tenda ya ununuzi wa mitambo ya kuzalisha umeme kurudiwa upya

Mkora

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
370
55
Waziri wa Nishati na Madini William Ngelleja akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uamuzi wa serikali wa kuona busara ya kurudiwa kwa zabuni ya ununuzi wa mitambo miwili ya uzalishaji umeme na kuwataka wazabuni wote waliofuzu kwenye mchujo na kuthibitika kuwa wana uwezo wawasilishe takwimu za kuwezesha kufanyika kwa tathimini ya gharama za ununuzi wa mitambo, ujenzi na uendeshaji.

Zabuni hiyo inahusu Mitambo miwili yenye uwezo wa kuzalisha Megawat 100 katika mkoa wa Dar es Salaam na Megawat 60 katika mkoa wa Mwanza.Kulia ni naibu waziri wa wizara hiyo Adam Malima

Je wadau mnaweza kutujulisha yaliyowasibu hao waliopata hiyo tenda mara ya kwanza
 
Nakumbuka ilishaletwa hapa JF na mdau mmoja (simkumbuki) thread yake ilikuwa na kichwa cha habari Richmond nyingine yafukuta Tanesco kama mwezi hivi umepita. Nadhani kwa hili JF kama jukwaa la wakereketwa Pongezi zinastahili.
 
Back
Top Bottom