Technology: Cheating made simple!

Masaki

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,463
752
Wadau,

Maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano ya habari imefanya usaliti katika ndoa na mahusiano kuwa rahisi sana. Zamani ilikuwa vigumu sana kutongozana kwa kuwa ilikuwa ni lazima muonane na muwe mtaa, ofisi au sehemu moja kwa wakati huo.

Siku hizi kwa sms, BBM, facebook, twitter, emails na kadhalika, mambo yamerahishwa sana. Ndio maana hata uaminifu kwenye mahusiano umekuwa TESTED sana. Mwanamke aliyekuwa anaonekana muadilifu katika ndoa miaka ya 80 kwa kuwa tu hakuwa na jinsi ya kuwasiliana na anaotamani ku cheat nao, leo hii ata cheat tu kwa kuwa cheating iko kwenye damu yake.

Kwa hiyo yale mambo ya eti zamani kulikuwa na maadili sana sio ya kweli kivile. Ni kwa kuwa kulikuwa na kikwazo kikubwa katika mawasiliano na ndio maana hakukuwa na kasi kubwa ya CHEATING!!

Sio mtazamo wangu, huo ndio ukweli!
 
Tueleze uzoefu wako ukoje. We uliwahi kucheat online hadi kufika hatua ya kuvunja amri ya sita au unasikia ya watu. Kwa upande wangu sijawahi na sitegemei kwa sababu sometimes huwa nahisi kuwa huenda ninaochati nao si watu - ni majini.
 
Kama una imani kama hizo basi hata hapa JF usingekuwepo. Maana hapa kuna majina bandia kwa hiyo kwa mtazamo wako wa kiimani, that is even worse!!
 
Kweli kabisa.
Uhaba wa vitu unaweza kuuficha uhalisia wa watu. si tunaona, mtu anakuwa muadilifu ila akipata ayatakayo hubadilika.
Mf. mtu anaonekana mwemw sababu y umasikini wake ila siku mambo yanapokuja kumnyookeya anaonyesha ule uhalisia wake kuwa yeye ni mtu mwenye kiburi na dharau.
Hivyo na kwa hata waliokuwa waaminifu kipindi hicho, ni kwasababu tu ya kutokuwa na njia za urahisi za kufanya wanavyotaka.
 
ni kweli kabisa, mawasiliano yamefanya dunia kuwa ndogo, unaweza kuwasiliana na mtu hata kwa sms mbele ya mume au mke na mkapanga mipango yenu yote ikakamilika bila mtu kujua. lakini zamani hali ilikuwa tofauti ilikuwa inataka ujasiri wa kutosha kusimama vichakana eti mnatongozana na msionwe na watu na hiyo ilikuwa inapunguza sana wizi wa mapenzi lakin siku hizi unaweza kujipinda kwenye laptop wenzio wakadhani uko bize na kazi kumbe una chati na mupenzi! na ndio maana ukitaka kuhatarisha uhusiano na boyfriend/girlfiend, mchumba, mume au mke basi pekua kifaa chake cha mawasiliano iwe simu au computer yake kama una access nayo lazima utoke na jambo ambalo litakuwa mwanzo wa ugomvi au kutokuaminiana tena.
 
teh teh teh
Masaki bwana

Na mie ningependa kusema TECHNOLOGY
imefanya watu wakamatwe kirahisi
..

vitu kama GPS tracking,Car mileage,
PC Pandora Key Tracking Software,
Cell Phone Trackers, Key loggers ,
Video Surveillance Equipments , Private Investigators etc...
 
Afrodenzi wantisha hapo

yaani mpaka cell phone trackers waijua?
We hufai kuwa mke lol
 
Nyakati hizi ndo nzuri kwani wanadam wenye akili nzuri utaweza kuwatofautisha kirahisi na wale wenye akili kama za mbuzi!
 
Mdau umesahau kwenye JF!!!!

Wadau,

Maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano ya habari imefanya usaliti katika ndoa na mahusiano kuwa rahisi sana. Zamani ilikuwa vigumu sana kutongozana kwa kuwa ilikuwa ni lazima muonane na muwe mtaa, ofisi au sehemu moja kwa wakati huo.

Siku hizi kwa sms, BBM, facebook, twitter, emails na kadhalika, mambo yamerahishwa sana. Ndio maana hata uaminifu kwenye mahusiano umekuwa TESTED sana. Mwanamke aliyekuwa anaonekana muadilifu katika ndoa miaka ya 80 kwa kuwa tu hakuwa na jinsi ya kuwasiliana na anaotamani ku cheat nao, leo hii ata cheat tu kwa kuwa cheating iko kwenye damu yake.

Kwa hiyo yale mambo ya eti zamani kulikuwa na maadili sana sio ya kweli kivile. Ni kwa kuwa kulikuwa na kikwazo kikubwa katika mawasiliano na ndio maana hakukuwa na kasi kubwa ya CHEATING!!

Sio mtazamo wangu, huo ndio ukweli!
 
hilo neno haswaa, usipokijua hakitakuumiza lakini once utakapokichimba ukakijua inakuwa ni mwanzo wa mlolongo wa matatizo na
kuumia

hapo kwenye red sina muda huo kwa kweli
labda kijitokeze chenyewe....
 
Ila kweli most of men and women ni vimeo. Once nilijaribu kupekua simu ya bf nilikaribia kuzimia, ten ladies na mwingne alitoka kulala nae dk 10 alizoniaga anaenda kununua vocha. Sikusema neno, niliondoka kimya kimya na mpaka kesho anatamani kurud ila nikiwaza hayo daaah.....! Technology imeleta wehu wa mapenzi!
 
Back
Top Bottom