Tenda Mema Usahau

bagwell

Senior Member
Sep 19, 2012
113
25
Alifu hapa naanza, kwa kumuomba Manani,
Ni Yeye ndio Muweza, kila kitu duniani,
Hakuna Wakumweza, kwa hilo ninaamini,
Tenda wema usahau, usingoje shukurani.

Tenda wema wende zako, usingoje shukurani,
Yalo mema ya wenzako, yazingatie moyoni,
Usitaje mema yako, kwa fakhari duniani,
Tenda wema usahau, usingoje shukurani.

Asojuwa ya wenziwe, yafaa kutafakari,
Ajuwe yake mwenyewe, ya kheri au ya shari,
Duaze zikubaliwe, na Mungu Amsitiri,
Tenda wema usahau, usingoje shukurani.

Mtandao umetanda, kwa masomo mbalimbali,
Fungua unapopenda, chemsha yako akili,
Tovuti yenye faida, Jamiiforums asili,
Tenda wema usahau, usingoje shukurani.......

Kwa kiongozi gani anaetenda Jema akaondoka?....hakuna hata kiongozi mmoja katika Nchi hii asietaka shukurani...

 
Wakuu nimeyasema hayo kwa sababu kuna baadhi ya viongozi au baadhi ya watu wakitaka hata kutoa pipi wanataka waoneshe kwenye luninga au magazetini..hivi tabia kama hii tutaiwacha lini?...........
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom