TCRA yasomesha watatu kwa Sh 2.2 bilioni

TCRA yasomesha watatu kwa Sh2.2bilioni
Send to a friend

Wednesday, 02 November 2011 21:17
0diggsdigg

mh-tcra.jpg
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Jaji mstaafu Buxton Chipata akijibu maswali ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), katika ofisi za bunge jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Makamu mwenyekiti wa bodi hiyo,Vuai Iddi Lica na Kaimu Mkurugenzi Mamlaka wa TCRA, Elizabeth Nzagi. Picha na Venance Nestory

Raymond Kaminyoge
KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imegoma kupitisha hesabu za Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), kutokana na ubadhirifu wa fedha za umma. Ubadhirifu huo uliobainika mbele ya kamati hiyo ni pamoja na mamlaka hiyo kutumia Sh2.2bilioni kuwasomesha wafanyakazi wake watatu nje ya nchi mwaka 2009/10.

Jumla ya Sh4.1bilioni zilitumika katika kipindi hicho kugharamia mafunzo. Hayo yalibainika Dar es Salaam jana wakati Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA, Jaji Mstaafu Buxton Chipeta na menejimenti yake walipofika mbele ya kamati hiyo kuhojiwa kuhusu hesabu zao. "Tumezikataa hesabu hizi kuna matumizi makubwa ya fedha za umma yasiyozingatia kanuni za fedha," alisema Makamu Mwenyekiti wa POAC, Deo Filikunjombe. Alisema TCRA imekuwa ikimlipa mwenyekiti wa bodi na wajumbe wake Dola za Marekani 350 kila mmoja kwa mwezi, sawa na Sh600,000 hivyo kutumia jumla ya Dola 2,000 sawa na Sh3.4milioni kwa ajili ya mawasiliano, wakati wao si watendaji wa shughuli za kila siku za mamlaka hiyo.

Aidha, alisema wajumbe hao walinunuliwa katika mwaka huo wa fedha, simu za mkononi zenye thamani ya Dola za Marekani 600, sawa na Sh1 milioni kila mmoja.

"Wajumbe wa bodi hawastahili posho hizi na kuanzia sasa wasilipwe kwa sababu siyo watendaji wa shughuli za kila siku. Pia kwa nini wanalipwa kwa kutumia Dola badala ya Shilingi ya Tanzania?" alihoji Filikunjombe. Makamu Mwenyekiti wa POAC aliongeza kuwa mamlaka hiyo imetumia Sh36 milioni kuwalipa posho wafanyakazi saba wa idara ya uhasibu wanaofanya kazi katika muda wa ziada, huku wakifanya kazi za kawaida wanazopaswa kufanya katika muda wa kawaida.

"Hawa wanalipana mamilioni ya fedha kwa kufanya kazi ambazo waliajiriwa kuzifanya na wanalipwa mshahara! Huu ni ubadhirifu," alisema Filikunjombe.

Kamati hiyo pia ilibaini matumizi makubwa ya fedha katika ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, Barabara ya Sam Nujoma, Dar es Salaam. Alisema licha ya mshauri wa mamlaka hiyo kukadiria gharama za jengo hilo kuwa Sh27 bilioni, hadi sasa kiasi kilicholipwa ni Sh45bilioni. Kamati pia imebaini matumizi ya Sh600milioni ambayo hayakufuata taratibu za zabuni ya ununuzi wa umma.
"Kiasi hicho kimetumika kununulia vifaa mbalimbali vya ofisi bila zabuni ya ununuzi kutangazwa jambo ambalo ni kinyume na sheria," alisema Filikunjombe.

Alisema sheria inaruhusu mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo, kuidhinisha kiasi kisichozidi Sh50 milioni tu kwa mwaka.Akijibu hoja hizo, Mwanasheria wa TCRA, Elizabeth Nzagi alisema fedha za mawasiliano zimekuwa zikitolewa kwa wajumbe wa bodi ili kuwarahisishia mawasiliano baina yao na menejimenti.

Nzagi alisema mafunzo katika sekta ya mawasiliano ni gharama kubwa na hiyo ndiyo iliyofanya itumie Sh4.1 bilioni kwa mwaka. Hata hivyo, alisema si kweli kwamba Sh2.2 bilioni zilitumika kusomesha wafanyakazi watatu tu nje ya nchi, bali hayo ni makosa ya kihasibu.
Alisema katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita, wafanyakazi wa idara ya uhasibu walilipwa Sh36 milioni za posho ya kufanya kazi katika muda wa ziada kutokana na uchache wa wafanyakazi.

"Tunatarajia kuajiri wafanyakazi wengine ili kazi hizo ziweze kufanywa katika muda wa kawaida," alisema Nzagi.
Kuhusu gharama za ujenzi wa jengo la TCRA, Meneja Mawasiliano na Uhusiano, Innocent Mungy alisema inaweza kuwa juu kuliko makadirio kutokana na kushuka kwa thamani ya shilingi.

"Hakuna ubadhirifu katika ujenzi wa jengo lile hata uchunguzi ukifanywa kila kitu kiko wazi," alisema.
Pia, Jaji Chipeta alisema hakuna ubadhirifu katika mamlaka hiyo akisema kilichojitokeza mbele ya kamati hiyo ni makosa ya kibinadamu katika utayarishaji wa hesabu zilizowasilishwa.

Source: Mwananchi



Hizi self enrichment project zinazoendelea sasa zitaiangamiza nchi kama hatutachukua hatua. Hicho ni chombo cha serikali. Kilichotakiwa kufanyika ni kuusimamisha uongozi with immediate effect na kufanya uchunguzi wa rushwa haraka.

Haya mazingaombwe sijui yatakwisha lini jamani??? Hii ni tamaa, uroho au ndiyo time ya Chukua Chako Mapema (CCM) kabla ya 2015??
 
Leo nimetokwa machozi. Nchi haina uongozi haina wenyewe. Nimesoka uk wa kwanza wa mwananchi kuwa tcra imetumia 2.2 bilioni kusomesha wafanyakazi watatu kwa mwaka mmoja. Nimepiga mahesabu hela hii ingesomesha watoto wa tanzania 300 vyuo vikuu hadi wamalize. Vijana wetu wanaambiwa hakuna hela ila kumbe wakubwa wanalipana mabilioni.

Wale washabiki wa ccm kina malaria sugu shangilieni tena. Mnashangilia wenzenu wanaokula, walioamua kuiangamiza nchi. Shame to ccm, shame to jk

Inawezekana walibadilishiwa ubongo wakawekewa wa kizungu ili wafikiri kama wazungu LOL
 
Hili gap la wenye nacho na wasionacho linatia kinyaa hapa nchini. Elimu ambayo ndio ingewakomboa waTZ na kuinua nchi ndo kwanza 'inafitiniwa' bila aibu na mijitu iliyosomeshwa bure. waTZ tuamke kwa kuikana CCM kwanza mengine yafuatie hapo.
 
manina zao.........na huyo anayejiita mdhibiti n amkaguzi wa hesabu za serikali naomba arekebishe title yake kuwa mkaguzi wa hesabu za serikali maana udhibiti haupo hapa!
 
Haya mambo hayataisha mpaka hapo tutakapoacha kuabudu accademic qualifications na kuangalia zaidi TRACK RECORD OF PERFORMANCE! performers wengi wamezama huko chini ya mfumo; walanguzi wa vyeti ndo wanapanda vyeo. Ukiwa well connected unaambiwa tafuta cheti fulani basi! Nobody cares wewe umeshafanya nini huko nyuma.
 
kwa kweli inauma sanaa! kuona watanzania wengi wanateseka maskini ,huku watu wachache wenye tamaa wananeemeka kihivyo!
 
TCRA mbona ni wabadhirifu siku nyingi tu, hata huo ukaguzi umefanywa kijuu juu sana.napendekeza an independent auditor aende akague mtakuja kuniambia, masafari na maposho wanayojilipaga kiukweli yanakiuka kabisa taratibu za malipo kama alivyosema makamu mwenyekiti wa kamati. hawa jamaa bwana wanaiba sana tena bila huruma kodi za walalahoi!

Hawa si watakuwa walikaguliwa vitabu vyao na Auditor General kabla ya kamati kupitia. Inamaana Auditor aliona mambo safi tu. Ushenzi mtupu.

Kuna taasisi ngapi zenye matatizo kama haya.
 
