TBC1 watoa habari kwa kutegemea maoni ya wachangiaji kwenye JF

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
Leo TBC waketoa habari ya mnajimu mkuu wa kambi ya upinzani akieleza kuwa alishaandika barua ya kutaka maelezo kwa shibuda.

TBC walisema kuwa wameomba maelezo hayo kutokana na maoni ya watu wengi hasa kwenye mitandao kutaka shibuda afukuzwe uanachama. Wakati wanaeleza hayo ilionekana picha waliyoshoot kwenye laptop ambayo ilikuwa inadisplay ile thread ya kunusu matamshi ya Shibuda kwenye JF. Walivyoscroll down ilionekana kuwa ilikuwa inaruhusu replay, kumaanisha kuwa user alikuwa member wa JF.

Hii inamaanisha kumbe hata maoni tunayotoa kuhusu TBC yanasomwa, ila sijui kama yanafanyiwa kazi.
 
jf ni mtandao unafikisha ujumbe kwa jamii husika ila nawashauli wanachama wenzangu tuwe tunatoa michango na hoja za msingi na zilizofanyiwa utafiti wa kina.
 
Leo TBC waketoa habari ya mnajimu mkuu wa kambi ya upinzani akieleza kuwa alishaandika barua ya kutaka maelezo kwa shibuda. TBC walisema kuwa wameomba maelezo hayo kutokana na maoni ya watu wengi hasa kwenye mitandao kutaka shibuda afukuzwe uanachama. Wakati wanaeleza hayo ilionekana picha waliyoshoot kwenye laptop ambayo ilikuwa inadisplay ile thread ya kunusu matamshi ya Shibuda kwenye JF. Walivyoscroll down ilionekana kuwa ilikuwa inaruhusu replay, kumaanisha kuwa user alikuwa member wa JF. Hii inamaanisha kumbe hata maoni tunayotoa kuhusu TBC yanasomwa, ila sijui kama yanafanyiwa kazi.

Mbona hata MJOMBA ni mwenzetu humu jamvini. Huwa wanakuja humu kuchukua hali ya kisiasa nchini na kupanga mikakati ya kuvua magamba.

Masahihisho kidogo hapo kwenye red: ni mnadhimu siyo mnajimu.
Tafsiri:
Mnajimu: Mtu anayetabiri nyota za watu; mfano leo utagombana na watu, leo utapata bahati, leo vaa nguo nyeupe, n.k.
Mnadhimu: Mnidhamishaji ama Mkuu wa masuala ya nidhamu katika jamii husika.
 
hao wanafe tu ngoja al jazeera wanakuja kuwameza kama hawana mikakati
 
Jana usiku wakati wa taarifa ya habari ya TBC, Jukwaa la Siasa la Jamii Forums lilirushwa live kwa watanzania wote. Ilikuwa ni wakati wa habari inayomhusu Shibuda kama ameshaandikiwa barua ya kujieleza kwa nini aliamua kukaidi maazimio ya chama kuhusiana na posho; na mbunge amabaye nafasi yake ni mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni,Tundu Lissu, akawa analifafanua.

Sasa suala hapa si kuwa Jamii Forums, hasa Jukwaa la Siasa limepata umaarufu hadi kwenye vyombo vya habari vya kitaifa; mbona hata bungeni Jukwaa hili limeshatinga? Suala hapa ni kuwaweka attention wajumbe wa Forum hii na Jukwaa hili kwamba tuwe tunapima kile tunachokiandika humu maana comment yako au ya kwangu kuna uwezekano mkubwa ikawa inachukuliwa na umuhimu mkubwa na wasomaji huru, wasiofungamana na upande wowote kisiasa, kiuchumi hata kidini.

Nina mantiki gani hapa? Nitajitolea mfano. Mwanzoni kabla sijajiunga na JF (Jamii Forums) nilikuwa tu napitapita kwenye mitandao ya kijamii kama uninterested reader baada ya kuwa nimechoka baada ya muda fulani wa kazi. Sasa kuna baadhi ya members hapa ambao huwa nadhani pengine siyo watanzania (wamarekani hivi au wamesoma ulaya - please forgive my racism) kwa jinsi ambavyo wana weledi wa uchambuzi wa masuala ya kijamii na kisiasa utadhani hawa hawajasoma bongo. Samahani kama ntawataja baadhi, Mzee Mwanakijiji, Lula Mwananzila, LAT na wengineo wengi. Wapo wengine pia tunaotofautiana fikra kama Malaria Sugu, lakini hapa mimi ninazungumzia uchambuzi wa mada, uwezo wa kutoa hoja kitaaluma na pengine upambaji wa hiyo hoja yako kifasihi na kisanaa ile isomeke na kupendeka kwa watu. Hivyo nikavutika nikajiunga. Nikawa member.

Sasa ikiwa JF inaweza kuvuta hata hisia za TBC na bunge mpaka wakaona kuna umuhimu wa kutajwa kwanye program zao iwe kwa mtazamo hasi, chanya au vyovyote vile, itakuwaje iwapo juhudi za makusudi kuongeza viwango vya uchangiaji kwenye hili Jukwaa zitaongezwa? Si ndio hapa panaweza hata pakawa sehemu ya kutafuta sera mbadala kwa watawala wa serikali?

Na katika kuchangia katika kulinda au kuongeza viwango vya hili jukwaa, napendekeza:

- Kila mjumbe kuandika, iwe ni kuanzisha thread mpya au kuchangia mada kwenye thread, maoni yenye mantiki (uwe na data sahihi, usiandike umbea)
- Kila mjumbe kujaribu kuwa objective katika uchangiaji (nakiri kwamba siipendi CCM naweza kushindwa katika hili, ila nitajitahidi), yaani, ufiche hisia zako useme ukweli -- mfano ikiwa wewe ni CHADEMA JK atakapofanya jambo zuri tumsifie hata kama ni mpinzani wako, hivyo hivyo kwa wana CCM inapokuwa ni CHADEMA yenye sera nzuri.
- Kuandika pale inapobidi, si lazima kila siku uandike, au si lazima kuchangia katika kila mada.
- na kadhalika.

Asanteni.
 
nina akili timamu siwezi kumsifia jk, hakutaka kukutana na wapiga kura wakati wa kampeni wamuulize maswali, katujazia makauli mbiu tu kwenye nchi yetu, kaigeuza kuwa nchi ya uzinduzi, katika watanzania 40m ngeleja na ma-agreco yake lazima awe waziri wa NICAB na madini, usije na pendekezo kwa namna yoyote eti turidhie kumsifu jk na chama chake, wakitenda vema ndiyo kutimiza wajibu huko, sifa za nini hapo? wakiboronga watoke kwa kujiuzulu au tuwawajibishe!!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom