Telegraph From Iddi Amin Dada kwa Nyerere Kisa cha Vita ya Kagera?

Duduwasha

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
5,703
3,653
Nimejaribu kuisoma na kutafakari hii telegraph(Simu ya Maandishi) ... na nimejiuliza maswali bila kupata jibu je inawezekana ilimuudhi sana j.k Nyerere(r.i.p) hadi akaamua potelea mbali kama vita ipigwe na aonekane na Mwanamume! nchi haijasiamama hadi leo hii Dollar ya mmarekani ilikuwa haipishani na Shillings Yetu....

Hebu isomeni kwa wale waliokuwa hawaijui na Tujadili... Nilishawahi sikia kuwa Iddi Amin aliitizama Tanzania Nzima akasema Anaona wanawake tu na mwanamume ni mmoja tu Mti Mkavu Gen Mayunga(r.i.p)... nadhani nchi hii ilipigana vita kwa sababu ya Matusi tu ya Iddi Amini Dada

A telegraph from Idi Amin Dada to Julius Nyerere: "I want to assure you that I love you very much and if you had been a woman I would have considered marrying you, although your head is full of grey hairs. But as you are a man, that possibility does not arise"

598624_515412845149473_21314379_n.jpg
 
Nimewahi kusikia kuhusu haya matusi. Amin alimdharau sana Nyerere na Tanzania kwa ujumla. Tulimpiga ili kulinda hadhi ya nchi yetu. RIP BABA WA TAIFA. TUTAKUKUMBUKA KWA USHUJAA WAKO
 
Si hilo tu, Idd Amin alikuwa fedhuri sana dhidi ya Mwalimu, tulifikia hatua ya kumchapa baada ya kutukaa kichwani kwelikweli
 
Kumbe vilikuwa vita vya kibinafsi! vikituacha wengine kulipia hadi leo hii,achilia mbali waliomwaga damu zao, walioachwa wajane, watoto walioingizwa katika uyatima...
 
duh hii ilikuwa ni dharau kubwa sana kwa mwl.....wale mabingwa wa kubadili signatures chukueni hiyo.
 
Ingekuwa hivyo, matusi ya nguoni yasiokuwa na maana yoyote binadamu anayotukanwa kila kuchao angeamua kutoyadharau na kuyafanyia kazi, mapigano yangetamalaki hapa duniani!
 
Kumbe vilikuwa vita vya kibinafsi! vikituacha wengine kulipia hadi leo hii,achilia mbali waliomwaga damu zao, walioachwa wajane, watoto walioingizwa katika uyatima...

Hivi upi uelewa wetu kwenye national security issues? Kwanini tulikwenda Comoro? Kwanini tulitaka kwenda Congo?
 
Duh hii haijakaa vizuri, ina maana Mzee wetu alikua kama Kopa?
 
Source yake ni nin.napo idd alikuwa na dharau sana.

ebu fikilia km zile vulugu za mbagala na kaliako angekuwepo mkapa madarakan asingevumilia pia namin ht huo ujumbe ungemkuta kipindi cha mwalimu laziba tu angemuadhibu.

ona jk pamoja na0matamko alishindwa kuzihilisha nguvu ya dora
 
Hiyo telegraph ni ya kweli kabisa na source yake ni ile documentary ya maisha ya idd amin,ni kweli kabisa nyerere hakumjibu
ila idd amin alifanya hivyo kwa sababu alikuwa hana namna ya kuminsult nyerere kutokana na vitendo vya uchokozi vilivyokuwa vinafanywa na tz wakati huo dhidi ya serikali yake,ndiyo ili kumuumiza ikabidi awe ana mtukana mara kwa mara kuonyesha kutokuridhika kwake na vitendo hivyo vya nyerere.
 
Nimejaribu kuisoma na kutafakari hii telegraph(Simu ya Maandishi) ... na nimejiuliza maswali bila kupata jibu je inawezekana ilimuudhi sana j.k Nyerere(r.i.p) hadi akaamua potelea mbali kama vita ipigwe na aonekane na Mwanamume! nchi haijasiamama hadi leo hii Dollar ya mmarekani ilikuwa haipishani na Shillings Yetu....

Hapo kwenye nyekundu nani alikuambia?
 
Kumbe vilikuwa vita vya kibinafsi! vikituacha wengine kulipia hadi leo hii,achilia mbali waliomwaga damu zao, walioachwa wajane, watoto walioingizwa katika uyatima...

Kwa hiyo mkuu unataka kusema kuwa Kagera iliyotekwa na Iddi Amin ilikuwa ni mali yake binafsi Nyerere?
 
Jamaa alikuwa jeuri kwelikweli, na sipati picha kama vita vile tungeshindwa ingekuwaje...!!
 
Jamaa alikuwa jeuri kwelikweli, na sipati picha kama vita vile tungeshindwa ingekuwaje...!!

Iddi Amini hakuwa na kitu kichwani. Uliotisha ulikuwa mdomo. Maamuzi yake mengi yalikuwa ya ajabu ajabu kwa hiyo kwa hakika hakuwa na uwezo wa kushinda vita ukizingatia hakuwa na sapoti ya kutosha toka ndani ya uganda yenyewe.

Kwa kifupi angekuwa na akili asingekuwa na maneno ya namna hii
 
Kumbe vilikuwa vita vya kibinafsi! vikituacha wengine kulipia hadi leo hii,achilia mbali waliomwaga damu zao, walioachwa wajane, watoto walioingizwa katika uyatima...

Imagine wewe ni mkuu wa nchi. Mkuu wa nchi nyingine anakutukana kiasi hicho na ukanyamaza eti ni vita binafsi...kwangu haiingii akilini. Nitampiga na wananchi wangu watanisupport kuondoa dharau kwa kiongozi mkuu wa nchi.
 
Back
Top Bottom