Television ya Taifa la Tanzania haina habari juu ya Mauaji ya Askari Dar na Mchungaji Buseresere

Ta Muganyizi

R I P
Oct 19, 2010
5,361
2,734
Kwa mara nyingine tena kama ilivyotokea Meli kuzama bahari ya Hindi huku TBC wakipiga Taarabu, ndivyo ilivyokuwa leo ambapo watanzania wengi waliosikia tukio la Ugomvi wa kidini huko Buseresere Wilayani Chato mkoa wa Geita walitegemea kuuona ukweli katika television ya Taifa ambayo inashikika hata kwa eria huku vijijini. Tulitegemea kuoneshwa walau kiongozi wa serikali akikemea suala hili na kusisitiza mshikamano miongoni mwa Watanzania. Badala yake wamekaa kimya kana kwamba kilichotokea ni sahihi.

Pia hata mauaji ya askari yaliyotokea kule Tazara TBC haina habari. Television ya Taifa hii imewaonesha watanzania mtoto wa Uingereza aliumwa na mbwa akakatwa kidole chake kimoja wakati Watanzania wawili wamekufa. Serikali kumbe haijali na wala haioni kuna haja ya kukemea kinachoendelea. Hapa nimeshangaa sana. Wananchi walikimbia kuangalia taarifa za habari hata kwa majirani hawakuona kitu. Kwa hali hiyo walioguswa wanapanga kuenda kulipiza kisasi maana serikali haijali suala hili kama ambavyo imekuwa makini kuongelea maandamano ya vyama vya upinzani.

Kwa akili yao mbovu wamekauka ili watanzania wengi wasijue lakini wanajidanganya. BBC inasikika kote hata mipakani ambapo redio za kenya , Uganda, Rwanda zinajiunga na tunasikia sana. Nchini mwetu chombo kikuu cha habari nchini wala haijakemea suala hii. Watu wazindua maajabu saba ya Africa na wengine mikutanoni wala hawana habari na kinachoendelea. Wanacheka cheka tu. Natamka rasmi kuwa hawa vijana walioko TBC ni wapumbavu na familia zao zione aibu kwa hili.

Kipindi kile wakati Afrika kusini wanapigania uhuru mwanaharakati mmoja alipokuwa ananyanyaswa na makaburu aliwahi kuwaambia kuwa niteseni sababu naipigania nchi yangu.......akasema kuwa hata wanangu watakuja kusema kuwa baba ni mtu aliyekuwa na uwezo wa kutetea na kusimamia alichokiamini kuwa ni kweli................kisha akamuuliza Kaburu....wewe wanao watajivunia nini kwako? Nawauliza vijana mlioko TBC wanenu wajivunie nini. Bwigane, Ahmed Salum, Mbozi Katala, Gabriel Zacharia na wengineo......mmefikia amri ya kuamrishwa kama mfugo mmoja ufugwao na binadamu ambao ukiambiwa shikaaaaaaaaaaaaaa............ ..........unakimbia na kung'ata bila hata kuhoji makosa ya anayeng'atwa. Mkikuta wanaume wanaongea wala msichangie mada. Hamna tofauti na ma house girl/boys mbele ya father/mother house ndani ya nyumba.

Naamini kuwa " It is better to be poor but free rather than being rich but a slave"

Ili mjue kwamba kulazimishana kuamini ambacho sio hadi mtu kufa ni jambo baya............



Hata hii TBC yetu imewashinda..................
 
Last edited by a moderator:
hii ni redio ya chama n a serikali.ila kodi zetu ndio zinaendesha hii radio,sijui kwanini hawatoi habari latest
 
hii ni redio ya chama n a serikali.ila kodi zetu ndio zinaendesha hii radio,sijui kwanini hawatoi habari latest

Mkuu television....tumekimbizana migombani hadi kwa majirani wenye erial walau za tube light ili tuone TBC lakini wapi....tumeona mtoto aliyeng'atwa na mbwa kidole Uingereza na kuambiwa kuwa anaendelea vizuri
 
Mkuu umechukia, tbc na psychokolojia za viongozi wake wanaamini kuwa kuonesha matukio hayo wanaongeza kasi zaidi hivyo ni heri kukaa kimya. Huu ni upuuzi, psych kama hii ktk utandawazi huu imepitwa na wakati. Kwao matukio sahihi ni yale ccm. Inasikitisha.
 
