TBC1 inapotumika vibaya: Nani alaumiwe?

Nadhani ni wakati muafaka kwa wananchi tujiandae kuchukua nchi yetu. We had enough of these pranksters and mafioso.
 
Tbc1 inastahili kulaumiwa kwa nguvu zote,kwa kuwa ni chombo cha serikali na kinatumia kodi za wananchi.

RA anatuhuma za UFISADI asingepatwa kutumia chombo hicho kumsafisha .Picha hapa ni kwamba serikali inatetea mafisadi , RA ni Mbunge asinge weza kulumbana kwenye vyombo vya habari badala yake angepeleka Mahakamani kwa kudai haki yake. RA ailichotakiwa kufanya ni kukanusha kuwa si FISADI wa tuhuma zote badala yake naye katoa tuhuma kwa RM ambazo maskini wa wa mungu hazina nguvu zozote sana sana zimewafumbua watu kuwa alicho kisema mengi ni kweli kuwa MAFISADI PAPA hawa wanatumia rushwa . Mfano hotel ya Kilimanajaro Mengi alisema wazi kuwa kuna rushwa imetumika na utaratibu haukufuatwa , tukaambiwa kanunua mtu wa nje Kumbe FISADI RA Alitia mkono wake.

Tunamwomba RA apeleke MAHAKAMANI HARAKA SANA wananchi wote nchi nzima tutamunga MKONO Mengi . Kampuni kufilisika ni kitu cha kawaida , nani siye jua kuwa RA anakampuni nyingi zenye majina tofauti tofauti ambazo zikianzishwa leo zikivuna zinakufa kesho. RA amaekuwa akisema ana wasaidia wananchi wa IGUNGA , Si Kweli amakuwa akiwadhalilisha sana , misaada midogo midogo tu. kwa mfano kuwalipia chanjo wafungaji wote wa jimbo lake ambayo kama shs 200 kwa mfugo . Hiyo siyo misaada tuanyotaka ni rushwa tu.

Ndugu zangu kwa kuwa wameshindwa kuona kipengele cha kumshitaki Mengi kwa kutumia TV yake ndio maana wameamua kumruhusu RA kutumia TV ya taifa ili KU -neutralise mambo hataenda mahakakma .
Serikali isome alama za nyakati hasa JK , kwani tunapoelekea si pazuri , kama tulikula cha watu tukirudishe na tuachane , Hasira za watu zikizidi ,kuzituliza itakuwa ni kazi kweli . Na lawama itakuwa kwako Mheshimiwa JK kijana wetu tunaye kuheshimu, na tunaye taka uendelea hata 2010, lakini mambo kama ndio haya lolote laweza kutokea na kama kukaja kutokea cha kutokea kwa watu wako dhambi hiyo haitasameheka!!!!!
 
Hapana, suala sio vyama hapa. Ni kuhusu Mwanamtandao Mshenzi(Uncivilized) Tido Mhando ambaye anakubali kuwa kuwadi wa mafisadi kwa kutumia television ya umma!

Asha
Asha dada yangu punguza munkali, unajua huyu Tido Mhando aliletwa na Lowassa katika mbinu zao yeye na RA kujipanga kumg'oa muungwana; kwahiyo ni dhahili atatumiwa na RA na mafisadi wengine katika kutetea maslahi yao. Don't count on TBC kuwakwamua wananchi na ndio maana hata walipotangaza hotuba ya Rostam ,hawahuonyesha wakati akishindwa kujibu maswali kwani hapo ndio wananchi wangefahamu utupu wake.
 
Hapana, suala sio vyama hapa. Ni kuhusu Mwanamtandao Mshenzi(Uncivilized) Tido Mhando ambaye anakubali kuwa kuwadi wa mafisadi kwa kutumia television ya umma!

Asha
Asha dada yangu punguza munkali, unajua huyu Dunstan Tido Mhando aliletwa na Lowassa katika mbinu zao yeye na RA kujipanga kumg'oa muungwana; kwahiyo ni dhahili atatumiwa na RA na mafisadi wengine katika kutetea maslahi yao. Don't count on TBC kuwakwamua wananchi na ndio maana hata walipotangaza hotuba ya Rostam ,hawahuonyesha wakati akishindwa kujibu maswali kwani hapo ndio wananchi wangefahamu utupu wake.
 
Huu mjadala watu wanakuwa so emotional for nothing, Dada Asha, kwa sisi tunaoijua TBC ilivyokuwa na ilivyo sasa, please, please, please, leave Tido na timu yake alone!

kipindi cha Fisadi Papa kuhusu fisadi Nyangumi sio TBC production. ni kipindi cha nje, by production house, jamaa kalipia, kosa la Tido lipi.

Hata Mbowe na Chadema akilipia kipindi kinarushwa.

Kile cha Mwembeyanga hata ningekuwa mimi ningekirusha bila majina kwa sababu ni tuhuma. Fisadi Nyangumi alimwaga tuhuma za fisadi papa bila kutoa ushahidi, fisadi papa kamwaga za Fisadi nyangumi na nondo juu. siye dagaa ni kuangalia movie tuu, kosa la TBC lipi?

Hivi kelele zote hizi kuhusu fisadi papa, anayelelewa na JK, halafu fisadi nyangumu anataka kumsaidia JK kumtokomeza fisadi papa, kweli inakuja hii?.

Mzee wetu ana agenda yake, ilidhamiria kulamba dume, tatizo kazichanga vibaya karata zake akalamba magarasa huku mshindani akichezesha mizungu na dume JK yuko mkononi.

Tuendeleeni kudebate ila TBC iacheni kando.

Ukiwa na pesa nchi hii unaabudiwa, mwenye CNN ni Ted Turner, ushawahi kumuona kwenye CNN?. Mwenye Sky ni Rupert Murdoch, ushawahi kumuona kwenye TV?. Mzee wako ni kila kukicha, unataka kumlinganisha na Tido?

Hata ukiwaweka wakae kimya kwa kuwatazama machoni tuu, kama una macho, utaona tofauti, leo unataka kuzielekeza hasira za kipenzi cha watu kuitwa papa nyangumi, kwa kuigeuzia kibao TBC?

Tudadilianeni, tulumbane, tubishane na tukubaliane au tusikubaliane, leave TBC alone.
Pasco, can you declare conflict of interest here!
 
Asha dada yangu punguza munkali, unajua huyu Tido Mhando aliletwa na Lowassa katika mbinu zao yeye na RA kujipanga kumg'oa muungwana; kwahiyo ni dhahili atatumiwa na RA na mafisadi wengine katika kutetea maslahi yao. Don't count on TBC kuwakwamua wananchi na ndio maana hata walipotangaza hotuba ya Rostam ,hawahuonyesha wakati akishindwa kujibu maswali kwani hapo ndio wananchi wangefahamu utupu wake.



Bulesi!

Hapo usimpooze Asha anatumia demokrasia yake!

TBC inamilikiwa na CCM na kwa hilo wametuweka sawa!! Mlipa mpiga zumari ndiye huchagua wimbo period.

Bila kutafuna maneno wote watano waliotajwa ni wafadhili wakubwa wa CCM na according to CCM ni watu safii na Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametoa baraka zake wafanye hivyo!! Hajathubutu kumfukuza kutoka Halmashauri kuu ya ccm ambayo yeye ni Mwenyekiti!!
Baada ya ITV AMBAYO ina coverage kubwa ya nchi wanafuatia TBC!! (japo sina data za kutosha )

TV ya taifa kuganga njaa na kulipwa pesa na ROSTAM aziz kutuambia kwamba mababu zake walipeleka WANYAMWEZI utumwani na bado wale waandishi wapumbavu hawakumchapa makofi pale Kempiski kwenye hoteli yake( AU labda IGP- Said Mwema alimwekea ulinzi kwani yeye na yule Chief wa usalama wa TAIFA aliwateua)

Sijawahi kuona NATIONAL TV inayoingia bifu na private TV's kama TBC!!
Any way hatuna Rais wala utawala si amewaweka mfukoni!! Akitaka JMK au CCM walete ushahidi vinginevyo!!

I don't want to go back kwenye zile blah blah alizotoa huyu kijana asiyekuwa na adabu!!! Angetueleza jinsi aliivyoanza kutengeneza pesa akawapeleka kule DODOMA EL na JMK mwaka 1995 na alivyosaidiwa na visadi kubwa lao BWMkapa kwa kupitia Caspian mpaka leo ameweza kumiliki mdogi wa RESOLUTE;;TICTS; na vinginevyo vingi tu !!kumwajiri William Ngeleja(from mwanasheria Voda Com kuwa waziri wa nishati) na Dr,Idris Rashid kule Tanesco aweze kuendeleza ufisadi pale SONGAS kupitia Pan African Energy na stakes zake na Karamagi kule BUZWAGI.(Mind you mwisho wa Mrach Kikwete alimpongeza Dr. Rashid kwa kutishia kuleta giza)

Huyo Edward Hosea wa takukuru yuko pale kwa maslahi yake na pia Mwendesha mashtaka yule Kijana Eliezer Feleshi (mpwa wake Hosea)amewekwa pale ili asishtakiwe!! (This was well tailored by Chenge na Mwanyika)

Na Mengi anajua hilo ndio maana kama angepeleka ushahidi kwao wasingemshtaki!!! Hakuna mahakama yenye ubavu huo he is above law!!

Sasa tungojee je huyu msanii JMK ataendeleza huu uswahiba kwa kukaa kimya mpaka lini???

Tutarajie vita vya wenyewe kwa wenyewe kwani from here sijui wataelekea wapi!! Let us assume Mengi alikosea na Mkuchika na Simba wakakoroma if they keep quite on RA rubbish then mimi naenda sabatical leave USA mpaka CCM ife!!!
 
Pasco nadhani hii issue imekugusa kwenye rizki..tbc was wrong for this and you know it..bbc hata sikumoja haiwezi rusha malumbano ya watu binafsi kwa kipindi maalamu..nadhani huelewi kazi ya public body. CNN and Sky ni Private wamiliki wakijisikia kujitangaza they can do so, uamuzi tuu!! Kama ulivyosema mwenye Tido na Mengi huwezi linganisha kwasababu Tido ni Mfanyakazi wa SERIKALI!!
No Kapinga, sio suala la rizki maana mimi sio mwandishi, sio mtangazaji, sio producer hivyo sina maslahi yoyote na TBC bali ni katika kupigania ukweli. Huwa najitahidi sana kusimama kwenye ukweli hii ni hulka yangu, ukweli umeishawahi kunicost sana tuu, lami nimesaga sana na bado nasaga kwa sababu ya kusimama kwenye ukweli. Sijidai wala kujivunia umasikini wangu, bali najisikia sifa kuwa masikini jeuri, kufa kizungu na tai shingoni kwa kulala njaa, badala ya kuendekeza njaa. Ndio ukweli huu unaonisikuma kuwaomba msimuingize Tido na TBC kwenye hili. pale ni bussiness as usual.
 
Pasco, Asante kwa uchambuzi wako katika suala hili. Lakini toka lini mbwa akamuuma master wake anayemlisha mabaki ya chakula?
Ni kweli kabisa, mmbwa ni miongoni mwa wanyama waaminifu kabisa kwa masters wao na husimama nao hadi kifo but infortunately kwenye hili, no one was my master, I'm glad to declare, I'm (was) the master of my own game. Kitu ninachopigania hapa ni ukweli kuhusu TBC, that was pure bussiness hakuna politics na Tido mmuache jamaa ni kama mzungu na miaka yake lukuki BBC, asije kasirika JF tunamchimba tukaingizwa kwenye kundi la 'waswahili'
 
Pasco

Pale Mwembe Yanga Dr Slaa na Tundu Lissu walilitoa tuhuma na ushahidi tena kwa kunukuu nyaka za serikali yenyewe. Kwanini TBC hawakurusha?

Halafu tofautisha TV ya umma na ya binafsi, ya umma si suala la fedha tu na kurusha. Inatizama pia maslahi ya taifa. Sasa kama hao TBC wameona maslahi ya Taifa ni kipindi maalum cha Rostam wakaacha Orodha ya Mafisadi na wakakwepa kurusha session contraversial za Bunge tena kwa kuzikatisha kati kati then hatupaswi kuwaacha hao Tanzania Broadcasting Corruption(TBC). Tido anatumiwa!

