TBC1 na Moudoudo

ECES

Member
Sep 15, 2010
61
24
Habari wakuu, kama kuna kipindi kiliwaha kunivutia TBC1 basi ni ile tamthilia ya kichina ambayo ilitafsiriwa kwa kiswahili Moudoudo na Wakwe zake, kwakweli ilinivutia na nilikuwa naifuatilia vzuri sana lakini cha kushangaza hata kabla haijaisha tbc wakaikatiza bila kutoa taarifa yoyote kwa watizamaji kiac kwamba tumebaki hatujui nini kimetokea kwa tamthilia yetu pendwa yani hawa TBC cjui wakoje inaonekana hawatujali kabisa watazamaji wao...ningependa kama kuna mwenye taarifa zaidi atujulishe kimetokea nini walau tupate kutuliza roho zetu....
nawasilisha...
 
toka tido mhando ameondoka hawa jamaa wamekuwa wababishaji ni kwere, yaani nimetafuta google hata sijaipata, nlitaka kuidownload.
ha ha ha ha mkwe wa maudodo ni kwere, maza kipere sana, angekuwa mkwe wangu ningekimbia nyumba
 
Ni kweli Maudodo ni mvumilivu sana na ni binti wa kipekee kabisa, uvumilivu wake ni zaidi ya uvumilivu wa kibinadamu!!

nafikiri hawa wachina hawaja walipa pesa zao hao tbc1 wachovu,unakatisha tu program kwenye luninga tena ya taifa inaonekana world wide embu badilikeni jamani toeni taarifa huo sasa uswahili.....fools hao wameniudh sana kutukatishia uhondo!
 
TBC wana tatizo kubwa sana tena kwenye habari za tamthilia ndio wanatia kichefuchefu kabisa, zilizopo kila siku zinarudiwa na wakati mwingine zinakatishwa kabla hazijafika mwishom kama hiyo ya kichina.
 
ovyoo kabisa wametukatisha uhondo wa maudodo na kaka yake mwenye vituko kila kukicha.basi toeni taarifalkn wapo kimya hii ni station ya magamba.
 
TBC ndivyo walivyo, tunaomba ITV, StarTV n.k zichukue program MOUDOUDO ianze mwanzo. TBC vipindi vyao havieleweki, vinakatishwa ovyoooo, vinarudiwa rudiwa yani sio ya kuangalia kabisa, hv hamuoni aibu, shame on TBC
 
kweli aisee yani kama kuna uwezekano ITV au StarTV wakakichukua kile kipindi wakichukue manake moudoudo alikuwa ananipa raha jamani.. :pray2:
 
ovyoo kabisa wametukatisha uhondo wa maudodo na kaka yake mwenye vituko kila kukicha.basi toeni taarifalkn wapo kimya hii ni station ya magamba.

Bila ya kumsahau mume wake ambae alikuwa anasema yeye hamuogopi mkewe ila anamuheshimu ila moudoudo akitokeza tuu mshikaji anakuwa mdogo kishenzi.... aarrrgghhh yani we acha tuu hawa TBC1 ni washenzi sana kutukatishia uhondo halafu bila hata ya taarifa......:A S angry::A S angry::A S angry:
 
Kwa kweli TBC sasa hivi ipo katika hali mbaya sana.....Inatia kinyaa, wapo hovyo katika kila Idara.....Taarifa ya HABARI YA HOVYO...kila kitu cha HOVYO....

Watanzania tutamkumbuka sana TIDO MHANDO.....Sijui ni kigezo gani hasa kimewasukuma kusimamisha Tamthilia hii ya DOUDOU na wakweze ambayo waliizindua kwa mbwembwe kweli.....

Vipindi vingi vya burudani vilivyoanzishwa enzi za TIDO havipo sasa.....Mfano Orijino Komedi Show, Bongo Dar es Salaam, Burudani ni Nyumbani(cha Mussa na Lisa), Boda 2 Boda na hata matangazo ya Live ya mpira ya Ligi Kuu ya Uingereza......Kwa ujumla TBC kwa sasa inarudi nyuma kwa kasi badala ya kuendelea mbele...

Huyu CLEMENT MSHANA sijui anafikiria nini hasa...........INASIKITISHA
 
Bora tu, scul tulikuwa hatupumui kila mtu moudodo moudodo. now hamna usumbufu wa kijinga na chaneli zingine wafute tu upuuzi wa tamthilia.
 
Sikuwahi kudhani hii tamthilia ina wafuatiliaji wengi tena watu wazima "dubbed chinese soap".Ilikuwa kila nikikutana nayo nabadili channel haraka.Dah,kweli tupo tofauti!
 
Sikuwahi kudhani hii tamthilia ina wafuatiliaji wengi tena watu wazima "dubbed chinese soap".Ilikuwa kila nikikutana nayo nabadili channel haraka.Dah,kweli tupo tofauti!

Ungejitolea cku moja ukaichek nadhani leo hapa ungekuwa na comment tofauti mkuu....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom