni za Urais za CCM, Abdulrahman Kinana alikanusha tuhuma hizo akisema hazikutolewa na Tendwa.
Mimi nina tap (mkanda uliorekodiwa) yake, hajazungumzia hilo. Kwa sababu hiyo usiniulize kuhusu mambo ambayo hakuyazungumzia, alisema Kinana.
Kinana pia alisema ana uhakika kwamba, Tendwa hakusema kuwa vijana wa CCM wanawafanyia vurugu vyama vingine vya siasa.
Hata hivyo alipotakiwa kufafanua kuhusu tuhuma za CCM kutumia rasilimali za serikali katika kufanikisha kampeni zake ajibu: Siyo kweli."
Alisema CCM inatumia rasilimali zake yenyewe kufanikisha kampeni hizo na sio rasilimali za umma.
Baraza hilo limeonya pia juu ya kampeni chafu zinazoendeshwa na baadhi ya vyama vya siasa na likivitaka kuacha kufanya hivyo.
Baraza halijaridhika na utekelezaji wa kanuni za uchaguzi kwa hiyo limeitaka Tume na Msajili kutoa tamko pale kanuni hizi zinapovunjwa, alisema Tendwa.
Katika taarifa yake Tendwa pia aliitaka Taasisi ya Kuzuaia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) kuwachunguza wagombea wanaojitoa baada ya kuanza kwa kampeni.
Baraza limehisi kuna harufu ya rushwa katika hili, ndiyo maana wakaitaka Takukuru iwachunguze hawa watu na pia limetaka itungwe sheria itakayo wabana hawa watu, alisema Tendwa.
Baraza hilo pia liliitaka Takukuru kuwachunguza wafanyakazi wa taasisi hiyo, ambao wanavujisha siri za taarifa za rushwa wanazopewa na wananchi hali inayofanya zoezi la kuwakamata kushindikana.
Baraza hilo pia limevitaka vyombo vya habari nchini kutokuwa wakereketwa wa vyama vya siasa ili kutenda haki kwa vyama vyote.
Lakini kwa vile vya serikali tunavitaka vitoe fair play (haki sawa) kwa vyama vyote, alisema Tendwa.
Kwa mujibu wa Tendwa, Baraza hilo limetaka kutoa tamko ili ufanyike mdahalo wa wagombea urais katika vyombo vya habari kwa vile mdahalo wa sasa wa wabunge unafanyika kwa upendeleo.
Mimi kama msajili nina-encourage (ninaunga mkono) kuwepo na dialog (mdahalo) ili kila mmoja apate nafasi ya kueleza sera zake, kwa sababu baraza linaona wagombea wenyewe wapo saba tu, kwa hiyo ni bora utaratibu ukawekwa hata wakifanya wanne siyo mbaya, alisema Tendwa.
Pamoja na mambo mengine, baraza hilo lilimtaka msajili kutoa tamko kuwa hakuna chama kidogo na kikubwa kwa kuwa vyote ni vyama vilivyopata usajili kwa mujibu wa sheria.
Kutokana na agizo hilo Tendwa alifafanua kuwa hakuna chama kidogo wala cha msimu na kwamba, chama chochote kitakachotimiza masharti kitasajiliwa bila kikwazo.
Hata hivyo alisema kuwa, yuko mbioni kurekebisha kanuni ambayo itamruhusu kupandisha ada ya usajili wa vyama vya siasa kutoka Sh25,000 kwa usajili wa muda mpaka Sh500,000 na usajili wa kudumu ukitoka Sh50,000 mpaka Sh1,000,000.
Chanzo: Mwanachi