TCRA Watazame Hivi Ving'amuzi!

Bornvilla

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
924
271
Hadi sasa serikali na kitengo
chakudhibiti mawasiliano
hawajatuweka bayana juu ya
hivi ving'amuzi.Hadi sasa kuna
makampuni zaidi ya moja
yanayotoa huduma ya ving'amuzi hadisasa.
Startimes imekuwa
ikilalamikiwa na wadau kwa
huduma mbovu na wakati
huohuo kasi ya kueneza
ving'amuzi nchi nzima ikiwa sio nzuri,kwani kipaumbele
kimetolewa kwa mikoa
ambayo tangu mwanzo
mfumo wa analog ulifanya
kazi vizuri tofauti na mikoa
mingine mfano ni Shinyanga,Mara na Kigoma
ambako mtu analazimika
kuwa na dish ili kupata
matangazo.
Shida iliyopo kwasasa ni
ving'amuzi vilivyopo kutokuwa na chaneli zote za
ndani,hivyo kama kampuni za
matangazo zitaamua kila moja
kuja na king'amuzi chake
itakuwa hatari kwani itambidi
mtu kuwa na king'amuzi zaidi ya kimoja mezani ili apate
chaneli zote za ndani.
Mashindano ya ving'amuzi
yawe kwenye premium
chanels tu,yani zile chaneli za
kulipia tu,lakini ving'amuzi vyote viwe na chaneli za ndani
na zote ziwe bure.
TCRA iwe makini ili
kuepusha lundo la ving'amuzi
majumbani na maofisini,pia
TCRA itazame gharama za ving'amuzi kwa malipo ya
mwezi ili watu wa hali za
chini nao wanufaike.
 
Tcra ipo tu ili ijulikane ipo ila siyo kwa maslahi ya wananchi na serikali kwa ujumla kwani wangekuwa watendaji wangekuwa washalisungumzia na kuanza kulifanyia kazi
 
Watu wa TCRA kama mnasoma humu amkeni usingizini, mishahara yenu ni kodi zetu.
Tutaingiaje kwenye digitali bila kudhibiti kampuni za ving'amuzi???
Lazima muoneshe uwezo wenu, walazimisheni wachukue channel zote za Tanzania, pia
walazimisheni wamiliki wa vituo vya kitanzania wasiweke vikwazo, waruhusu kampuni za ving'amuzi
kutangaza hapa nchini for free. Haki yetu ya kupata habari ni haki ya kikatiba inalindwa chini ya ibara ya 18 ya katiba iliyopo
Kamwe haki hii msiione kama ni anasa. TCRA AMKENI!!!
AMKENI HARAKA MMELALA SANA USINGIZI WA FOFOFOOO!!
 
halafu ni vya muda mrefu, mathalani vya "startimes" vinaonyesha ni vya mwaka 1990, vya ting 1995, vya easy tv sijui kwa kweli, ila vya dstv vingi ni vipya 2005-present. decorders za "free-to-air" nazo zingine za zamani, zingine mpya though nyingi ni fake, TCRA na other agencies responsible wafanye kazi yao ...
 
TCRA mwaka jana mlitueleza kuwa mtatoa elimu kwa jamii juu ya mawasiliano ya Digital, lakini mpaka sasa Ovyo jamii haijui nini maana ya Digital na Analog. Mkayaacha haya ya Digital mkaenda kwenye Mkonga Wa Taifa nayo sijui yamefika wapi.
Fanyeni kazi ionekane sio kujisomesha kwa Mabilioni ya kodi za Watanzania halafu Output hatuioni.
 
Naskitika mpaka sasa wananchi hawaelewi chochote kuhusu digital..! Na kingine iweje tv za kibongo tunakuwa tunalipia? Au ndo itakuwa mwisho wa mlala hoi kuangalia tv? Na kwanini king'amuzi hakina channel zote za hapa tz? Inaonyesha kunaudhaifu hapo ..'na kama hakuna udhaifu kwanini kila kampuni inafanya kama itakavyo? Inabidi TCRA muangalie hili, bado miezi michache tu tusahau analogia afu hakuna cha elimu na mnatuchanganya wananchi kwa ujumla
 
Yaani mimi mpaka ndio sielewi chochote kinachoendelea kuhusiana na hivi ving'amuzi.
 
Back
Top Bottom