TBC wasitisha matangazo LIVE bungeni

Wakuu, mbona mnaongelea kitu ambacho hamna uhakika nacho? Ni bora tukafanya subira ili tupate ukweli juu ya nini kimetokea. Kwani ni haki ya wananchi kupata matangazo ya bunge. Wabunge tumewachagua kwa kura zetu na hivyo ni vyema tukatumia muda huu wa bunge kupima uwezo wao ili tuamua kama 2015 tuwe nao tena au tuchague wengine wanaotuwakilisha vizuri

Mkuu, tusubiri nini tena wakati matangazo ndo ivo tena yeshakatwa? Wangekuwa waungwana kama wangetoa sababu basi, sasa unaambiwa mtangazaji kasema tu hawatajiunga Dom bila kutoa sababu. Wewe unaona bado wana maana hao?
 
Inasikitisha sana Watanzania hatuna uhuru na vyombo vyetu vya umma ila vinatumiwa na watu wachache kwa maslai yao. waliopo bungeni watujuze yayoondelea huko
Mkuu, heri ya wewe angalau umependekeza jambo la maana. Ninaamini tuna wabunge wanachama wa jf. Watumie muda huu wakati bunge haliko live kutujuvya kinachoendelea badala ya kukimbilia kuomba miongozo na wengine kulala
 
Mkuu, tusubiri nini tena wakati matangazo ndo ivo tena yeshakatwa? Wangekuwa waungwana kama wangetoa sababu basi, sasa unaambiwa mtangazaji kasema tu hawatajiunga Dom bila kutoa sababu. Wewe unaona bado wana maana hao?
Wamesema kuwa kwa sasa hawatajiunga bungeni dodoma kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao. Watatujulisha zaidi hapo baadaye. Tusubiri. Naamini TBC wanalipwa pesa za walipa kodi kutokana na matangazo yao. So wana haki ya kutujulisha sisi walipa kodi ni nini kinaendelea
 
Dr.F.Ndugulile naamini uko bungeni,kulikoni tena?au na wewe unaogopa kukisaliti chama chako?najua wengi mko huko CCM kwa njaa tu ila mioyo yenu iko CHADEMA!
 
Last edited by a moderator:
Bila shaka maswali ya papo kwa papo leo hii yangelenga sana mlipuko na uchakataji wa matokeo ya kidato cha 4 2012. TBC wamepigwa pini kurusha live. Hii ndo bongo bana.
Du, kweli wewe si great thinker. Ndo maana tangia 2012 mpaka sasa bado ni junior member humu jf
 
Ben saanane uko wapi? Au ndo unasherehekea kufutiwa mashitaka ya ugaidi lwakatare umesahau majukumu yako humu mtandaoni
 
Samahani watazamaji na wasikilizaji wetu tuko kwenye shamrashamra utiliaji saini mkataba wa ushirikiano na Radio Uhuru chini ya mkurugenzi mmoja hapa Rumumba, tutarejea mara tu baada ya shuguli hii.
Ahsante na poleni kwa usumbufu!!
 
"Mtazamaji wa TBC1,hatutaweza kuwaletea matangazo ya bunge kutoka dodoma kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu mpaka hapo tutakapowataarifu tena, tunaomba radhi kwa usumbufu" hivyo ndivyo tangazo linavyosomeka hapa tbc1
 
Sasa ni lazima wananchi wote tuchachamae na kuihoji TBC, ni kwa nini chombo hicho kinaendeshwa kwa kodi zetu sote, wanachama wa CDM, wa CCM, na wa vyama vingine,lakini wao wanakiendesha kwa maelekezo ya ofisi ya Lumumba?!

Haihitaji mtu uwe na degree,ujue sababu ya kusitisha matangazo ya bunge leo,ni kuwa hivi leo ni siku ya maswali ya papo kwa papo,na kutokana na matukio mfululizo yaliyotokea nchini,kama vile matokeo ya kidato cha nne kufutwa, suala la Mwigulu na wenzake wa usalama wa Taifa kuwabambikia viongozi wa CDM,makosa ya ugaidi na tukio la kulipuiiwa kwa bomu, kwa kanisa la Arusha,ni dhahiri maswali ya kiongozi wa upinzani bungeni,Mbowe na makamanda wengine wa CDM,ni dhahiri leo bungeni kungrkuwa na shinikizo kubwa la vigogo wa CCM,kuachia ngazi,jambo ambalo Pinda,angeshindwa kulihimili,badala yake angebakia kutoa machozi kama ilivyo kawaida yake!!

Sasa kwa kuwa TBC,siku zote inafanya shughuli zake kwa kulinda maslahi ya CCM na viongozi wake, wameonelea wasitishe matangazo hayo,ili kumuepusha mzee wetu Pinda,kuonekana kwenye luninga akimwaga machozi ya kufa mtu!!!
 
Samahani watazamaji na wasikilizaji wetu tuko kwenye shamrashamra utiliaji saini mkataba wa ushirikiano na Radio Uhuru chini ya mkurugenzi mmoja hapa Rumumba, tutarejea mara tu baada ya shuguli hii.
Ahsante na poleni kwa usumbufu!!
Tiger, acha kupotosha. Tangazo lipo kama nilivyoliweka hapo juu
 
leo session inaanza na maswali ya papo kwa papo, nadhani ni sawa tu kwa uamuzi huo mzuri walioufanya wa kukata matangazo maana sio busara hasa Afrika kumuonyesha mtu mzima akilia adharani. PM akishamaliza hiyo session nadhani watarejesha!
 
Wabunge tumewatuma sisi
mishahara/posho kodi zetu sisi
Tbc inaendeswa kwa kodi zetu sisi
af tbc na bunge sisi ili tuwaone wanatupangia!!
Kwa upande wangu
its still
loading.........
 
Wanaficha uozo wa ccm wakati kila mtanzania anaujua mahakama imewaumbua baada ya kutenda haki!!! sioni maana ya tbc bora wazipe channel nyingene ridhaa ya kurusha live vipindi vya bunge, watu leo tulitaka kuckia kutoka serekalini kuhusu tuhuma za ugaidi dhidi ya chadema lakini ccm wametunyima haki yetu ya kupata habari!!! ccm + tbc ni wakuchingia baharini
 
TBC kwasasa wana mkurugenzi msikivu. Na lazima ajifunza yaliyomtokea Tido Muhando, haiwezekani kabisa Viongozi wanakuambia achana na Midaharo weka Ze commedy wananchi wafurahie wewe unang'ang'ania Midaharo tu.

Nimecheka hadinimesahau nilikuwa naenda wapi!ngoja nitafute daladala nirudi zangu nilikotoka!!! He! Hivi nilitokea wapi?????
 
umeme umekuwa stable kidogo so alternative ni kukata matangazo ya moja kwa moja ila hapo kabla walikuwa wanatake advantage ya uhaba wa umeme
 
Back
Top Bottom