Tbc na miwani ya kisogoni.

Bendera ya Bati

JF-Expert Member
Apr 6, 2011
279
363
Kwa sisi tunaovaa miwani,mala nyingi inatusaidia kuona zaidi ya kuona kwa kawaida kutokana na aidha macho yamepungunza nguvu ya kuona mbali au karibu katika hali ya ufasaha.Sasa nikirudi katika dhamila ya kile kilichonisukuma kaundika thread hii ni kile ninachakiona kwa tv yetu ya umma kama wanavyojiita ikiwa na mwonekano wa upofu ambayo pamoja na kuvaa miwani ili waone kwa ufasaha wao miwani yao wameikita kisogoni.

Nalazimika kusema hivyo kutokana na shirika hili la utangazaji kujiondoa kabisaaa katika kuonesha matukio mbalimbali ya kijamii kwa umma zaidi ya kutuletea show za chama fulani au makada wake au viongozi wa serikali ili kukishafisha dhidhi ya tuhuma nzito zinazokikabiri chama hiki,na hata baada ya kujishtukia kuwa hakina mvuto tena kwa raia,Vikao vya chama ambavyo kwa maslahi ya umma sioni kama ni kitu cha kupewa coverage kubwa zaidi ya vyama vingine katika chombo kinachomilikiwa na umma......Ooh, kujivua magamba hii ina tija gani kwetu sisi watz wenye mitizamo tofauti ya kisiasa?

Chombo kama Tbc kwanza kilitakiwa wakati huu wa miaka 50 ya uhuru wa nchi hii kiwe kinatoa matangazo yake nchi nzima tena bila chenga si kwa tv wala redio.Nenda mikoani tena tusiende mbali saana kama kwetu kule kanda ya ziwa ebu twende Moshi tu mwendo wa masaa manane kutoka hapa Dar,utashangaa hata redio tbc Taifa haipatikani mpaka uangaike kwelikweli mala redio uibembeleze kama mtoto,uipake losion lakini bado utaendelea kuipata kama vile unaisikilizia ndani ya bahari (umezama).Hapo kuhusu tbc1 sahau kabisa,sasa huwa najiuliza katika kijiji hiki cha dunia moja na sayansi na teknolojia,Hivi sisi ni watu wa kukamata mkia kwa kila kitu.Naomba mnisaidie pale KENYA redio na tv yao ya taifa inaoneshwa na kusikilizwa Nairobi na mikoa ya jirani tu?Na hata kama kwa kenya kuko hivyo sisi tunawazidi sana kwa utajiri,ina maana hatuko serious kwani hatuwezi kujipima na kenya interms of rasilimali,inatakiwa pia miundombinu tuwe zaidi ya wao.

Nikitolea mfano wa shirika la utangazaji la Uganda ,nchi nzima wana access habari kupitia chombo chao cha umma maeneo yote ya Massaka,Kiotera,Mbarara Jinja,mpaka Kampala ambako ndiko yalipo makao makuu ya UBC wanafaidika na matangazo ya tv yao,ispokuwa sina hakika hasa katika pande za Guru HUKO kaskazini mwa UG Kama wanaipata make kulikuwepo na vita kwa muda kati ya waasi na majeshi ya serikali.Ikitokea kuna tukio la kitaifa lazima litaonyeshwa bila kujali category ya tukio hilo hususani MPIRA pale nchi yao inapokuwa inacheza mechi za kimataifa katika ngazi yoyote aidha ya virabu au vingineyo.Vivyo hivyo kwa Kenya.

Kwa nchi yetu kinachoshangaza na kusikitisha,ni mala chache sana kukuta wanaonesha matukio kama hayo mfano,LEO TIMU YA VIJANA U23 Ilikuwa inachuana na vijana wa umri kama huo wa Uganda lakini Tv yetu ya taifa iko busy na mambo mengine kabiasa.Yaani haina habari......miwani imevalia kisogoni,haioni mbele ni wapi.......inaona maruweruwe..........hii ndiyo TBC bwana...KAAAAAAZI KWELIKWELI.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom