Tcu ilichagua wanafunzi kozi ya bsc. Agriculture education sua wameibadilisha!!!!

Malyenge

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
6,658
3,646
Wakuu habari za usiku?
Kuna habari kutoka SUA zinansema wale vijana waliochaguliwa kozi ya Bsc Agricutural Education leo wamebadilishiwa kozi. Wameambiwa wasome Bsc Education (Agriculture and Biology).
Sasa tatizo wanafunzi wengine wanasema hawana msingi wa Biology (kuna waliochaguliwa kwa masomo ya Physics, Geography and Mathematics, Economics, Geography and Mathematics). Wanasema somo la biology litawasumbua maana hata katika kozi ya Bsc Agricutural education biology haikuwamo.
Walikuwa wanomba ushauri wangu lakini kwa kuwa kuna jukwaa la great thinkers nikaona nilete kwenu wapate ushauri toka jukwaa moja kwa moja.
 
Waende MUM si kipo jirani? Pale kuna digrii hadi za kuchoma makanisa na kuua nguruwe. Background yoyote iwe ya arts au science inakubalika
 
Wakuu habari za usiku?
Kuna habari kutoka SUA zinansema wale vijana waliochaguliwa kozi ya Bsc Agricutural Education leo wamebadilishiwa kozi. Wameambiwa wasome Bsc Education (Agriculture and Biology).
Sasa tatizo wanafunzi wengine wanasema hawana msingi wa Biology (kuna waliochaguliwa kwa masomo ya Physics, Geography and Mathematics, Economics, Geography and Mathematics). Wanasema somo la biology litawasumbua maana hata katika kozi ya Bsc Agricutural education biology haikuwamo.
Walikuwa wanomba ushauri wangu lakini kwa kuwa kuna jukwaa la great thinkers nikaona nilete kwenu wapate ushauri toka jukwaa moja kwa moja.
Kama ni jina tu (na sio contents) la hiyo shahada ndio limebadilika, sioni kama kuna tatizo kubwa sana. Hata hiyo Bsc Agricutural Education si lazima ingekuwa na kozi za kibaolojia?
 
...mtu mwingine anaweza kuhoji kwamba mbona watu wanasoma LAW(LLB) bila kuwa msingi wowote wa sheria kutoka O'level au A'level......ni kweli hili swala la SUA ni utata mtupu lakini kwa vile O'level wengi Biology tunasoma na kwakua mtu alipata nafasi ya kuingia A'level ina maana alifaulu masomo zaidi ya matatu ikiwemo na Biology hivyo sioni tabu sana mtu mwenye nia thabiti kushindwa kusoma hiyo Kozi
 
Hii ni degree mpya hapo SUA?? Kulikuwa na Bsc. Agriculture Education and Extension, imefutwa??
 
Back
Top Bottom