Tbs wafanya ufisadi wa kutisha duniani!!

BASIASI

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
9,735
5,003
TBS wafanya ufisadi wa kutisha Send to a friend
Saturday, 10 March 2012 10:11
0diggsdigg

cag-top.jpg
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali Ludovic Utoh

Mwandishi Wetu
WAKATI kukiwa na taarifa za ukata Serikalini, imebainika kuwa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), limefanya ufisadi kupitia mpango wa ukaguzi wa magari nje ya nchi kabla ya kuletwa nchini, hivyo kulikosesha taifa mamilioni ya fedha. Taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali, imethibitisha kwamba hadi kufikia mwishoni mwa waka jana, Serikali ilikuwa imekosa kiasi cha Sh243 milioni kufuatia hatua ya TBS kushindwa kukusanya ada kutoka kwa kampuni zilizopewa leseni za kukagua magari katika nchi mbalimbali duniani. Taarifa pia imebaini udanganyifu uliodaiwa kufanyika kwenye tozo za faini kwa magari yaliyodaiwa kuingizwa nchini bila kukaguliwa.

Hali kadhalika, Serikali ilipoteza mapato baada ya TBS kutoa msamaha kwa maduhuli bila kufuata taratibu za fedha. Taarifa hiyo ambayo gazeti hili limeiona, inakwenda kwa kamati za Bunge za Hesabu za Serikali na ile ya Hesabu za Mashirika ya Umma na huenda ikawasilishwa katika mkutano wa saba wa Bunge la kumi,utakaofanyika Aprili mwaka huu mjini Dodoma. “Kwa sasa shirika (TBS) linatoza kiasi cha asilimia 25 ya gharama ya ukaguzi kwa kila gari linalokaguliwa na wakala.

Hata hivyo baadhi ya wakala wameshindwa kuwasilisha kiasi hicho kwa wakati na wengine kushindwa kabisa kuwasilisha mapato yaliyokusanywa kwa mujibu wa makataba uliopo,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo. Hata hivyo alipotafutwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Joyce Mapunjo, alionyesha kushangazwa na ripoti hiyo, huku akifafanua kuwa uchunguzi wa Mkaguzi Mkuu wa Serikali bado haujaanza.

“Hiyo fedha kwa ajili ya kufanyia uchunguzi bado haijapatikana sasa hiyo ripoti wewe umeipata wapi,” alihoji na kuongeza, “hakuna kitu kama hicho.”

Kwa jumla taarifa hiyo inabainisha udhaifu mkubwa katika utendaji kiasi cha kutoa mapendekezo yanayoitaka Serikali kupitia Bodi ya Wakurugenzi wa TBS, kuwawajibisha watendaji wakuu wa shirika hilo akiwamo Mkurugenzi Mkuu, Charles Ekelege.
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serilali pia alibaini kuingizwa nchini kwa kiwango kikubwa cha bidhaa zinazohatarisha afya za watumiaji kwa kuwa chini ya kiwango au kukosekana wa taarifa za ziada kuhusu bidhaa ambazo zilibainika kutofaa kwa matumizi ya watu baada ya kufikishwa nchini.

Orodha ya bidhaa zisizo na ubora ambazo zinadaiwa kuingizwa nchini wakati TBS ikijua kuwa hazifai kwa matumizi, ni ndefu na miongoni mwake ni mafuta aina ya siagi, kondomu, matairi ya vyombo vya moto,mbolea, mafuta aina ya petroli, oili za magari, mabati, nondo, sabuni na pikipiki.
Taarifa hiyo ilisema TBS iliwatumia barua baadhi ya waingizaji wa bidhaa zisizokuwa na ubora wakitakiwa kwenda kumuona Mkurugenzi Mkuu kwa maelekezo zaidi, lakini hakuna ushahidi uliodaiwa kuonyesha nini kiliendelea baada ya maelekezo hayo.Taarifa kwamba bidhaa ambazo hazikuwa na viwango ziliingizwa sokoni zinachagizwa na ripoti ya CAG inayothibitisha kwamba TBS haina kumbukumbu ya bidhaa ambazo zimepimwa na kuthibitika kuwa hazina ubora unaotakiwa.

Taarifa hiyo katika moja ya sehemu zake inasema “kuna uwezekano mkubwa wa bidhaa nyingi ambazo hazikukidhi viwango kuingizwa sokoni na hivyo kuhatarisha afya za watumiaji”.

Upotevu wa fedha Mbali na Serikali kukosa kiasi cha Sh243 milioni za ada kwa kampuni zilizopewa leseni za kukagua magari, ripoti ya CAG pia inabainisha kuwa upotevu wa fedha pia ulisababishwa na kutoa misamaha ya maduhuli bila kufuata taratibu za fedha.
 
Kinachoshangaza report imefanywa na CAG kwamba ina ukweli ndani yake wadau tukishauri JK awafukuze kazi hawa wahujumu uchumi wa taifa mtoto wa mkulima anasema tusimpangie jinsi ya kufanya kazi,kwa nn tusiamini dili hilo ni la wote?
 
Back
Top Bottom