Tecno kutoa Phantom 6 Septemba hii, itathibitisha ubora wake?

TECNO Tanzania

Senior Member
Jul 6, 2016
192
216
Kutoka kwenye Blogs.......

Tecno kutoa Phantom 6 Septemba hii, itathibitisha ubora wake?

Sio suala jipya kwamba Bara la Afrika limegubikwa kwa kishindo na ulimwengu wa Smartphone (vijana wa mjini wanaziita simu janja). Ulimwengu huu umeshuhudia mapinduzi makubwa ya kiteknojia kwenye simu za mkononi. Urahisi huu umeonekana kwenye manunuzi, mahusiano, ajira, kupata taarifa kwa haraka zaidi n.k. Kampuni kubwa ya kutengeneza simu, TECNO, imegusia mwendelezo wa simu zake kali za PHANTOM mwezi wa Septemba.

Nimefuatilia kwa makini matoleo ya PHANTOM na kugundua kwamba bidhaa zao zimekuwa zikiwalenga watumiaji wa maisha ya kati. Sasa wanagusia kwamba toleo lao jipya litawalenga watumiaji wa maisha ya juu.

Swali linakuja... Je! Wataweza kuliteka soko Septemba hii? Kwa jinsi mambo yanavyoonekana, lengo hili linaweza kufikiwa au kuvukwa.

TECNO PHANTOM 6 itakuwa nit oleo jipya la TECNO lenye vitu vingi vya kuangaliwa katika teknolojia nzima ya utengenezaji wa Samrtphone

Betri inayochaji kwa haraka
Huu umekuwa ni wimbo wa taifa kwa watumiaji wa Smartphone. Sawa, kuna vitu vingi vya kufurahia lakini tatizo linakuja kwamba simu haikai na chaji sana. Inapokuja kwenye PHANTOM 6, port yake ya Type-C 2.0 USB ina uwezo wa kuchaji simu yako kutoka 0% mpaka 35% ndani ya dakika 10 tu.

Kamera ya mbele (13MP) + Kamera ya nyuma (5MP)

Sasa hapo ni mwendo wa kutwanga selfies na picha kali ukiwa na kamera zenye uwezo wa hali ya juu mbele na nyuma. Picha hizi zenye ubora wa kipekee zinazoongeza rangi na uhai kwenye matukio yako ya kukumbukwa huku zikikutoa mwakemwake kama vile haujapatwa na jua.

Muundo wa chuma

Habari nilizozipata kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika ni kwamba, TECNO Phantom 6 itakuwa na ‘kava’ la chuma lilitengenezwa kwa umahiri wa hali ya juu na watu wanaoipenda kazi yao.

Umbo Jembamba
Inasemekana kuwa TECNO Phantom 6 itakuwa miongoni mwa simu nyembamba zaidi kutengenezwa duniani. Yaani utafikiri aliyekuwa anabuni muundo alikuwa kwenye ‘diet’

Bei

Ingawa TECNO Phantom 6 inategemewa kuwa ni miongoni mwa Smartphone zenye ubora wa hali ya juu, wataalamu wa mambo wanasema kwamba bei yake haitapishana na mfuko wa mwananchi.

Tusubiri kuona zaidi maujanja ya Phantom 6, endapo unahitaji taarifa zaidi unaweza kutembelea mitandao ya kijamii ya Tecno kama ilivyoorodheshwa hapa chini.

Facebook: TECNO Mobile | Facebook

Instagram: TECNO Mobile Tanzania (@tecnomobiletanzania) • Instagram photos and videos

Twitter: TECNO Mobile TZ (@TECNOMobileTZ) | Twitter
 
Tecno1.PNG
 
Attachments

  • Tecno3.jpg
    Tecno3.jpg
    6.8 KB · Views: 66
Tecno kutoa Phantom 6 Septemba hii, itathibitisha ubora wake?
Sio suala jipya kwamba Bara la Afrika limegubikwa kwa kishindo na ulimwengu wa Smartphone (vijana wa mjini wanaziita simu janja). Ulimwengu huu umeshuhudia mapinduzi makubwa ya kiteknojia kwenye simu za mkononi. Urahisi huu umeonekana kwenye manunuzi, mahusiano, ajira, kupata taarifa kwa haraka zaidi n.k. Kampuni kubwa ya kutengeneza simu, TECNO, imegusia mwendelezo wa simu zake kali za PHANTOM mwezi wa Septemba.

Umbo Jembamba
Inasemekana kuwa TECNO Phantom 6 itakuwa miongoni mwa simu nyembamba zaidi kutengenezwa duniani. Yaani utafikiri aliyekuwa anabuni muundo alikuwa kwenye ‘diet’

Tecno3.jpg
 
Mi tecno nawapenda sana upande wa baterry ni shida pia camera ziko poa sana mi natumia w3 iko poa sana ila ukiupdate inakua fasta na kucharge ni usiku tu. Mchana ni H+ kama kawa
 
phantom 5 ilikuwa dissapointment sana kama unaweza kuwaambia wakubwa zako hizi ni constructive criticism
1. huwezi ukawa na simu ya flagship kama hio halafu ukatumia processor za cortex a53 wakati kuna simu hadi za dola 150 zina soc zenye nguvu kuliko simu zenu za laki 8
2. gpu zenu ni ndogo phantom 5 ilikuwa na mali t760mp4 kama sijakosea huku ikiwa na kioo full hd ambacho hakiendani na hio gpu
3. flagship yenu hamjaipa update wakati low end c8 mumeipa sidhani mtu alietoa laki 8 yake atajiskia vizuri
4. bei zenu ni kubwa kuliko munachotoa, flagship za china zenye specs kali zaidi ya simu zenu zinauzwa rahisi zaidi simu kama xiaomi mi5, one plus 3, meizu pro 6, etc
 
tecno mpo vizuri nawashauri punguza bei ya simu zenu ili watu wa hali ya chini wamudu kununua.
 
phantom 5 ilikuwa dissapointment sana kama unaweza kuwaambia wakubwa zako hizi ni constructive criticism
1. huwezi ukawa na simu ya flagship kama hio halafu ukatumia processor za cortex a53 wakati kuna simu hadi za dola 150 zina soc zenye nguvu kuliko simu zenu za laki 8
2. gpu zenu ni ndogo phantom 5 ilikuwa na mali t760mp4 kama sijakosea huku ikiwa na kioo full hd ambacho hakiendani na hio gpu
3. flagship yenu hamjaipa update wakati low end c8 mumeipa sidhani mtu alietoa laki 8 yake atajiskia vizuri
4. bei zenu ni kubwa kuliko munachotoa, flagship za china zenye specs kali zaidi ya simu zenu zinauzwa rahisi zaidi simu kama xiaomi mi5, one plus 3, meizu pro 6, etc
Aliyetoa post anaonekana ni market manager, anacchojua ni size ya kamera na vitu vidogovidogo, hawezi jibu hizo nondo mnkuu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom