TBS na ukaguzi wa bidhaa

Elai

Senior Member
May 26, 2011
154
9
Katika taarifa ya habari ya saa 2.30 usiku wa leo RFA, TBS wanasema kuwa kuanzia Februari 2012 watakuwa wakikagua bidhaa kwenye maeneo zinakotokea ili kuthibiti bidhaa zisizo na ubora. Je, kuna ufanisi utakaopatikana?Tathimini.
 
Mimi nawasifu sana waTZ Wenye dhamana ya uongozi kwa ubunifu. Tatizo ni kwamba ubuunifu wao ni kwa ajili ajili yao na si kwa sababu ya uzalendo. Na wakitetea hoja zao huwa wakali kweli kweli!
Wanaogopa kusafisha nyumba yetu kwa sababu moja kuu inayosumbua takriban nyanja zote za huduma - kuna mkono wa mkubwa!
Akigusa tu, kibarua kinaota majani.
 
Kwanza watuambie yale mafuta machafu yaliyoingizwa juzi yalipokewaje wakati wao wapo???
 
Hamna kitu hapo wameshindwa kukagua ndani sasa wanakokimbilia bidhaa feki zitakuwa maradufu
 
Hivi jamani ina maana nchi yetu haina watu wanaofikiria???Ina maana tumeshindwa kulinda nchi yetu mpk tukakague bidhaa zinakozalishwa??sasa tutaenda nchi ngapi???nasikitika sana na TBS ina mawazo mgando!!! Ebu angalia nchi yetu,tuna bidhaa za kila nchi. Mi nashindwa hata kujua watafanyaje hiyo kazi,watakaa kwenye port zote??na watajuaje hizi bidhaa zinakuja TZ??je zikibadilishiwa kwenye ndege au meli itakuwaje??? Wake up Tanzania!!!
 
Back
Top Bottom