Tembo kubaki kwenye historia kama dinasaurs

Shoo Gap

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
246
71
Kuna kila dalili Tembo kuwa history kama Dinasaurs. Kwa wiki moja(23/10/2012 & 29/10/2012) meno ya tembo yamekamatwa sehemu mbili na yote yametoka Tanzania. Ni matokeo ya Corrupt(Kifisadi) society

[h=3]MENO YA TEMBO KUTOKA TANZANIA YAKAMATWA HONG KONG[/h]


121020083223-hong-kong-ivory-bust-story-top.jpg


Hong Kong authorities confiscated $3.4 million ($26.7 million in Hong Kong currency) worth of ivory found in two shipping containers this week.


The illegal goods weighed more than 8,000 pounds, making it one of the biggest seizures of ivory in Hong Kong.


The containers arrived from Tanzania and Kenya, according to Hong Kong customs officials. The agency seized a total of 1,209 pieces of ivory tusks and three pounds of ivory ornaments from the two containers.


iHong Kong Customs was on alert after a tip-off from Guangdong officials in China. On October 16, Hong Kong officers inspected a container from Tanzania claiming to carry plastic scrap and found $1.7 million worth of ivory. A day later, a second container from Kenya was seized with ivory valued at $1.7 million, according to Hong Kong Customs.


Seven people, including one Hong Kong resident, have been arrested by Chinese authorities in connection to the cases, said a customs spokeswoman.


Hong Kong is viewed as a transit point for the illegal ivory trade, feeding into increasing demands in China, according to a Time article published this week.


Elephants are being killed in Africa at an alarming rate as international demand soars for ivory. Much of the demand comes from increasingly affluent Asian countries, particularly China and Thailand.


The last major bust in Hong Kong occurred in 2011, when officials seized a shipment of ivory and rhino horns valued at $2.2 million in Hong Kong dollars. Priest embroiled in ivory smuggling controversy. Will elephants still roam earth in 20 years?

[h=2]Pembe za mabilioni zamakatwa jijini Dar[/h]


BY MWANDISHI WETU



30th October 2012












*Zilikuwa zikisafirishwa kwenye jeneza
*Za kutwa kwenye nyumba jijini Dar




Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limekamata shehena ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh. bilioni 2.15.

Aidha, watu wanne wanashikiliwa kwa tuhuma za kukutwa na shehena hiyo.

Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Suleiman Kova, jana aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwamba, shehena hiyo ni vipande 214 vya meno ya tembo na mifupa mitano ya mnyama huyo yenye uzito wa kilo 450.6.

Alisema watuhumiwa hao walikamatwa eneo la Kimara Stop Over juzi baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kwamba kuna nyumba inashukiwa kuwa na mali zilizoibiwa pamoja na nyara za serikali.

Kamanda Kova aliongeza kuwa, baada ya Jeshi hilo kupata taarifa lilijipanga na kuipekua nyumba hiyo aliyopanga Peter Kami ambaye anaishi pamoja na Leonida Kabi na kukuta vipande 214 vilivyokuwa vimehifadhiwa kwenye chumba kimojawapo.

Alisema meno hayo yalikutwa yakiwa yamehifadhiwa kwenye magunia 12 huku yakiwa yamefunikwa kwa bendera ya Taifa.

“Pamoja na meno hayo, pia zilikutwa pembe za ng’ombe 10 zikizokuwa zimeshindiliwa pamoja na chokaa, pamoja na mifupa ya tembo mitano, yenye kilo 450.6,” alisema Kova.

Aidha, Kamanda Kova aliwataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni pamoja na dereva wa daladala aliyekuwa akijifanya kuwa ni ofisa wa polisi aliyejulikana kama Polisi Simoni (42), Charles Wainaine (41), mkazi wa Rombo Tarakea, ambaye ni ndugu yake na Peter Kabi, ambao wote ni Wakikuyu kutoka nchini Kenya.

Kamanda Kova alifafanua kwamba uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa watuhumiwa hao ni wahalifu wazoefu katika matukio ya mtandao wa ujambazi, usafirishaji, pamoja na umiliki wa nyara za serikali.

