Tbc tbc tbc!

kivyako

JF-Expert Member
Feb 2, 2012
14,341
12,045
Hakuna taarifa yoyote kuhusu taarifa za uharamia aliofanyiwa dr. Ulimboka, hii inamaanisha nini wadau? nafikiri ni majibu tosha kuwa hii serikali dhaifu na ya kidhalimu inahusika moja kwa moja, Mungu mbariki dr. apone.
 
Hili ni jambo la kushangaza sana hv kweli TBC mnashindwa kurusha habari hii badala yake mnaonyesha ngonjera za bungeni?ss wananchi sasa imefika mahala tunasema basi maana mnapotosha uma watu tuwafikirie vipi??

UPDATES
Jamaa wameonyesha hii habari ya Dr Ulimboka!
 
Siyo TBC tu bali hata ITV. Hakuna TV ya Tanzania inayoweza kurusha habari kama hii na ikabaki salama!
 
TBC wajifunze yaliyowakuta kitua cha TV Siria kilichokuwa kikirusha matangazo ya kuipendelea Serikali, kimepigwa mabomu na watu 3 wameuwawa, Tbc ni mali ya Umma si mali Ya ccm na Serikali yake Dhaifu,
Hili ni jambo la kushangaza sana hv kweli TBC mnashindwa kurusha habari hii badala yake mnaonyesha ngonjera za bungeni?ss wananchi sasa imefika mahala tunasema basi maana mnapotosha uma watu tuwafikirie vipi??
 
Star tv imerusha mkuu. Tbc a.k.a tb magamba/mafisadi/maghaidi /majambazi hawawezi kurusha. Waliohojiwa star tv wanasema dr ulimboka alikuwa anawasiliana na mtu kutoka ikulu aitwaye abedi. Unadhani kwenye tbc ambayo imejaa uozo na upotoshaji watatangaza?
 
Tangu aondoke TIDO MUHANDO, hii imekuwa sio television tena ya kuangalia, huyu mkurungezi mpya MSHANA, yaani ni full gamba. mimi huwa siangaliagi hii television. naangalia ITV, STAR TV & CHANEL TEN.
 
Jamani nimeangalia televisheni yetu hii ya serikali, kwani inachukua ruzuku kutoka serikalini, fedha ya kila mwananchi mlipa kodi. Cha kushangaza! Habari iliyovuta watu wengi, umma kwa ujumla ya kutekwa kwa dr. Na kukutwa mahututi katika msitu wa magwe pande. Haikuwa ni issue. Hivi wanahabari na umma kwa ujumla mnalionaje hili? Wangeitoa tuu kwani kwani ingekuwaje..............basi tu.
 
TBC inatumika kupotosha watanzania ili waendelee kuibiwa kwa ufisadi. ndio maana mimi hata taarifa yao siangalii maana hakuna waledi wa habari ila ni ukanjanja tu ndio umetawala
 
na mim nilishaacha siku nyingi kuangalia taarifa ya habari ya TBC,,, join the boat
 
Ni lazima kurasha hiyo habari ya dr.ulimbuka ziko habari za msingi hiyo si kipaumbele... Tunamuombea apone ili aje ahadithie kifo kikojo ,,kwani wao wanaona utamu ndugu zetu kufa kwa migomo yao ya kishenzi tu.
 
habari muhimu ni kumuonyesha pinda akitema pumba bungeni, yana mwisho!?.
 
Back
Top Bottom