Teknolojia ya Digitali ya Startimes na Ting: Kero za watumiaji

Halafu ndio nimenunua vocha hapa ya star times tulionunua mwanzoni mbona clear tu ,hakuna kugomagoma!

Mie natumia king'amuzi[decoder] cha hawa "EASY TV" naona watu wengi hawakijui, ila ni wazuri saaaana. Channel zote za tz zinapatikana, na znz, kenya-KTN, CITIZEN., Uganda-UBC, ALJAZEER,CNN, BBC, CCTV1 & 2, zakidini-christo ipo EMMANUEL ya nigeria na muslim ipo PEACE TV, NA za movie kibao. Gharama ya decoda sh 140,000/- na ada ya mwezi sh 9,000/-simu yao customer care ni- 0658688633. Hamia easy tv.

inaonyesha hiki kiko vizuri sana!vp kinapatikana mikoa yote?au ni baadhi ya mikoa tu km ilivyo star times na Tin!

Startimes ni wezi,wameweka channel za ovyo kabisa,wanazidiwa na cable tv za mikoani,wakienda miji kama Bukoba hawapati kitu,hakuna channel nzuri ya movie,ile MGM zimejaa old skul tu! Hela ikiisha silipi tena !

channel kama Emanuel tv,HBO,Star Movies,My tv,Ten sports n.k mbona zingeongeza walau thamani ya kuangalia tv.wachina wametuingiza mkenge hawa.

Tatizo lenu mnakurupuka then mnatoa lawama za ajabu...wana vipeperushi vinavyoonyesha chanel zilizomo,.kabla ya kununua mngezichunguza kwa waliokua nao kabla ndipo mnunue au la...binafsi nilichunguza huduma zake nikaridhika ndipo nikanunua...sina fav. Chanel lakin napenda baadhi ya vpndi km vile navy seals clas 234(discovery),inside story(aljazeera) na most of reality shows za E!...

Pole sana!!unakaa wapi wewe!mimi kwangu haigomi..jana mtv ndio ilikuwa inagoma goma muda wa videos and music awards..leo furesh kabisa.

heheeee we acha tuu mi yangu karibiaa natupa huko inagomagoma mara zote

channels za hooovyo wanarudiarudia movies

sibuka na kbc1 zinasauti mbili unaona movie af unasikiliza reggae

stupid zao

Kwenye rimonti bonyeza batani ya Track,utaingia kwenye setting ya audio ni rahisi tu!
Tatizo la hawa startimes wameokoteza chanels za bure huko halafu wanatuuzia sie na chanels maana wameshindwa kuzinunua!!

Mambo yote DSTV -Extra view wakuu hao wachina kavu sana promo kibao kumbe 0 kabisa

Nimenunua decoda ya STARTIMES ni kama nimepoteza hela yangu. Wakati inafanyakazi inagomagoma. Nimewauliza inakuwaje hali hii, wanasema ni antena. Nimebadilisha antena kwa kununua ya kwao, hali ni hiyohiyo. Vipindi vyenyewe havikidhi haja kabisa, kwa ujumla vingi havipendezi.

Wakati huohuo natoa wito kwa mamlaka ya mawasiliano kuhakikisha decoda zote zinakubali kadi za tv zote. Ili mtu anunue decoda moja itayoingiliana na kadi zote kama ilivyo sim kadi za simu na simu zenyewe.

Kitendawili, kulipia hudumu hatutaki lakini huduma bora tunataka!
License za kurusha vipindi vizuri ni gharama jamani, msifikiri unajirushia tu.

Mamlaka zipo wapi kuhusu ubora wa picha? Au wachina hawahusiki na TBS? mie changu sikitizami kwani dakika tano tu macho yanaanza kuuma tofauti na Cable TV (CTV) yangu hata Local Channel Na nikienda kwenye Holiday inn kutizama Soccer huwa Fresh Macho hayaumi.

Hata kama wapo bei chini ndio waumize watu macho na pia channel zao zina vipindi vibaya na ni mbaya. Walishawahi kutudanganya Kuwa TBC2 ni ya Sports lakini kila ukichungulia utaona music! nilinunua mwanzoni offer ilipoisha sikuweza lipia tena hadi august 2011 nadhani ndio itakuwa mwisho hadi watakapo ongeza channel za ukweli.

Waboreshe picha na kuongeza channel zenye mvuto sio za sasa hivi ukitizama unasinzia

Startimes ni hovyo kabisa sijapata ona,wameokoteza chanel za bure halaf wanatuuzia.chanel ya maana pekee waliyonayo ni discovery.halaf walivyowapuuz watuwekea na channel zinazorusha matangazo kwa kifaransa eg.animax na voxy .nimeamua kutupa kapun kingamuz chao nimenunua dish la inch 6 (FTA) nimefunga LNB kubwa moja 4 local channel na KU(LNB ndoggo) mbili for internation channel nimepata stations 97 pamoja na radio zote za kibongo zilizo kwenye satelite na za nje radio 73 ikiwemo za e.africa.yaani raha tupu.

We kwani ulilazimishwa kununua,maana yake wana vipeperushi vyao vinaonesha chanell zote zilizopo. KUKURUPUKA KWAKO(KWENU) KUMEKUPONZA. Holy crap!

Back
Top Bottom