change we need
Member
- Aug 10, 2011
- 81
- 9
Kuna mambo mengi sana nchi hii ambayo hayako sawa..na ndio maana ukijjiuliza sana huwezi kushangaa na takwimu zinazotolewa kuwa nchi maskini na ombaomba zaidi duniani yenye rasilimali kibao..
kila sehemu matatizo tena yanayoweza kuepukika lakin kwa vile tunachumia tumbo basi hakuna wa kumfunga paka kengele tuchukulie mifano michache:
kila sehemu matatizo tena yanayoweza kuepukika lakin kwa vile tunachumia tumbo basi hakuna wa kumfunga paka kengele tuchukulie mifano michache:
- Ukienda maliasili ni kichefuchefu mpaka wanyama wa hadhi ya Twiga wanaibiwa achilia mbali mambo ya vitalu na nk
- Ukienda nisharti na madini ni balaa zaidi kuanzia mikataba ya madini,nishati ya umeme mambo ambayo yanazidi kudidimiza uchumi
- Ukienda nyumba na maendeleo ya makazi hali mbaya hakuna mfano haijulikani kama sehemu unayoishi ni salama maana panawez kubadilishwa matumizi muda wowote au kuuzwa kwa wenye pesa
- Takukuru nako si pa kukimbilia
- Mahakama utata mtupu
- Ukienda mawasilianao na uchukuzi ni vumbi tu linatimka kuanzia masuala ya bandari na kampuni zinazotoa huduma mpaka ufikie reli na mikataba yake pamoja na miundombinu ni hali ya kukatisha tamaa, usafiri suala ambalo ni nyeti sana kwa uchumi wa nchi halithaminiwi.
- Ukija wizara ya afya, elimu na nyingine nyingi tu mpaka sasa TBS wazee wa viwango unafikiri kuna kutoka hapo?