TBC1 bora muache kabisa kusoma MAGAZETI

'..................Ninafahamu vizuri shida mnazopata kina mama, kwa sababu mama yangu amenisomesha kwa kuamka saa 11:00 alfajiri kwenda soko kuu kununua mboga akifukuzwa na mgambo wa halmashauri ili apate fedha za kunisomesha, leo hii ni mgonjwa wa kifua kutokana na baridi, mvua na jua kali.........' Nassari

Imenifanya nilie,
Huwa napigania sana mbuge amabye ni mkazi wa eneo husika. Ona Ndesamburo, shida zilizopo Moshi ni zake, anaziona day in day out, hasimuliwi.
Yani yuko in touch na hali halisi.
Sio kwamba ana majibu yote, bali atakuwa na feelings za ukweli na pain, na struggle itakayokuwa inafanyika.
Arumeru mkimkosa huyo dogo tutawapeni pole miaka mingi sana ijayo.
 
leo wamesoma magazeti mawili tu ya uhuru na habari leo wakati walikuwa na magazeti yote kisa chadema imeanika uporaji wa mkapa na magazeti yote yameandika. Mjue mmepoteza fedha za umma kununua magazeti halafu hamsomi kama vp muache kabisa program ya magazeti msiige itv na startv

Wamesoma magezeti matatu, Uhuru, Habari Leo na Zanzibar Leo. Huu kwa kweli ni upuuzi yaani kituo kinaongwa kwa kodi zetu alafu wanatuchagulia habari. Haipenzi Bw. Mshana jua hilo. Hatakama unahofia yaliyo mkuta Tido simamia taaluma yako kama huwezi Sepa mzee
 
...na wanaotuma sms wanatuma zenye mrengo mmoja tu! Yaani ni kusifia tu hatujui upande pili. Kiukweli inaboa.
 
Hawa wamenunuliwa na hawana kwa kwenda ni lazima wafuate amri ya analinda japokuwa sisi walipa kodi ndiyo tunaowalipa hizo pesa za kuvaa suti uchwara
 
leo wamesoma magazeti mawili tu ya uhuru na habari leo wakati walikuwa na magazeti yote kisa chadema imeanika uporaji wa mkapa na magazeti yote yameandika. Mjue mmepoteza fedha za umma kununua magazeti halafu hamsomi kama vp muache kabisa program ya magazeti msiige itv na startv[/QUO

Kama mnakumbuka juzi wafanyakazi wa KBC waligoma na walikuwa wakiitaja KBC kama Kazi Bila Chakula. Wafanyakazi wa TBC wanasema Taarifa Bila Chadema! Tafakari. Alafu tabia yenu ya kufikiri TBC ni idhaa ya taifa nani kawaambia jamani? Hii inaeleweka ni kwa ajili ya propaganda za CCM zienee kote hasa vijijini. Ingawa hela wanazotumia ni zetu watz
 
Nilikuwa nataka kuanzisha post ya kuhusu utaratibu wa TBC siku hizi, ila naona na ww umewaamkia kwa jingine, naomba kuunganisha.
Hawa jamaa wamepoteza wafanyakazi au mwelekeo?
Taarifa zao za habari zimekua hovyo sana hadi nawaonea huruma na aibu wale wasomaji, hawana mpangilio, picha zinajichanganya, mara hazitokei, graphics zinaptiliza screen, maandishi hayaonekani, mara msomaji haonekani.

Jana jioni nilikuwa na angalia News TBC na binti yangu hatukuamini tulicho kiona na kusikia - taarifa zilikuwa aziendani na picha husika, wakati mwingine tulikuwa tunasikia channel mbili at the same time, na upande wa lip synch ulikuwa vivid kabisa, Ndugu mkurugenzi mkuu ambaye nakuheshimu sana kwa uchapa kazi wako - Hebu twambie kinacho endelea kwenye Chombo chako cha Kitaifa?

Ndugu Mshana, tatizo la TBC siyo watangazaji, tatizo liko upande wa matumizi ya tekinolojia-vifa wanavyo lakini jinsi ya kuvitumia kiufanisi hilo hawana, I can asure you kwamba watu walio wekwa pale ni wababaishaji na sitashangaa kama siyo ndugu au rafiki za wakubwa. Mimi sioni ni kwa nini Mkurugenzi upande wa Technical hasiwekwe to task, shughuli zake ni nini hasa kama awezi kusimamia chombo hiki muhimu cha Taifa ana faida gani pale! TBC wanashindwa na jamaa walioanza juzi juzi wa AGAPE ambao resources zao ni ndogo sana lakini wanatoa vitu vya huakika, lakini wenzetu ni wazito sana kubadilika; kwao ni business as usual si wanapata ruzuku kutoka Serikalini kwa nini wahangaishe vichwa vyao.

Nendeni mkapate mafunzo kwa vitendo kutoka ITV au STAR TV sina shaka watawasaidieni sana, sisemi haya kwa nia mbaya, inauma sana kuona chombo cha kitaifa kinacho pata msaada wa kila aina kinashindwa kufanya kazi kwa kiufanisi. Nataka niweke wazi kwamba Mkurugenzi Mkuu wa TBC ni mtu mahiri na msikivu, kama anataka kuleta mabadiriko TBC basi atupie macho upande wa kiufundi na editing.
 
Kwani kazi yao kusoma magazeti au kutangaza habari?
Unachekesha, magazeti huwa hayana habari yana nini?...

Waondoe kipindi cha mapitio ya magazeti na sio watuletee ukilaza wa kutusomea magazeti ya chama cha mapinduzi.... Aliyewaambia tbc ni mali ya ccm ni nani?
 
msimlaumu mtangazaji muulizeni kilochompata TIDO MHANDO jamaa anaepuka malumbano na waajiri wake tumia TV nyingine
 
simple, huwa nazima na huwa ni ara chache sana naangalia TBC
 
Habari Leo, Daily News, TBC1,2 na TBC Taifa vyote kwa sasa vinamilikiwa kibabe na CCM. Yani ni kama wanavyomiliki kibabe viwanja vya michezo na majengo meeeeeengi nchi nzima.
 
kiukweli wanapoteza tu muda wao sasa hivi taarifa zinapatikana kila kona na ndio maana kwa kifupi hata sina time ya kupoteza kuangalia hiyo tv,utandawazi umewamaliza ila wakumbuke wanachezea kodi zetu ipo siku wataumbuka
 
Nabado ni lazima wakae joshua nassari anakubalika zaid ya yule wao anayejiita sioi ilhali hadi watoto anao ,yaani jina lake linasadifu hali halisi kuwa ni muongo na piaaaaaaaaaaaaaaaaaa magaaaaaaaaaaambaaaaaaaaaaaaa hawana cho hapa arumeru na vilago vyao viko tayaaaaaaaaari kabsa kufungashia aibu yao siku ya uchaguzi.
 
Nilishachoka kuanjgalia TBC 1 maana is too biased(CCM 100%). ila inauma sana wanavyocheza na kodi zetu kwa kufanya kama kituo ni cha wao CCM na kuiremba remba serikali hii ya kimatako ******.

Ifike mahali watanzania we stand together na kuamua either tusiwe na televison ya taifa au radio ya taifa ambazo zinatumiwa kwa manufaa ya chama kimoja yaani CCM. Hakuna haja ya kuwa na upuuzi kama huu.

Imagine watu wa vijijini ambao wataweza kuona TBC wataamini use**e unaotangazwa na kuandikwa humo.

Yaani kuanzia mfagizi,mlinzi,mameneja mpaka mkurugenzi ni wamekaa ki CCM tuu,na ndo maana ni wajinga wa kufikiri,they lack confidence kwa sababu hawana sifa,si wasafi kuweza kukemea mwingine ama kujitetea coz they fake kuanzia qualifications,umri,etc.

I cant wait to hear and see CCM siku itakapozikwa rasmi, maana kufa imeshakufa nusu inaelekea 3/4(three quarter). We are counting days.....
 
nilikwisha sema tbc ni tawi moja wapo la ccm.....nchi hii ilishaingia kwenye mfumo wa vyama vingi lakini hadi leo bado haijaukubali mfumo huoo.....1
 
ila kwa kweli taaarifa za sasa za habari TBC ni ovyo kabisa yani haipiti siku hawajaharibu jambo,sasa sielewi mitambo yao imeharibika imezeeka au wanaotayarisha kipindi hawajalipwa mshahara au vp.
 
Kiukweli TBC imepoteza mwelekeo, hakuna time management tulizoea ikifika saa 12 unasikiliza habari, saa 12 na dakika 10 mahojiano, saa 12 na nusu habari za michezo na 12 na 45 magazeti, sasa siku hizi hata huo mpangilio ni hovyo. Kiukweli waambieni Orijino Komedi watoe hilo kwa kuwa wamezoea kukosoa wengine na sasa mkosoane.
Wengine wanaoboa ni hawa Channel 10. Leo nimekaa zaidi ya dakika 8 nasubiri waanze kipindi chao cha mahojiano ile asubuhi nikaona wanatuyeyusha na matangazo tuuuuuuuuuuuuu nikahama channel, kufika TBC ndo ugonjwa kabisa nikaenda CITIZEN TV nikakuta mambo muktadha kabisa.
Jamani mwenye mtaji wa kutosha amuite Tido aje kuanzisha kituo chake tupate uhondo
 
Back
Top Bottom