Elections 2010 TBC wamefanya kweli

Ule umati wa Mwanza unafanya hata uchakachuaji wa matokeo kuwa ni shubiri kwa sababu mchakachuaji huyo ataielezea nini jamii ya watanzania kuwa Chadema na Dr. Slaa hawajashinda?

Huyo atakayeongoza kwa kura za wizi uhalali wake utatoka wapi?

Kadamnasi hizi na chereko chereko ni dalili za ushindi mnomno J2 ijayo.............
 
Nimesikia kwenye radio tangazo la mdahalo wa dr slaa. Inatia moyo kuwa watanzania wengi watafuatilia mdahalo huu. Ni fursa kubwa kuwafikia wapiga kura wengi kupima uwezo wa dr, ingawa inaonekana wagombea wenzake hawatashiriki
 
Ukweli TBC wana afadhali sana kulingasha na Channel Ten, Channel Ten wanatia aibu. Wameamua kuwa chombo cha propaganda badala ya kuwa chombo cha habari. Ikianza tu taarifa ya habari ujue maneno ya kwanza yatakuwa "mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi" hayo ndio maneno yao ya kwanza siku zote. Basi atapambwa hapo dak hata 20, ukisikia chadema ujue ni mashitaka hakuna cuf wala chama kingine. Watuambie kama imekuwa m/c ya propaganda ya ccm na wamejitoa kuwa chombo cha habari. TBC pamoja ya kuwa ndiye mwajiri wao, wanajitahidi sana.

Jamani mm sio fisadi lakini naomba niwatetee channel 10 japo katika hili. Kwa siku za karibuni (kama wiki au zaidi) nimekuwa nikiangalia taarifa zao za habari, na ingawa wanaiweka ya mwisho, lakini kila siku lazima watoe habari ya mikutano ya Slaa, na kuonyesha umati unaokuwepo kwa kadiri ya uwezo wao. Nawapa big up kw hilo...
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom