TBC taifa au TBC CCM?

JACADUOGO2.

JF-Expert Member
Dec 13, 2010
930
217
Ndugu wana JF napenda kuuliza kuwa TBC1 ni shirika la umma wa watanzania au ni shirika la CCM? Tukiangalia mwenendo wa TBC1 kwa kweli inatukatisha tamaa sisi kama wananchi wa Tanzania tunakuwa na wasiwasi mkubwa dhidi ya TBC1. Kwa mfano ukifuatilia taarifa ya habari ya TBC1 kila siku lazima watoa habari za CCM hata habari zisizokuwa na msingi wowote kwa maendeleo ya taifa letu. Ukifuatilia mambo makubwa na makongamano na hata maandamano ya CHADEMA hayatangazwi wala hayazungumziwi TBC na watu wanaoalikwa kwenye kipindi cha jambo cha asubuhi TBC1 ni wale wale wa CCM kila siku! Je, watanzania tutafika?
 
Ni TBC Taifa kwa sababu wasio wana CCM sio Watanzania na hili sio Taifa lao. Naichukia sana TBC hasa baada ya kuondolewa kwa Tido Mhando
 
CCM imepoteza mvuto kutokana na 'sintofahamu'. Sasa TBC itakuwa next. watu wanapolalamika ni vizuri wahusika wachukue hatua badala ya ku-supress. Kitendo cha ku-black-out habari za wasiopenda either kwa niaba yao binafsi au kwa maelekezo ya wakubwa ni kama kujichimbia kaburi.

Na huyu Clement Mshana kwangu mimi naona kama ndio msumari wa kuziba kabisa jeneza la TBC na wanaowapamba. Pengine wangejifunza toka Dodoma kwamba Mama Makinda na wenzake wamegeuza bunge kama kamati ya CCM matokeo yake wananchi wameamua kunzasha mabunge yao mtaani - maandamano.
 
Tbc ni ya ccm au ya watu waliojivua magamba imepoteza mvuto wasomi wameipa kisogo pamoja na wananchi wengine kwa kweli hakuna anayeangalia sasa hivi watu wanaangalia itv
 
Tido alijitahidi ndo maana wakamtimua. Walobaki wote Mapompompo kuanzia Mkurugenzi wao, mie nawadis kinomaa...wanaboa.
 
Watanzania tutafika lakini siyo kupitia TBC,

Siyo habari tu,hata mpira wa timu zetu tena michezo ya kimataifa?hivi hili ni genge ama ni ni kitu gani,mfano,mechi Simba Vs Mazembe zote mbili,U23 Vs U23 Ug zote mbili,T.s Vs Moz,T.s Vs S.A,hizi mechi zote watanzania hawazioni tena kwa maana Tbc imekodiwa na wanaojikoboa magamba,wanatuwekea mambo ya kifara mda wote,taarabu,nyimbo,masharobaro na uchafu mwingne,ndugu zangu tufanyeje hapa?
 
Msuya alikuwa mmoja wa waalikwa katika semina elekezi pale dom na hotuba ya president wakati anafunga semina amesema wazi wajumbe wote wajipange kwa next election na Mshana ni mjumbe, hapo unategemea nini?
Kampeni imeanza
 
Back
Top Bottom