Asha
Dada Asha heshima mbele, nakubaliana na wewe it might look unfare, waliorusha sio TBC ni kampuni ile iliyoandaa ile press com. Tbc walichofanya ni kuhakiki maudhui na kupokea hela yao.
japo mimi sio TBC lakini nakuhakikishia hata ule mkutano wa mwembe yanga, wangataka kurusha kipindi maalum wangerusha.
kwa msaada binafsi, dada Asha, kama unawafahamu hawa jamaa wa Chadema na wana pesa ya production na airtime, naweza kukuunganisha na jamaa wa PPR kipindi chao kikirushwa sio TBC tuu, bali TBC na ITV na DTV na Channel Ten na Star TV na EATV na CTN na C2C na TVZ na Mlimani TV na Aboud TV na SUA TV. yaani ni mambo ya fungu tuu. TV pekee ambayo hawa jamaa hawajaweza kurusha ni Trenet, Agape na Tumaini TV tuu tena sio wameshindwa, bali hajatokea mteja akataka program yake yake irushwe kule, akitokea, hata huko itapelekwa.
 
Kusema kweli jana mimi binafsi nilifurahi na hapo hapo kusikitika! Nilifurahi kwa sababu tendo la Bwana Mengi hatimaye limtoa nyoka pangoni! Kwa mara ya kwanza tumeshudia mtuhumuwa wa ufisadi namba moja akijibu mapigo hadharani. Hakuishia hapo tu akamtaja Mengi kwa vile vile naye ni fisadi tena kuliko yeye!! Mjadala sasa umeanza kunoga na ni swala la muda tu kujua nani anasema ukweli na nani ni mwongo.

Nawashangaa wale wanaosema mjadala huu ni hatari. Kwa nini? Hizi ni dalili nzuri kwa demokrasia changa kama yetu na hakuna haja ya kuhofia. Namsikitikia Waziri Sophia Simba kwa kujiingiza katika sakata lisilo lake kwa kuwasemea watuhumiwa wakati wenyewe wana midomo na uwezo mkubwa wa kujisemea. Sijui sasa safari hii mama Simba atamkaripia Rostam kwa kumuita Mengi Nyangumi bila kupitia Mahakamani? Au tuseme naye Rostam ni mbaguzi wa rangi kwa kumtuhumu Mengi kuwa fisadi "Nyangumi"? Ugonvi huu kama ule wa wake wenza utatusaidia watanzania kujua mengi.

Kilicho nisononesha ni TBC1 kijiingiza katika sokomoko hili. TBC1 kama yailivyo magazeti ya Daily News na Habari Leo ni 'mdomo" (mouthpiece) wa serikali tofauti na ITV, Channel Ten na Star TV. TBC inapaswa kuwa makini katika mambo sio swala la kulipia pesa tu. Vyombo vya serikali kama TBC ni "vitakatifu" havipaswi kutumiwa kwenye malumbano kama haya ya wafanya biashara. TBC ilipaswa iwe "neutral" na hata wangeletewa furushi la pesa wangekataa kurusha kipindi maalum cha Rostam bali wangeishia kwenye taarifa ya habari tu.

Kufanya hivo ni kuonyesha wao wako upande gani kwa sababu tunajua fika kitendo cha TBC1 kurusha kipindi maalum kama jana kinawezekana kwa mkono wa Rostam Aziz peke yake na si vinginevyo. TBC1 inatuonyesha nini kwa kuonyesha ushabiki wa wazi wazi katika malumbano haya ya wafanya biashara? Waingereza wanasema "who pays the piper calls the tune". Kwa kukubali kupokea pesa za Rostam kurusha kipindi maalum TBC1 imejidhalilisha mbele ya umma. Haya mambo waachiwe kina ITV, Channel 10 na Star TV sio TBC1.

Inajulikana kwamba Rostam ameisadia serikali ya nne kuingia madarakani na uenda TBC1 kama chombo cha seriakali hii ilitumiwa kulipa fadhila. Sisi kama wananchi tunaomba huu uwe mwanzo na mwisho wa kufanya mambo kama haya. Lakini hii yote inaashiria udhaifu mkubwa wa serikali hii. This government is caught between the rock and hard place na haijui cha kufanya. Kwa kitendo cha jana nasema TBC1 ziiiii!
 
Wadau wa blog huwa mie napenda sana kuanza kazi na kuimaliza na ndio maana huwa nakaa pembeni mara nyingi,mie nina idea moja ambayo tukiinzisha le tutapata matunda hata kama ni kidogo kama nchi za waatu walioendelea:

TUSUSIE:
1. TBC- ZAWADI YA TIDO MUHANDO
2. HABARI LEO -ZAWADI KWA LOWASSA (ALIZINDUA KUDUMISHA UFISADI)
3. DAILY NEWS (I WISH MWL JKN ANGEKUWEPO)
4. MICHUZI BLOG -ANAVUKA MIPAKA KWA HABARI ZA UCHOCHEZI HUYU-NINA MPANGO WA KUMRIPOTI GOOGLE
5. HABARI CORPORATION IMESHAKUFA WANAISHI KWA HELA ZA RA
6. MWANANCHI CORP-INAELEKEA KWA HABARI CORP. (WAKENYA HAWAFAI)
7. CHANNEL 10 - TRAMPATONA ACHUNGUZWE NA IKIWEZEKANA ARUDISHWE KWAO
 
Hii Mwananchi si nasikia fisadi no 1 kajitoa kwa kuuza share? Au bado yuko kwa mlango wa nyuma? Nielimishe tafadhali.
 
Nafikiri ingefaa zaidi ungesema TBC ni sauti ya Mafisadi nambari wani.
 
TBC OYEEEEEEEE.....!
ONA WANVYOKUGWAYA, ENDELEZA KUTOA HABARI ZA UHAKIKA NA ZENYE UHAKIKA......!
HAWA WATAUWA VIZABIZABINA WASIOITAKIA MEMA TANZANIA YETU....! mimi hupenda kusikiliza na kuangalia TBC kwa habari za uhakika na zenye tija.....!
Pata habari motomoto kutoka kwa wahusika na si POROJO, UVUMI NA MINONG'ONO KUTOKA REDIO MBAO ZINAZOISHIA MAGOMENI.....!
ukiona wanakuandama jua kuwa wameona juhudi zako........!
KEEP IT UP TBC.....!
 
TBC OYEEEEEEEE.....!
ONA WANVYOKUGWAYA, ENDELEZA KUTOA HABARI ZA UHAKIKA NA ZENYE UHAKIKA......!
HAWA WATAUWA VIZABIZABINA WASIOITAKIA MEMA TANZANIA YETU....! mimi hupenda kusikiliza na kuangalia TBC kwa habari za uhakika na zenye tija.....!
Pata habari motomoto kutoka kwa wahusika na si POROJO, UVUMI NA MINONG'ONO KUTOKA REDIO MBAO ZINAZOISHIA MAGOMENI.....!
ukiona wanakuandama jua kuwa wameona juhudi zako........!
KEEP IT UP TBC.....!

mhhhhh.. pole sana
 
TBC OYEEEEEEEE.....!
ONA WANVYOKUGWAYA, ENDELEZA KUTOA HABARI ZA UHAKIKA NA ZENYE UHAKIKA......!
HAWA WATAUWA VIZABIZABINA WASIOITAKIA MEMA TANZANIA YETU....! mimi hupenda kusikiliza na kuangalia TBC kwa habari za uhakika na zenye tija.....!
Pata habari motomoto kutoka kwa wahusika na si POROJO, UVUMI NA MINONG'ONO KUTOKA REDIO MBAO ZINAZOISHIA MAGOMENI.....!
ukiona wanakuandama jua kuwa wameona juhudi zako........!
KEEP IT UP TBC.....!
safi sana
naona payroll inafanya kazi yake hapa
 
Jamani wandugu wapinga ufisadi, lolote lile linalotokea la kuvunja moyo please,....wala lisitutishe ndiyo kwanza tuzidi kushambulia adui ameongeza mashambulizi, lakini avuja! anvuja damu keshajeruhiwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom