Tegeta Nyuki - Bahari Beach - Ujenzi wa Barabara na MATUTA!

Obuntu

JF-Expert Member
Feb 6, 2008
510
34
Katika pitapita zangu jana nilibahatika kufika maeneo ya Tegeta na kwa kuwa niliambiwa kuwa mida ya jioni saa 12 hadi saa 2 usiku kuna foleni kubwa Tegeta Kituoni niakaamua kupitia barabara ya "kuzungukia" maeneo ya Bahari beach na kutokezea Tegeta Nyuki.

Takribani miezi mitatu iliyopita hii barabara ilikuwa "rough" sana lakini majuzi niliambiwa kuwa imewekewa kifusi na inapitika vizuri!

Ambacho kimenishangaza katika hii barabara ni kuwa baada ya kuchongwa na kuwekewa kifusi wakaazi waliopo kando kando ya hii barabara wao wamejitolea kuweka "road bumps" wenyewe! Na kinachoshangaza zaidi hizi "road bumps" zipo kila baada ya mita kama 5 hivi kutoka moja kwenda nyingine!

Sifahamu ni kwa nini wameamua wao "kuisadia" serikali katika kutimiza wajibu wake, tatizo langu ni kwanini wao wameonelea "road bumps" is all that they can contribute on na ziwe karibu karibu kiasi hicho!

Nawasilisha

Obuntu
 
Back
Top Bottom