“Mpango wa siri uliokuwepo ni kutumia gari aina ya Coaster, iliyokuwa iendeshwe na dereva Polisi Simon na kuweka jeneza lenye meno hayo na kulifunika na bendera ya Taifa ili ionekane wanasafirisha maiti ya mtu maarufu serikalini kwa lengo la kuvihadaa vyombo vya dola,” alisema Kamanda Kova.

Kwa mujibu wa Kova, mtuhumiwa Leonida Kabi, anashikiliwa kwa kosa jingine ambalo ni kumshawishi askari aliyezikamata nyara hizo kwa kutaka kumpa rushwa ya Sh. milioni 15, na kuahidi kuwaongezea kiasi kingine siku ya pili yake.

Aidha alisema kuwa uchunguzi wa kina utafanyika ili kubaini mtandao mzima wa wizi wa nyaraka za serikali hapa nchini pamoja na nchi za Kenya na Mashariki ya mbali na popote duniani ili kukomesha uhalifu huo.

Watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, kiasi hicho cha meno ya tembo ni sawa na tembo 91 waliouawa.

Aidha, kukamatwa kwa meno hayo kunakuja siku moja tu baada ya Waziri Kivuli wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa, kueleza kwamba mwendelezo wa matukio ya kuuawa kwa tembo ni matokeo ya kuwalinda majangili badala ya kuwachukulia hatua.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi jijini Dar es Salaam Mchungaji Msigwa alimshauri Rais Jakaya Kikwete kuingilia kati na kuvunja mtandao wa ujangili ili kunusuru wanyamapori na maliasili nyingine za Taifa.

Mchungaji Msigwa ambaye pia ni Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), alisema mpaka sasa ni miezi mitatu tangu alipowasilisha taarifa za ujangili bungeni na kumtaka Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, achukue hatua dhidi ya majangili hao na matokeo yake amewaajibisha watu watatu wa Idara ya Wanyamapori huku watuhumiwa wakubwa wakiachwa jambo ambalo alidai ni hatari na kusababisha idadi ya wanyama kupungua kila wakati.

Alisema wiki iliyopita pembe za ndovu zenye uzito wa tani nne kutoka Tanzania na Kenya zenye thamani ya Sh. bilioni 2.5 zimezipotiwa kukamatwa na vyombo vya usalama vya mamlaka ya Jiji la Hong Kong.

Katika Mkutano wa Bunge uliopita, Kambi ya Upinzani bungeni pamoja na maoni ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira iliwataja vinara wa ujangili akiwemo Bryson Baloshingwa ambaye ni kiongozi wa mtandao wa ujangili kwa kufadhili uwindaji wa faru na biashara haramu ya meno ya tembo; uharamia unaofanyika katika hifadhi za Serengeti, Katavi, Tarangire, Ziwa Manyara na Ngorongoro.

Alisema Baloshingwa anafadhili pia majangili wanaoua wanyama katika mapori ya akiba ya Ugalla, Rungwe, Moyowosi na Maswa.

Alisema inashangaza kwamba wafadhili na majangili wanafahamika kwa majina lakini hawachukuliwi hatua na pindi wanapokamatwa hufunguliwa kesi rahisi zenye dhamana hivyo huachiwa kwa dhamana.

“Usalama wa tembo uko hatarini kutokana na serikali kutochukua hatua dhidi ya ujangili wa tembo pamoja na taarifa hizi kuwepo serikalini na viongozi wa CCM kushiriki katika ujangili," alisema.




 
kwa hali ilivyo sasa ndani ya ccm na serikali kuu hakuna cha maana kitakachofanyika kulinda tembo wetu na maliasili nyinginezo, madini yatazidi kuibiwa wanyama watazidi kuuwawa watuhumiwa hawatafanywa kitu kwakuwa kila mmoja amechanganyikiwa akijipanga kulinda ulaji wake baada ya 2015
 
Kagasheki anachukuliaje hili suala.??naona yupo kimya wala hajishughulishi kanakwamba suala lenyew ni dogo tu.au mzigo ulikua wa bosi wake???kweli anae suport sisiemu analaana na hajui atendalo.
 
Back
Top Bottom