TBS na sukari kutoka nje, je mnalijua hili?

Kiresua

JF-Expert Member
May 13, 2009
1,184
259
Ni takribani miezi 6 tangu nilipomuuliza mwenye duka kwa nini hauzi sukari ya nje, 'Brazili' anauza ya Ilowo! Wakati sukari ya TZ ni ghali kuliko ya Nje. Alinijibu kitu ambacho sikukitilia maanani kwani sikukiamini. Aliniambia sukari ya nje huwa sio kamili ki-uzani! Ni mwezi uliopita kijana wangu alinunua sukari ya Brazili kwa bei ndogo kdg ya Tz, akapiga simu kwa duka analonunua bidhaa, kumuuliza mbona unauza sukari bei ghali? Alimjibu kwani ni ya wapi? Akamjib ni ya nje! Akamwambia ipime ndo utajua ni kwa nini. Oh! Ilikuwa pungufu kilo 10, yani badala ya kilo 50, ilikuwa ni kilo 40. Nikakumbuka maneno aliyowahi kuniambia. Sasa hi imekuwa ni kawaida kwa matani na matani ya bidhaa hi inayoingizwa hapa nchini kwa ujanja wa wafanyabiashara, na kutumia fursa kuwaumiza WaTZ. Wafanya biashara wengi wadogo hawajawahi kulijua hili ndio maana wanaenjoy punguzo la sh 2,000 wanaliwa sh 18,000. Swali langu ni kuwa hv hawa TBS na WMA wanalijua hili au na wao ni sehemu ya tatizo? Au mnahangaika na malumbesa tu? Wanapotuambia wanakagua bidhaa zinazoingia nchini wanakagua badhaa gani? Kumbukeni tunawalipa mishahara kupitia kodi zetu mtulinde halafu mnazurura tu mjini. Kama mnaingiaga humu mkamwambie bosi wenu muanze ukaguzi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom