Elections 2010 TBC1 ni wachafu!

TzPride

JF-Expert Member
Nov 2, 2006
2,616
1,167
Jana jioni niliangalia taarifa ya habari ya TBC1 nakuona jinsi hii TV ya uma ilivyo chafu! Walitoa habari ya ukosefu wa maji katika mjini wa Karatu. Ni aibu sana TV ya uma inayoongozwa na mtu aliyepata "exposure" ya jinsi vyombo vya uma vya wenzetu vinavyoendeshwa, yeye anafanya kinyume!
Hii habari ilikuwa ni kumchafua Dr. Slaa na Chadema kwa ujumla. Hivi jamani ukosefu wa maji katika nchi hii ni habari kweli? haya ni maisha ya kila siku. Dar ni sehemu ngapi maji yanatoka muda wote, watu wasichote kwa madumu kutoka mbali? Kwa nini iwe habari kwa Karatu?
Ushauri wangu mafisadi wa nchi hii, mwisho wenu hauko mbali. Tumieni tu ulafi wa akina Tido Mhando na wengineo kwa maslahi yenu, lakini mjue wazalendo inatuuma na ipo siku tutaikomboa nchi yetu. Wakuu wa vyombo vya uma na wote wale wenye dhamana kama hizo, muogopeni Mungu----watanzania wamedhulumiwa sana kwa kitendo cha ninyi kuabudu mafisadi na kutumia dhamana hizo kwa maslahi yenu binafsi.

Nalaani kitendo hicho kiovu cha TBC1, kodi zetu mnatumia kwa manufaa ya mafisadi!
 
Kwa taarifa yao hiyo sio aibu kwa Slaa ni aibu kwa Kikwete, yeye hajawahi kumiliki Dola amepambana sana bungeni pesa zilizoporwa na wachache zirudishwe na zitumike katika kuleta maendeleo ya jamii ikiwemo maji Karatu , hajawahi kulala hata siku moja bungeni tuseme hakuwakilisha vyema, kwa taarifa yao Slaa ni kama Mbunge wa Tanzania wote na sio mbunge wa Karatu pekee.
 
Mungu aipushie mbali yatakayo ikumba Tz kutokana na hizi nguvu za mafisadi, maana ipo siku watanzania tutasema inaf iz inaf
 
Habari haina impact wala tusihofu .Watanzania wa leo ni wa elewa sana wanajua pumba na chuya.CCM wako kimakosa ikulu hawa sifa za kukaa na kuongoza nchi hata ukiangalia tu mikakati yao ya kusaka ushindi ni ya kitoto zaidi.Kwa mfano hii habari.
 
Jana jioni niliangalia taarifa ya habari ya TBC1 nakuona jinsi hii TV ya uma ilivyo chafu! Walitoa habari ya ukosefu wa maji katika mjini wa Karatu. Ni aibu sana TV ya uma inayoongozwa na mtu aliyepata "exposure" ya jinsi vyombo vya uma vya wenzetu vinavyoendeshwa, yeye anafanya kinyume!
Hii habari ilikuwa ni kumchafua Dr. Slaa na Chadema kwa ujumla. Hivi jamani ukosefu wa maji katika nchi hii ni habari kweli? haya ni maisha ya kila siku. Dar ni sehemu ngapi maji yanatoka muda wote, watu wasichote kwa madumu kutoka mbali? Kwa nini iwe habari kwa Karatu?
Ushauri wangu mafisadi wa nchi hii, mwisho wenu hauko mbali. Tumieni tu ulafi wa akina Tido Mhando na wengineo kwa maslahi yenu, lakini mjue wazalendo inatuuma na ipo siku tutaikomboa nchi yetu. Wakuu wa vyombo vya uma na wote wale wenye dhamana kama hizo, muogopeni Mungu----watanzania wamedhulumiwa sana kwa kitendo cha ninyi kuabudu mafisadi na kutumia dhamana hizo kwa maslahi yenu binafsi.

Nalaani kitendo hicho kiovu cha TBC1, kodi zetu mnatumia kwa manufaa ya mafisadi!

Achana nao Wanafiki
 
najaribu kufikiria siku tutakapomng'oa Kikwete, ni watu wangapi wataango'ka nae! baiolojia ya mimea inataja mimiea inayoitwa 'parasite' mimea ambayo uhai wake hutegemea mti mkubwa. Mti huo ukikatwa viparasite vyote vinakufa. Akina todo wasubiri anguko.
 
Wangefanya tathimini hiyo hapa hapa Dar wangepata mengi zaidi ya huko Karatu. Shida ya maji ipo Tanzania nzima ila kwa uelewa finyu wa kummaliza mtu wanafanya wasioyajua. Muheza kuna shida ya maji pia ningewashauri waende kule wapate habari tuone.
 
Kwa taarifa ni kuwa kabla Slaa hajawa mbunge hata hiyo foleni ya maji haipo kwa sababu maji hayakuwepo. Tatizo la sasa ni kuwa baada ya watumiaji kuongezeka na matumizi binafsi(majumbani) hali kadhalika na baadhi ya maeneo mabomba kupasuka. Yote hayo yanasababisha kutokea hilo linalotokea sasa.

TBC 1 walichakwenda kufanya ni agizo la mabosi wao kuwa wakachukue picha kwenye maeneo ambayo wanaweza kupata kile wanachotaka kuonesha. Wangeenda maeneo mengine huko huko Karatu wangewakuta watu wengine wanapata huduma bora ya maji, mbona hayo hawataki kuonyesha? Kero ya maji Karatu wameona kuwa ni habari inayostahili kupewa coverage kubwa tena kwa muda mrefu wakifikiri Watanzania watashindwa kuelewa kuwa lengo lao ni kumchafua Dr. Slaa kumbe ndo wanamwongezea umaarufu.

TBC 1 wanatujosha wanaposhindwa kutofautisha kati ya majukumu yao kwa CCM (kama kweli wanstahili kupewa majukumu na CCM) na majukumu yao kama chombo cha Serikali kwamba wanawajibika wananchi. Wanatekeleza maagizo ya CCM wakijua kuwa wao siyo chombo cha CCM.
 
Naunga mkono Kulaumu hujuma hii na matumizi mabovu kwa makusudi mali za uma.
 
Ile taarifa walidhani wanamchafua Slaa lkn kwa upande mwingine naona inampa credit kwani afadhali Karatu wanapata maji japo kwa muda mfupi. Mbona hapa Dar Es Salaam kuna maeneo ambayo wananchi hawajui hata sura ya bomba la maji achilia mbali kupata hayo maji. Dsm watu wananunua maji ambayo hawajui yanakochotwa (dumu la lita 20 sh. 200 - 500) na wkt mwingine watu wanaishi kwa maji ya mabondeni.

Karatu wako mbele na ktk hilo nawafagilia mno, aibu iko kwa TBC1 na CCM yenyewe inayoimba kila siku kuwa imeweza kuboresha maisha ya Watanzania.
 
Mungu aipushie mbali yatakayo ikumba Tz kutokana na hizi nguvu za mafisadi, maana ipo siku watanzania tutasema inaf iz inaf
Iko siku ipi? Saa ya ukombozi ni sasa. Twahitaji kusema tumechoka, na ikiwezekana tutangaze vita kamili na hawa viongozi wa TBC maana hawa ni adui zetu wanamapinduzi kabisa!!!!!!!!!!!! Hili waliona siku ile Jangwani na bado inawezekana hata sasa!!!!
 
Jana jioni niliangalia taarifa ya habari ya TBC1 nakuona jinsi hii TV ya uma ilivyo chafu! Walitoa habari ya ukosefu wa maji katika mjini wa Karatu. Ni aibu sana TV ya uma inayoongozwa na mtu aliyepata "exposure" ya jinsi vyombo vya uma vya wenzetu vinavyoendeshwa, yeye anafanya kinyume!
Hii habari ilikuwa ni kumchafua Dr. Slaa na Chadema kwa ujumla. ]

Inanikumbusha habari ya mfalme Nebkadneza kwenye Biblia alipoamuru Shadraki, Meshaki na Adebinego watupwe kwenye tanuru la moto uliyokoleza sana matokeo yake waliowabeba kuwapeleka (TBC) motoni wakateketezwa na ule moto na akina shadraki wakiwa ndani ya moto walipeta hata unywele mmoja haukuungua
 
Kimara mabomba yaliacha kutoa maji siku nyingi sana, sasa yanatoa supu ya kuku.
weee ni kuchota tu, kisha unakaa pembeni na kipande chako cha ndimu na pilipili kidogo tu.
 
Mwanza kuna maeneo kibao maji yanatoka usiku tu kuanzia saa sita hadi saa kumi na moja, ziwa liko karibu! hilo ccm haliwanyimi usingizi isipokuwa wanataka kuonyesha watz hata karatu ni hovyo.

CCM toka ikulu wanazlendo tujenge nchi. Muone kama hatujaendelea mbele.
 
KARATU haina maji kwa sababu ya mipango mibovu ya serikali ya CCM.
wanasabotage makusudi ili ionekane kwamba wapinzani wameshindwa kuleta maendeleo. Ukiangalia hata yale majimbo ya wapinzani yenye maendeleo ambayo ccm inatamba ni sera zake, mbona hawatolei maelezo majimbo mengi ya ccm ambayo hayana maendeleo?
SWINE kabisa hawa ccm
 
huwa wanaanza vizuri kweli 'habari za jioni mpendwa mtazamaji wa tbc1' then kinachofuata ni kutuharibia jioni yetu.
 
Mimi natumia king'amuzi chao lakini channel za TBC1 na TBC2 nimeweka ktk PG (parental Guide). hakuna ruhusa kuangalia na sijampa mtu password.
 
Back
Top Bottom