TBC1 na 'Valentine Day' isiyo na Maana Kwetu!

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

Nilikaa kuangalia taarifa ya habari kwenye TBC1 leo saa mbili usiku. Kwa mshangao mkubwa, nikasikia cha kwanza mtangazaji Grace Kingalame akituambia Watanzania ni; " Leo ni siku ya Wapendanao". Sentesi hiyo haikupaswa hata kutamkwa mwisho wa taarifa ya habari.
...
Tunawakumbusha TBC1 , kuwa ni wengi tunaosubiri taarifa ya habari kila ifikapo saa mbili usiku. Hivyo basi, taarifa ya habari ni ' serious issue'. Si jambo la kufanyia mzaha mzaha. Valentine Day ni mzaha wa watu wa Kimagharibi. Hiyo ni siku inayotumiwa kufanya biashara. Haina maana na wala haimsaidii kwa lolote Mtanzania wa Nyarugusu au Malampaka. Na wala si utamaduni wetu. Vingine si vya kuiga.

Maggid Mjengwa,


Iringa,
Mjengwa Blog
 
Ni kweli mkuu; Sisi waafrika tuna kasumba ya kuiga hata yale mambo ambayo hayana faida na tija kwetu.
 
Serious issues na habari kuhusu yanayotokea na kuitafuna nchi wanauchuna, ****** wa Valentino ndo wanatuletea, inatusaidia nini?
 
Alianza na kile alichoona appealing to Tanzanian Audience. we angalia tu thread ngapi zimeanzishwa leo zenye kuhusu valentine, as if it is the most important thing to discuss right now!
 
Mjengwa umenena, si TBC tu, channel zote. Mashetani wameingia katika nyoyo za watu. Hii ilikuwa ni sherehe za kipagani za kwenda uchi (wanga).

Ni ujinga wetu wa kuiga kila uozo.
 
Yani nilipotinga home na kuikuta hii kipindi niliizima Tv kbs!
Yani tuna hasara sana uongozi wa idara zote ktk serikali tawala.
 
what the hell is valentine's day! it has got nothing to do with my love and affection, valentine's day can not mend a broken heart or make somebody love more, love is thru inner willingness of one's heart and not thru valentine's day madness!
 
Hivi hiyo valentine day kwenye public holidays ipo!! Sasa huyu anaanzaje kutupa salamu za valentine day kwenye public tv. Vitu vya kijingajinga kama hivi vinavyotokea nchi za magharibi mara nyingi vinahusisha mambo ya ibada za kishetani msipende kuigaiga kila jambo.
 
Back
Top Bottom