Na yule mzee wa pozi marin hassan yupo
Hao ni majuha tu hawajitambui..ndoo mana walimtoa T.do ili wabaki ma kina ndio mzee.
 
yaani wewe na ukamanda wako wote huwa unaangalia tbccm hovyo kabisa..

Mkuu mimi kuona sio Tatizo wananchi.....waliofurika kuicheki hii ndo wanaumia. Kitendo cha kutokemea ndo kibaya. Pia lazima tuangalie tuone inavyowadanganya wananchi ili tuwaelimishe.
 
Sina hakika kwamba wamelazimishwa kuwa hivyo, lakini ninaona wao kukosa hekima na weledi. Utaachaje kutoa habari muhimu Kama hii kwa wananchi ambao wanasubiri kupata taarifa. Kuna maeneo katika nchi yetu na pila watanzania walio nje ya nchi wanategemea TBC nayo kila Mara inawaangusha!Ni muda wajirekebishe, wanatuangudha. Nilidubiri kupata taarifa baada ya kuwa nimesikia habari hizi mbili kutoka kwa jamaa zangu lakini all in vain.
 
Hivi hii TV bado iko hewani? Nilishaitrash!!!

ipo inawadanganya wananchi.............kuwa BBC niwazushi hakuna aliyekufa buseresere maana wamekaaa kimya. Habari za Buseresere Tanzania tunzipata Tanzania na Sio London...........kama ilivyokuwa leo
 
Me sitaki habari za tbccm leo walikuwa live kuonesha mambo ya maajabu 7 ya afrika arusha na kwakua mtoto wa mkulima alikuwepo..... habar ya tazara wakati wapo karibu sana na hapo kwa TBC TAIFA ilikuwa rahisi sana ku cover story hiii.......

Ngoja majibu ya ili likitu yatapatikana 2015......

al-jazzera, channel10 na citizen uone mambo mazito ambayo JK 2010 ALISEPA..
 
Sina hakika kwamba wamelazimishwa kuwa hivyo, lakini ninaona wao kukosa hekima na weledi. Utaachaje kutoa habari muhimu Kama hii kwa wananchi ambao wanasubiri kupata taarifa. Kuna maeneo katika nchi yetu na pila watanzania walio nje ya nchi wanategemea TBC nayo kila Mara inawaangusha!Ni muda wajirekebishe, wanatuangudha. Nilidubiri kupata taarifa baada ya kuwa nimesikia habari hizi mbili kutoka kwa jamaa zangu lakini all in vain.

Pole sana hii ni mbaya sana. Aibu kwa kizazi cha sasa cha vijana......walioko TBC kugeuzwa puppy
 
Hivi hii TV bado iko hewani? Nilishaitrash!!!

Mkuu,

Hii tv ni yetu-walipa kodi na wewe ukiwemo. Kuwaachia hawa jamaa watanganze wanavyotaka ni sawa kukataa kwenda kupiga kura kwa kiongozi umtakae. Sio uzalendo kutoingslia na si uzalendo kutotutanganzia yanayoendelea nchini. Suluhisho ni kuwaambia ukweli ili watimize wajibu wao
 
Pole kamanda, hata Jana nilikwambia achana na TBCCM. Hata waki report si ajabu wakatoa taarifa za uongo kutegemea jinsi wanavyoelekezwa kuandika.

Kesho ndipo wata report baada ya kupata maelekezo Na ku edit.
 
Hata ITV na Capital hawajaonesha; ingawa si za Taifa.

Kodi yangu haimlipi mfanyakazi wa IPP directly bali inamlipa wa TBC................kila mwezi na mshahara wangu mdogo nakatwa 105,000/= kama kodi ya mapato. Wala Capital huku hatuooni inaonekana TBC, wao ITV/CAPITAL ni hiari yao kutangaza lakini si TBC........
 
Back
Top Bottom