Kwa kweli lile shirika ndio maana limeshindwa kuboresha huduma zake kwanza kupunguza tariffs za kwenye simu huwa gaharama ni kubwa mno Tanzania na ndio hata Dstv huwa tunalipa viwango kubwa sana Tanzania ikilinganishwa na nchi akama Angola wa Premium ya USD 78 kwa Tanzania wao ni dola 40 na hii inatokana kodi kubwa inayopelekwa TCRA yaaani Prof Nkoma is a failure kwani fees anazokusanya kwenye mashirika ya communication ni mwiba kwa mashirika ambao yapo kwenye sekta ya mawasiliano. Sasa basi ni pesa wanachukua mashirika ya cm na kuishia matumbo mwa TCRA ushauri ni bora nkoma na wezi wenziwe wang'atu tu tumechoka kuonewa.
 
huyu jaji alokua anasoma hyo taarifa ni KILAZA

Tena kilaza hasa! Nikifikiria ni watanzania wangapi wamehukumiwa kwa mkono wake ikiwapo kunyongwa hadi kufa sina hamu. This situation shows the type of people we are having in the public sector.

Nilivyokuwa nasoma gazeti sikuamini kwamba majibu yalikuwa yanatolewa na Mh. Jaji kwa Kamati husika kutetea wizi na ufisadi ulikubuhu. Nilitegemea chombo ambacho Mwenyekiti wa Bodi ni mtu wa aina ya Jaji na Mkurugenzi Mkuu ni Profesa tena anayeheshimika kimataifa, basi chombo hicho kingekuwa na uadilifu uliotukuka kama si kupindukia lakini wapi!

Nikikumbuka ile hukumu maarufu ya "mgombea binafsi" iliyotolewa na jopo la majaji saba wa Mahakama ya Rufaa, nikikumbuka vituko mbalimbali vifanywavyo Bungeni dhidi ya maslahi ya wananchi na taifa, nikikumbuka ufisadi na ubabaishaji uliojaa serikalini na mambo mengine chungu nzima; nafikia conclusion kwamba nchi yetu inaangamia kama siyo kusambaratika kabisa.
 
Ile nafasi ya ukurugenzi wa TCRA ni nzuri. Na allowance zao pia ni nono sana. Tatizo hawakujua kama bunge litakuja kukagua hizo hesabu.
Bottomline, hii nchi haina displine toka juu kabisa mpaka huku chini. Ndio maana watu wanafanya haya tunayoyasikia na kuyaona.

..there you r! tena kuanzia at family levels, watz hawana disciline kabisa!!! on anything!
 
Nilipata kumfahamu DG wa TCRA, Prof John Nkoma alipokuwa Botswana, ni miongoni mwa Watanzania makini waliopata kutokea, siamini kama angeweza kuwasomea wafanyakazi watatu kwa Billion 2.2, something is wrong somewhere...

Mkuu, hii imetokea kwa sababu ya mfumo wetu wa kiutawala ulishakufa. There is absolutely zero good governance and personal responsibility. Hakuna atakayejiudhuru kutokana na hili. Kila mmoja katika nafasi yake kuanzia kwa Bodi ya Wakurugenzi, DG, menejimenti utamsikia akijitetea na kujilinda kwa kutoa visingizio lukuki. Subiri hivi visingizio utaniambia kuanzia leo hii utaona Press release kwenye TV, magazeti kesho.

Bila, kupata Sata wa Kitanzania au China style tutaendelea kupata habari za uozo kila siku bila ya watu kuwajibika au kupelekwa Segerea. Ni hatua mbaya sana tuliyofikia kwa nchi ambayo ilikuwa kioo cha haki na uwajibikaji.
 
hizi kamati za bunge zikishabaini kuna ubadhirifu au upotevu wa pesa za umma then what next? Am tired of this trend of business as usual.

hayo ndiyo madili yao......nasikia wanakasirika kama wanakagua hesabu halafu hawapati kosa.......wananuna kama trafiki barabarani wakikukuta bila kosa la triangle na fire extinguisher kwenye gari.
 
nimejaribu ku google gharama ya kusoma chuo babu kubwa kama mit usa naona tuition fee kwa mwaka ni kama dola 40000 sawa na tsh million 70 na kitu hivi, hiki chuo cha bilion 2.2 kwa wanafunzi 3 ni kipi isije ikawa ni mambo ya pangu pakavu?????
 
Duuh! Hao jamaa itakuwa walikuwa wanasomea kushikiria mkonga wa mawasiliano ndani ya bahari. Ili usije kutawanya mawasiliano halafu samaki wakaanza kutumia internet bila kulipia.
Hii mbona kali! Wanasomea nini hicho cha ajabu???
 
Back
Top Bottom