TBC wasitisha matangazo LIVE bungeni

Mi naona afadhali PM angesepa na wangesema yuko Arusha na wangeendelea na mambo mengine kama kawa maana sio mara ya kwanza kusepa. Hii staili waliokuja nayo ni ya kizamani mno.
 
Mi naona afadhali PM angesepa na wangesema yuko Arusha na wangeendelea na mambo mengine kama kawa maana sio mara ya kwanza kusepa. Hii staili waliokuja nayo ni ya kizamani mno.
 
Hapa dili ni wabunge wa upinzan wote kugoma mpaka lionyeshwe live
mpaka kieleweke wapiga kula tunataka tuone kilichowapeleka mjengoni!
Kwa hayo mabunge ya nje ambayo huwa wabunge wanazpiga kavu kavu na linakuwa live wao ni wanyama sisi ndo binadamu?
Umburula tu na kuficha maovu!
 
Samahanini hivi haiwezekani stations nyingine kurusha bunge live pasipo kupitia TBC? Au ndo mpaka wadhamini kisa ni private au hairuhusiwi tu?
 
TBC ni janga la kitaifa mara kumi hata Clouz ambayo ugonjwa wake unaeleweka.
 
"Mtazamaji wa TBC1,hatutaweza kuwaletea matangazo ya bunge kutoka dodoma kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu mpaka hapo tutakapowataarifu tena, tunaomba radhi kwa usumbufu" hivyo ndivyo tangazo linavyosomeka hapa tbc1

Wakuu, let us wait. Truth never dies. Ukweli utajulikana tu.
 
kookolikoo;6316236]hawako hewani si redio
wala luninga. hakuna sababu yoyote iliyotolewa zaidi ya mtangazaji wa
zamu kusema anasikitika hakutakuwa na matangazo toka bungeni hadi
tutakapoarifiwa tena

VIPI KUHUSU STAR TV NAO SI HUWA WANAONYESHA AU NAO NI TBC 2?
 
Nyie watu, Bunge ni chombo huru, Waandishi wa habari, TV Za serikali Na watu Binafsi mnaruhusiwa kuingia Na kureport AMA live au Kwa makhtadha Yale yanayojiri pasipo kuvunja Sheria Za Nchi au kufanya uharibifu mradi tu nafasi hiyo inapatikana Ndani ya Bunge letu..

Hakuna TV au Redio iliyoomba kureport matangazo ikakatazwa unless Sheria ibadikike kitu ambacho si rahisi Kwa Sababu Bunge ni la wananchi.
 
Wanabodi:
Mimi na wewe kama walipa kodi wa nchi hii ambayo kwa njia moja ama nyingine ndiyo inasaidia kuendesha television ya taifa TBC,sasa naona ni bora ikaondolewa ruzuku hiyo kwa kutotimiza wajibu.Kuna mtu kanidokeza kuwa TBC si chombo cha Umma bali ni chombo cha Seriakali(kuna tofauti kubwa kati ya mali ya Umma na Serikali).

TBC imeshindwa kukidhi mahitaji au matarajio ya wananchi kwa maana ya wamiliki wa hiki kituo.

tazama hoja zenye maslahi ya jamii wao wanafanya ya kwao,urushaji matangazo ya moja kwa moja matatizo,ukitazama website yao hakuna habri mpya nk.

wana kipindi kinaitwa ZE COMEDY ambacho licha ya kuchekeza hivi sasa wanarusha matangazo ya biashara tu,huku wakitoa matangazo mpaka ya aibu kabisa katika TV ya taifa ,hata kama ni vichekezio.huwezi kutoa kichekezo kuwa 'chachandu ya chakula kwa wanandoa ni CONDOM' tena bila kuonesha kuwa ni uongozo,watoto wetu wanatazama huu upuuzi.

Tazama website yao leo katika kitengo cha video.

Video

na tazama website ya KBC (Kenya) na UBC (Uganda)

Kenya Broadcasting Corporation

http://ubc.ug/ubc/index.html

Nina mengi ,nitarejea
 
Wako sawa kwakuwa TBC inaendeshwa na fedha zao mifukoni na si kodi za watanzania,siku yaja watakuwa nje ya mfumo huu ndipo wataelewa nini maana ya television ya Taifa.
 
Haya ni maoni ya wadau,yaliwekwa katika post kadhaa humu jF juu ya mustakabali wa TBC,kwa kuwa yanaendana na hoja hii,nimezitafuta.nitaleta nyingine.mpaka kieleweke

Sasa ni lazima wananchi wote tuchachamae na kuihoji TBC, ni kwa nini chombo hicho kinaendeshwa kwa kodi zetu sote, wanachama wa CDM, wa CCM, na wa vyama vingine,lakini wao wanakiendesha kwa maelekezo ya ofisi ya Lumumba?!

Haihitaji mtu uwe na degree,ujue sababu ya kusitisha matangazo ya bunge leo,ni kuwa hivi leo ni siku ya maswali ya papo kwa papo,na kutokana na matukio mfululizo yaliyotokea nchini,kama vile matokeo ya kidato cha nne kufutwa, suala la Mwigulu na wenzake wa usalama wa Taifa kuwabambikia viongozi wa CDM,makosa ya ugaidi na tukio la kulipuiiwa kwa bomu, kwa kanisa la Arusha,ni dhahiri maswali ya kiongozi wa upinzani bungeni,Mbowe na makamanda wengine wa CDM,ni dhahiri leo bungeni kungrkuwa na shinikizo kubwa la vigogo wa CCM,kuachia ngazi,jambo ambalo Pinda,angeshindwa kulihimili,badala yake angebakia kutoa machozi kama ilivyo kawaida yake!!

Sasa kwa kuwa TBC,siku zote inafanya shughuli zake kwa kulinda maslahi ya CCM na viongozi wake, wameonelea wasitishe matangazo hayo,ili kumuepusha mzee wetu Pinda,kuonekana kwenye luninga akimwaga machozi ya kufa mtu!!!

TBC kwasasa wana mkurugenzi msikivu. Na lazima ajifunza yaliyomtokea Tido Muhando, haiwezekani kabisa Viongozi wanakuambia achana na Midaharo weka Ze commedy wananchi wafurahie wewe unang'ang'ania Midaharo tu.

hiki chombo kwa kweli akina nguvu ata kidogo TBC ina matatizo mengi sana kiuchumi kati mashirika ya serikali yalitelekezwa na kupewa watendaji vibaraka ni TBC hali yake ni mbaya sana kile kipindi cha kusoma taarifa ya habari kwa kutumia kibatari pale RTD (TBC TAIFA) NYERERE ROAD. inarudi akika.

"NI BORA KUPIGANA NA MTU ANAESIKIA KULIKO KUPIGANA NA KIZIWI KWANI ATA KAMA AMEKUZIDI NGUVU HAWEZI KUKUACHA HADI DAMU IKUTOKE"

Kuna kipindi watajikuta wanashindwa kutangaza chochote kwa kuhisi sasa kila kitu kiko against CCM. Manake mambo yanazidi kuongezeka kila siku. Bora waanze kuachane na matangazo yote tu kuanzia sasa, wapige taarabu manake mitaa ya pwani ina washabiki wengi.

Wanaficha uozo wa ccm wakati kila mtanzania anaujua mahakama imewaumbua baada ya kutenda haki!!! sioni maana ya tbc bora wazipe channel nyingene ridhaa ya kurusha live vipindi vya bunge, watu leo tulitaka kuckia kutoka serekalini kuhusu tuhuma za ugaidi dhidi ya chadema lakini ccm wametunyima haki yetu ya kupata habari!!! ccm + tbc ni wakuchingia baharini
 
Sidhani kama TBC wamekatazwa kurusha matangazo yumkini kuna tatizo kiufundi. Tusubiri kwanza tuone tatizo ni nini, tusitoe hukumu kwanza. Bunge ni letu na TBC pia ni yetu.
 
Atu!
Ukubwa wa miaka/mwili au cheo si tija. kuwa junior hapa si topic. pengine ungekuja na sbbu kwa nn hakuna matangazo ya bunge live leo?
 
Tetesi ni kwamba wana kikao cha ghafla na cha dharura na mkuu wa nchi, yamemfika shingoni.
 
Wanabodi:
Mimi na wewe kama walipa kodi wa nchi hii ambayo kwa njia moja ama nyingine ndiyo inasaidia kuendesha television ya taifa TBC,sasa naona ni bora ikaondolewa ruzuku hiyo kwa kutotimiza wajibu.Kuna mtu kanidokeza kuwa TBC si chombo cha Umma bali ni chombo cha Seriakali(kuna tofauti kubwa kati ya mali ya Umma na Serikali).

TBC imeshindwa kukidhi mahitaji au matarajio ya wananchi kwa maana ya wamiliki wa hiki kituo.

tazama hoja zenye maslahi ya jamii wao wanafanya ya kwao,urushaji matangazo ya moja kwa moja matatizo,ukitazama website yao hakuna habri mpya nk.

wana kipindi kinaitwa ZE COMEDY ambacho licha ya kuchekeza hivi sasa wanarusha matangazo ya biashara tu,huku wakitoa matangazo mpaka ya aibu kabisa katika TV ya taifa ,hata kama ni vichekezio.huwezi kutoa kichekezo kuwa 'chachandu ya chakula kwa wanandoa ni CONDOM' tena bila kuonesha kuwa ni uongozo,watoto wetu wanatazama huu upuuzi.

Tazama website yao leo katika kitengo cha video.

Video

na tazama website ya KBC (Kenya) na UBC (Uganda)

Kenya Broadcasting Corporation

UBC.ug - Uganda Broadcasting Corporation - UBC TV

Nina mengi ,nitarejea

tbc website is a turd.
 
Back
Top Bottom