Elections 2010 tendwa afundisha somo la uraia wa watoto wa msingi

Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Apr 17, 2009
3,517
1,360
Gazeti la majira toleo la leo ukurasa wa kwanza kuna picha ya Msajili wa Vyama vya Siasa Bwana John Tendwa akifundisha elimu ya uraia kwa wanafunzi wa darasa la Tano wa Shule ya Msingi ya Bunge.

Kutokana na picha hiyo inasemekana mafunzo hayo yalizungumzia mfumo wa vyama vingi vya siasa na usajili wake wakati tukielekea katika uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani Oktoba 31, Mwaka huu.

Jamani nisaidieni, was it necessary? Kwa nini elimu hiyo asitoe kwa watu wazima wenye uwezo wa kupiga kura badala yake afundishe chekechea ambao hawatapiga kura kwa umri hauwaruhusu kupiga kura?

Je, huko sio kupoteza muda wa serikali, nadhani ingekuwa busara kama angeshughulikia vitu vya muhimu kama pingamizi la CHADEMA dhidi ya CCM

 
Labda hana kazi nying leo huko ofisini kwakee. Pingamizi la CHADEMA linamtoa jasho!
 
Back
Top Bottom