TBC1, hata hili linahitaji mjadala? Chonde Chonde Tubadilike

Mzalendowetu

Member
May 22, 2012
87
34
Wakati wa taarifa ya habari ya TBC1, nimekuwa nikisikia (hata jana saa 2 usiku) mtangazaji akisema '.......Habari yetu Muhimu ya Leo' akiwa anamaanisha miongoni mwa habari zote zilisomwa siku hiyo, kuna moja ambayo ni muhimu. Binafsi huwa najiuliza, habari hiyo ni muhimu kwa watazamaji, watangazaji au TBC1 yenyewe kama kituo?. Naamini kwamba habari zote ni muhimu kulingana na mtu husika, kazi anayofanya na mazingira anayoishi. Kuna watu huwa wanatazama michezo tu, wengine siasa etc. Ndugu zangu wavuvi wao hupenda kufuatilia habari za hali ya hewa pekee.

Chonde! Chonde!, tubadilike
 
TBC1 hawako makini katika taarifa zao, kama habari si muhimu wasiitangaze.
 
Acha kumaliza muda wako kuwajadili hawa jamaa ni wapuuzi sana hakuna wanachokifanya zaidi ya kula kodi za watanzania kwa kusafiri na wakuu wa nchi, ndo maana wanapeana zamu.Kila siku hakuna taarifa yao ambayo haina neno KUMRDHI ni wezi wa rasilimari za taifa maana vifaa wanavo lakini kila siku hakuna kinachoendelea
 
sasa wao wamesema ukweli,katika habari zao wamesema kuna habari nyingine muhimu nyingine zinasindikiza,ulitaka wadanganye? mimi nimependa kwa wao kuwa wakweli
 
hapo jua hawana habari, wewe wakimaliza hiyo muhimu zima tv maana hizo zingine hamna kitu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom