TBC mnatia aibu, acheni kujiita TV ya taifa

Mpanzi

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
785
440
Leo katika taarifa ya habari ya tbc wametangaza tukio la jaribio la ulipuaji ndege ambapo undercover agent mmoja wa saudi arabia alikwenda yemen na kujiunga na kikundi cha alqaeda, walichotangaza tbc ni tofauti kabisa wakidai mnijeria aliyekamatwa mwaka 2009 kuwa alikuwa double agent wa cia, huo ni uwongo uwongo, uwongo, uwezo wa waandaaji wa news ni mdogo sana, sijui tatizo ni lugha au uvivu?
 
mi nshachoka taarfa yahabari kumradhi nyingi kuliko habari zenyewe
 
Habari za Tanzania nyingi hazina ishu za maana zenye kuwa gusa wananchi moja kwa moja ila kuwatukuza viongozi na kurepoti habari za mataifa mengine japo kuwa hakuna uhitaji wa namna hiyo. Ukitazama taarifa ya habari ya vyombo vingine vya nje kwa mfano CITIZEN TV utagundua kuwa habari zinahusu Kenya na hata kama kuna habari ya kimataifa ila ni lazima iwe kwa njia moja au nyingine ina kitu flani kinahusu Kenya. (Hawa jamaa unaweza angalia TV yako asubuhi mpaka jioni na usichoke....vionjo kwa sana)

Ifike wakati vyombo vya Tanzania vijifunze kutoa kipaumbele kwa habari zenye manufaa badala ya kuhangaika kupoteza fedha nyingi kwa kuandaa habari na vipindi vywenye ubora duni.

Hivi viongozi wao wakienda semina/wekishopu huwa wanajifunza nini huko nchi zilizoendelea?
 
TBC wanaibudu serikali ya ccm chini JK Maana wakienda kinyume watu si hawana kazi hapo?mambo ya kutangaza ishu zinazowahusu wananchi hakuna hapo kabisa. Mimi hata siangaliagi hili tbc.
 
naangalia usiku wa habari. Ni maudhi matupu. Walitaka kumuonyesha Mama Tibaijuka na tamko lake la ujenzi wa fukweni. Sauti imegoma. Wakaomba radhi na kujaribu kuweka tangazo la biashara likagoma, wkataka warudie taarifa ya waziri sauti ikagoma. Nimemuonea huruma dada mtangazaji maana ameonakana kukereka mwenyewe hadi akakatisha kipindi na kuweka mziki wa sharobaro. Inabidi tuanzishe kampeni ya kuisema sana hii tv ndani ya hii forum kwa kuyakemea mapungufu yake. Nina hakika kuna siku hawa wenye nchi wataamka usingizini. Ni aibu aibu sawa na ATCL.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom