Elections 2010 TCRA disassociates itself with defamatory messages against Slaa

JK alipokashfiwa na mtandao wa Ze Utamu ulifungiwa mara moja na TCRA. Slaa anapokashfiwa anaambiwa aende polisi. JK alipopigwa mawe huko Mbeya wapiga mawe walidakwa haraka sana, lakini Mtikila alipopigwa mawe Tarime hakuna kilichofanyika! Anyway, "all animals are equal but there are those who are more equal than others!"
 
Mkuu pole sana, ni vocha za Kampuni gani ya simu, hii inweza kuwa mwanzo mzuri wa kufuatilia kwenye hayo makampuni
namba yao ni 15016 ndiyo wanayotumia. na ukishaingia hupati hiyo vocha bali ujumbe kuwa umejiunga bure na takataka zingine. Hizo coupon waliwapatia vijana wadogo wadogo wazisambaze. walizigawa nyingi sana kwenye mikusanyiko ya watu. Mimi sikuchukua kwa sababu nataka free voucher bali nilitaka kujua kama kuna hongo ndani yake ili nikawashtaki.

Hapa tujiulize. hivi hawa TCRA wana maana gani kuruhusu huu tumbo kufanyika hasa kipindi hiki cha uchaguzi? pia kuna sms nyingine zinasambaa kupitia namba za kawaida mabazo zina uchochezi hatari wa kidini ambapo kwa mtu mwenye asiyeweza kupambanua mambo atahamanika sana na kushawishika vibaya.
 
JK alipokashfiwa na mtandao wa Ze Utamu ulifungiwa mara moja na TCRA. Slaa anapokashfiwa anaambiwa aende polisi. JK alipopigwa mawe huko Mbeya wapiga mawe walidakwa haraka sana, lakini Mtikila alipopigwa mawe Tarime hakuna kilichofanyika! Anyway, "all animals are equal but there are those who are more equal than others!"
... kondoo walikuwa wanajifunza wimbo mpya kwamba 'MIGUU MINNE NI MIZURI, LAKINI MIWILI NI MIZURI ZAIDI' ndipo wanyama wakaona nguruwe wakiongozwa na MZUSHI wakijaribu kusimama kwa miguu yao miwili ya nyuma.....
Thanx mkuu kuna funzo kubwa hapo
 
JK alipokashfiwa na mtandao wa Ze Utamu ulifungiwa mara moja na TCRA. Slaa anapokashfiwa anaambiwa aende polisi. JK alipopigwa mawe huko Mbeya wapiga mawe walidakwa haraka sana, lakini Mtikila alipopigwa mawe Tarime hakuna kilichofanyika! Anyway, "all animals are equal but there are those who are more equal than others!"
Tumeona humu JK amekashifiwa lkn mtandao haujafungiwa the same applied to Dr Slaa hasa kipindi hiki cha kampeni kila kitu kimewachiwa huru .Point niliyotaka kuiweka ni kwamba unapoamua kupambana pambana na wacha ulalamishi weka mkakati mbadala na endelevu kufikia lengo husika kwasababu ulalamishi si moja ya njia mbadala au endelevu ya kufikia lengo!
 
ni kwa sababu hawawezi kufungia; ila kwa vile ndio wamekubali kuwa hizi ndio siasa basi mkuki ukirudishwa wasije wakasema "huyu ni binadamu"..
 
Namba nyingine ni +3588108226

+3588976578

Nimetumiwa na Namba zote hizo.

Nashauri tuchukue hatua haraka: Kwanza ku 'counter attack' message.

Tutumie watu message kwamba "Tupuuze propaganda za ccm, Chadema ni Chama cha Amani. Tunataka uchaguzi Huru na Haki. Chagua Chadema, Chagua Slaa. Tusidanganyike"

Asanteni
 
wewe umenena na Angalau hili linaonyesha mbadala wa kombora lao!
 
Mimi ni telecom engineer all my lyf toka nipo A-level my dream was kuja kusaidia huduma ya mawasiliano nikiwa na TCRA na nilikua naihwshimu hii taasisi kiasi ya kwamba nilikua tayari hata kufanya kazi nao kwa kujitolea but toka zoezi la usajili lilivyoendeshwa nimegundua ni genge la loosers tu kama zilivyotaasisi zingine ambazo zinaongozwa na maprofesa wakubwa lakin maamuzi wanatoka kina Makamba, Riz1 na nduguze... Eeeee MUNGU wape watanzania uwezo wa kutambua mambo angalau kwa mwezi huu mmoja ili waone utombu uliopo kwenye serikali yao
 
Mi naomba kwa haraka sana CHADEMA wakishirikiana na Rais mtarajiwa wa awamu ya Tano Dr Slaa.Waitishe mkutano na vyomba vya habari kutolea ufafanuzi wa hizi msg za vitisho na zinazovyucha amani.Wananchi wengi wameingiwa hofu na wanaotuma msg hizi.CHADEMA ni chama makini sana na kinapendwa na wananchi kwa 90%,watoe tamko kali.Msg hizi zinavunja amani kwa 100%.Zinatoka +3588108226 na numba nyingine pia
 
Hakuna haja ccm wanaweweseka wacha wahangaike na cheap popularity Mara !Mara kwa waalimu lakini jk is as good as dead..na kuhangaika nao is wasting time biting a dead snake
 
Hivi TCRA hawajafungia namba zisizosajiriwa hadi leo si walitoa dealine, then waka revice deadline na muda ukaisha!!! Anyway bongo no Deadline!!! By the way ilipokua ishu ya "call in RED number" walitoa tamko la kufuatilia source ya ujumbe, iweje hii ikwamishwe na zoezi la usajiri?? Kweli authorities zote bongo Zimechakachuliwa!! Tutakimbilia wapi jamani

Hawa ni wajinga unataka kusema hawawezi kumjua sender? Ni waongo tu. Na inawezekana kuwa lile daftari feki la wapiga kura limeandaliwa kwa copy ya vitambulisho vya wapiga kura walipoenda kusajii simu nina tia shaka kuwa hilo ndo lilikuwa ni lengo kuu ka zoezi zima
 
Mkuu kuna kitu lazima kifanyike kukomesha hizi chokochoko dhidi ya TAIFA letu maana inaonekana kwamba nchi ipo kwenye UTASHI wa kikundi fulani kinachoamua hatima yetu in very childish way
Tusubiri, JWTZ limeahidi kuwachukulia hatua wachafuzi wote. Bila shaka watawachukulia hatua na wanaosambaza sms hiyo. Ni wakati muafaka wa kumueleza shimbo achukue hatua kama alivyoahidi.
 
Majibu ya TCRA ni kichefuchefu..lazima wawajibike... walisasema weameyaagiza makampuni ya simu za mkononi kufunga namba zote ambazo hazijasajiliwa sasa iweje wanashindwa kuwajua wasambazaji wa ndani... Ni kweli kwamba hawawezi kuzuia namba kama kweli imetoka nje ya nchi kama namba hio haijapiikwa, basi ujumbe umetoka Finland.http://countrycode.org/ ..... lakini wanaosambaza ujumbe huo mchafu lazima wawajue.... Hii si haki kwa mgombea huyo...na kwa vyovyote ni kampeni za wanaomwogopa including status quo!!!!
 
Poleni sana!

Hizi sms zinatumwa kwenda namba uliyotumia kuchangia CCM kwa mtandao; kama mnakumbuka mwanzoni mwa kampeni ccm walitoa namba ambayo ukituma sms unawchangia Tsh. 600, na tangia hapo wamekuwa wakituma updates za kampeni zao kwenye namba hizo zilizowachangia.

Sasa kama wewe ni shabiki wa Chadema na umetumiwa hii sms ya kumkashifu mgombea wako wa uraisi, ni dhahiri kwamba ulichangia ccm sh. 600. unategemea wenzio wakueleweje? Kwenye msafara wa mamba na kenge wamo; nadhani chadema watumie nafasi hii kuwatambua ndumilakuwili miongoni mwao.
 
ilivyokuja ile ishu ya namba zenye mionzi serikali ikajifanya kutoa tamko fasta...ila hii aaaah!! pu..*&*^%$%%$$%..ff kabisa!
 
Naungana na wote wanaosema TCRA wanatakiwa kutoa maelezo zaidi, pamoja na umuhimu wa kuwahusisha polisi. Tatizo hapa ni ukweli kwamba namba hii inaonekana ni ya nje. Hakuna nchi yenye code +3 wala +35. Lakini Finland code yake ni +358. Swali hapa ni kujua kama kweli SMS hizi zinatumwa toka Finland, au baadhi ya matapeli hapa nchini wameweza ku-register code yao na kuitumia kuwajenga hofu wananchi. Hapa ndipo mkono wa TCRA unahitajika, kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Sio jambo la kunyamazia, kwa sababu leo ni Slaa, lakini huwezi kujua kesho itakuwa nini.
 
Natoa wito kwa mnadhimu wa jeshi kwenda tena mbele ya umma na kutoa tamko kukemea hii hofu mpya yenye upotoshaji wa hali ya juu utakaopelekea rasmi kutokea machafuko aliyoyatabiri. Shimbo ulisema kuna watu wametoa kauli za umwagaji damu. Sasa kuna wahuni wameenda hatua zaidi na kusambaza ujumbe hatari. Tunakusubiri mbele ya luninga zetu utuondoe hofu katika hili pia.
 
Back
Top Bottom