Technical report about Loliondo, Uchakachuaji ni kila mahali jamani! Tutafika?

Katika tembea tembea online nimekuta mkurugenzi wa NIMRI Mwele Malacela akiikana ripoti kupitia facebook na kusema kuwa ni literature review. Nilichoshangaa ni literature review gani inafanywa ikiwa na terms of reference na pia mahojiano na watu mbalimbali kama walivyoeleza kwe acknowledgment page.
Wadau wa afya, research, madawa na vitu vingine mpo wapi? Au mimi sina imani ndo maana sioni wanachoona wengine.
Msaada kwa tuta jamani ila mwenzenu uzalendo umenshinda.

pubis medicine ina matatizo sana!ndio hivi hivi wanacopy na kupaste miongozo ya utabibu bila kuangalia mazingira yetu.usije kushangaa kesho tunaambiwa watu wapewe rufaa kwenda kwa babu.
 
Natumaini upungufu mkubwa na ambao naweza kusema kwamba ni kosa kubwa la kitaaluma, ni hawa mabwana kutokuwahoji watu mbalimbali waliotumia hiii dawa ili kuona kama kweli kuna ambao wamepona baada ya matumizi ya hii dawa. Mbona hawakuenda kutembelea vituo vya afya na kwenye mahosipitalini ili kujua kama wapo watu ambao, baada ya kunya dawa, wamerudi kupimwa na hali zao zikaonekana kubadilika ??

wanafiki hawa!hiki ni kitu rahisi ambacho hata mimi nimekifanya!they know kwamba hii dawa haitibu lakini sijui wanalinda maslahi ya nani?mbwambo amenisikitisha sana!
 
mbona kinafulani wengi wanavipindi hadi kwa matv na wanadai kuponya watu kwa kuwashika na kuwasukumiza hadi waanguke chini namuwasemi sana? nasikia kuumwa presha ngoja nije.
umekumbusha kitu muhimu.kakobe,ndodi na sasa babu wa loliondo ni matokeo ya usimamizi mbovu wa wizara ya afya.wanaacha watu hawa kutumia media kupotosha na kuwachafua wahudumu wa afya.nadhani wengi walioko wizarani ni wabovu kitaaluma au wamepata nafasi hizo kimagumashi ndio maana hawaelewi nini cha kufanya.
 
Jamani Kimsingi niliwahi kuyasema haya kwa baadhi ya scientists wa NIMR kule centre ya AMANI pamoja na TANGA mjini, zote hizo unazozisema mtoa mada ni collection ya reports ambazo zimefanywa na KEMRI wakishirikiana na ICIPE nchini kenya on species ya Carrisa edulis ambayo imeonekana kuwa na anti-viral content. Specie ya babu ya loliondo ni Carissa Spinarum. For those who wishes send to me your emails then i will share with you the paper describing the genus Carrisa na species zake. Kimsingi NIMR ya MWELE hakuna kitu wakenya walishafanya haya mambo siku nyingi na tayari report yao ilishatua WHO huku tunashangaa tu na siasa.
 
wasiojua kinachoendelea kuhusu pastor mwasapile ni kuwa huyu pastor ni pyschatric ni kichaa, inabidi akapimwe tujue uhalali au level ya akili zake. kuotehswa ni jambo lingine, lakini kuoteshwa na MUngu ni jambo kubwa. taifa linaangamia, watu wanaokunywa kikombe wengi wanapoteza maisha, hakuna anayediriki kukiri wazi wazi kuwa amepona tuishi kwa kuhisi. jitihada zifanyike haraka kuondoa hii hadaaaaa
 
bado tunazumgumzia wakenya na kemri yao? mmesahau jinsi walivyomdanganya moi kuwa wamegundua dawa ya ukimwi inayoitwa kemron na moi akatangazia taifa na dunia, kumbe ilikuwa ni hoax? namshukuru sana alyekuwa waziri wetu wa afya wa wakati ule the late Aron chiduo, yeye hakumumunya maneno alisema wazi wazi kupitia gazeti la wakati huo, yaani family mirror kuwa kemron n hoax, mawaziri wenzake akina mwabulambo walikuwa njiani wakienda kenya kunywa kemron wakamshangaa chiduo lakini huo ukawa ni huo mpaka leo kuwa kemron was a hoax. na leo NASEMA KIKOMBE CHA BABU NI HOAX, NA HAKITAFIKA MWEZI AUGUST BILA WATU KUSHTUKA NA KUMKIMBIA.
UKO WAPI MWAROBAINI? WAPI NGETWA 11!!!!!!!
MSISAHAU HISTORIA KIRAHISI HIVYO
 
Mchangiaji uliyesema hii ni technical report kwa matumizi ya ndani. Does it mean ikiwa technical report ndo inatakiwa iwe na uzembe wa kisayansi kama ilio nao? Hata kama ni internal report it has to be scientifically sound. Wanatumia extrapolation kuwa mti unapamaba na HSV kwa hiyo unaweza tumika kwa HIV? Jamani hivyo ni virusi viwili tofauti kabisa.
Swali kubwa niinalojiuliza ni kuwa walifanya makusudi au ndo uwezo wao umeishia hapa? Kama ndo uwezo wao kama taifa tuna shida kubwa.
Chonde chonde bongo ndo hii, tutafika tu goligota.
 
Back
Top Bottom