TBC1 - Huu ni utapeli

analysti

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
729
612
Ukifuatilia taarifa ya habari ya saa mbili usiku TBC1, utakutana na tangazo "mpenzi mtizamaji yuma maoni yako kwenda namba fulani hivi, na maoni yako yatarushwa katika live kwenye taarifa hii ya habari". Ndugu wana JF namba hii unayo tuma hayo maoni ni zile namba ambazo unakatwa hela zaidi ya gharama ya meseji ya kawaida!!. Mara nyingi hutumika katika baati nasibu na huduma nyingine ambazo huu utaratibu huwa kama ndo njia ya kukusanya malipo yake. Sasa TBC hupokea hizi meseji kutoka kwa watanzania(poor people) wasioelewa huu utapeli na kisha husomwa meseji tatu nne hivi!!!. Sasa kama TBC wanaendesha bahati nasibu ni bora wawatangazie kabisa watanzania kwamba ukibahatika meseji yako itasomwa na watangaze na hiyo gharama ya meseji!!.
 
Hehehe unapotuma maoni si unataka ujumbe wako usomwe na usikike kwa watanzania wote? Na pengine na jina lako litangazwe nchi nzima? Hiyo ni huduma tofauti na msg unayomtumia rafiki yako, kwa hiyo lazima ukatwe zaidi.
Na la pili, katika hali ya kawaida si rahisi kwamba TBC wataweza kusoma maoni yote ya wasikilizaji. Kwa mara moja huwa kuna watanzania wangapi wanaosikiliza TBC? Na unafikiri huwa zinatumwa msg ngapi? Nafikiri siyo rahisi kusoma msg zote kwakweli.
 
Umeanza vizuri sana ila utapeli upo hapo kwenye red mkuu. TBC1 wanajua wazi hawawezi kusoma msg zote sasa ni kwa nini bado wanaahidi kutekeleza hilo????????????????????????? Wizi mtupu
 
Sio wizi mkuu!!

Unapotuma hizo premium msg unajua kabisa kuwa hawatazisoma zote lakini unajipa matumaini kwamba labda yangu itasomwa!. Kwani umeshasahau miaka ile tulipokuwa tunatuma kadi za salamu? mbona zilikuwa hazisomwi zote lakini bado wiki ijayo mtu unatuma tena na tena mpaka hapo itakaposomwa then unajisikia vizuri rohoni....:A S tongue:

Pia unatakiwa kusoma zile terms zinazoambatana na hiyo shughuli kabla hujatuma msg yako. Hii itakusaidia sana kujua gharama halisi.
 
Shame on them!

Usiwatetee ni ujinga, wizi na utapeli unaoendelea hapo. Wanafidia gharama za hisani wanazotoa kwa CCM kwa kuwaibia Wadanganyika wanyonge, watoe hadharani gharama za kubinafsisha TV ya taifa kwa chama siku mbili tena channel zote mbili na kama wamelipwa!!!!!!! Na wadanganyika nao wamezidi kudanganywa na agenda za kitapeli SMS wao, DECI wao, Upatu wao, nk. nk. nk. Tuwe tunajiuliza kwanza kabla ya kuingizwa mitegoni
 
Sorry Kwetunikwetu! Nimeteleza nilikuwa na quote Bantugbo (5) hapo juu
 
Haya mambo ya msg huwa hayana maana yoyote labda kwa wengine ..ni namna ya kuingiza fedha kwao na kwa kampuni za simu.. kwanza hawasomi msg zote
 
Ukifuatilia taarifa ya habari ya saa mbili usiku TBC1, utakutana na tangazo "mpenzi mtizamaji yuma maoni yako kwenda namba fulani hivi, na maoni yako yatarushwa katika live kwenye taarifa hii ya habari". Ndugu wana JF namba hii unayo tuma hayo maoni ni zile namba ambazo unakatwa hela zaidi ya gharama ya meseji ya kawaida!!. Mara nyingi hutumika katika baati nasibu na huduma nyingine ambazo huu utaratibu huwa kama ndo njia ya kukusanya malipo yake. Sasa TBC hupokea hizi meseji kutoka kwa watanzania(poor people) wasioelewa huu utapeli na kisha husomwa meseji tatu nne hivi!!!. Sasa kama TBC wanaendesha bahati nasibu ni bora wawatangazie kabisa watanzania kwamba ukibahatika meseji yako itasomwa na watangaze na hiyo gharama ya meseji!!.

QUOTE]

hili ni swala zito!!naomba lifikishwe TRA NA SHIRIKA LA BAHATI NASIBU...wanatakiwa wawe wanalipa kodi na hilishirika kujua kinachendelea...
thanks for info
 
Nafikiri huwa wanalipia .kama hawalipii kwa tume ya mawasiliano,tra,whatever, basi wafunguliwe kesi.halafu huo utaratibu unaboa hasa ukizingatia ni national broadcasters,watafute njia ya kubuni kipindi kingine cha kutoa maoni sio lazima wakati wa news 2.waige kwa itv.
 
User Beware.
Jamaa walitakiwa watoe taadhari [Disclaimer] kwamba ukituma meseji basi hapo Tshs.500 inatozwa au wafuate kale ka msemo ka wadau wa mawasiliano ya vinganjani kwamba: Vigezo na masharti kuzingatiwa. Makampuni nguli ya habari kama Sky News et al utoa kabisa taadhari kwamba viwango vya kutuma sms zitatoza na anayetoa huduma[service provider] wako.
 
TBC ni chombo cha umma na wewe unaekatwa pesa kwa kutuma msg ni mmiliki, shida iko wapi?
 
TBC ni chombo cha umma na wewe unaekatwa pesa kwa kutuma msg ni mmiliki, shida iko wapi?

Ni chombo cha umma kinadharia na si kiutendaji!! Hatakama kingekuwa chombo cha umma kiutendaji, mtu unatakiwa uchangie kwa ridhaa yako. Ufahamishwe kuwa kutuma meseji ni shilingi ngapi na pia uambiwe kuwa ile ni bahati nasibu, kwamba ukibahatika meseji yako itasomwa na kama ni vinginevyo ujaribu tena kesho. Sasa wao wanatangaza as if watazisoma meseji zote na they don tel the poor Tanzanians how much that messege costs!!. Hapa ndipo utapeli ulipolala, na wao wanalijua hilo, na wanaendelea kufanya kila siku. Ni nani wakuja kuwatetea watanzania, ambao kutoelewa kwao kunakuwa ni mradi kwa taasisi zao wao wenyewe!!! Mungu tusaidie Tanzania. Wanaazia kwenye chaguzi sasa hadi huku!!!?
 
Back
Top Bottom