TBC mna bifu gani na CHADEMA?

Habari wana JF! Nimechukua fursa hii kutoa mawazo yangu juu ya mchezo mchafu unaofanywa na TBC1 ambayo inajiendesha kupitia kodi zetu, si jambo la ajabu kwa tbc1 kuipendelea CCM na upande wa pili ikiukandamiza upinzani kupitia habari zake, mfano tulishuhudia upotoshaji uliotangazwa na tbc1 kuhusu sakata la CDM na mkuu wa wilaya pale Igunga.

Pia tumeshuhudia tbc1 ikificha kutangaza hata habari muhimu za CDM na upinzani kwa ujumla, pia tumeshuhudia tbc1 ikitumia muda mwingi ktk kutangaza habari zinazohusu chama tawala mfano ktk miaka 35 ya ccm pale mwanza, pia tumeshuhudia TBC1 ikipotosha umma mara nyingi kuhusu sakata la mgomo wa madaktari kwa lengo la kuikingia kifua serkali etc...........

Sasa ni wito kwa viongozi makini wa CDM hasa waziri kivuli wa habari na utamaduni kulishikia bango swala hili ili sisi wananchi tupate tbc1 ambayo haina ubaguzi kwa maslahi ya taifa letu na si kwa maslahi ya magamba pekee.
 
achana nayo hiyo tbc1,kazi kubwa umbeya tu.lini utakuta cnn au bbc wanaonyesha kitchen party?

Hawana kingine cha kuripoti, kazi yao ndo hiyo ya kitchen party, then waone waandishi wa tBC kuwa na function uone wanavyolilia posho
 
Kwa kweli umeraise issue muhimu na ya kweli naomba wana JF wenzangu tuijadili kwa kina, Ukiangalia TBC utadhani matangazo yake yanarushwa kutoka pale Lumumba ofisi ya CCM, Nape Nawie anapewa nafasi kubwa kweli. na habari anazozitoa ni za Chama cha magamba.

Upinzani hata kama una hoja nzuri kiasi gani nakwambia huwezi kusikia mambo yao yakitangazwa kupitia TBC, yes kwa vyombo binafsi hatujali sana kwa vile ni discrition yao kutangaza ama kuacha.

kama alivyoongea Tido Muhando kwenye mjadala wa JUlilee ya BBC vyombo vingi vya habari (kama si vyote) ni vya marafiki wa CCM kwa hiyo wangependa kutangaza habari zisizowaudhi magamba hata kama zina umuhimu na maslahi kwa taifa.

TBC rudisheni chombo hicho kwa wananchi, ni chetu chote na kwa matumizi yetu wote. tunadhani wabunge wa CDM mnapaswa kulipigia kelele hili hata kama labda nyinyi mnadhani si lazima sana. sis wananchi na hasa wanachama wenu tunajisikia vibaya sana kwa kuwa kuwasikia viongozi wetu ni nadra sana.
:lol:
 
Nawasikitikia ambao bado wanatazama TBC, Mie nimeshaacha mda mrefu kuangalia Taarifa zao. Angalau Star tv, Itv na Channel ten kidogo. TBC ni Magamba.com.
 
Nawasikitikia ambao bado wanatazama TBC, Mie nimeshaacha mda mrefu kuangalia Taarifa zao. Angalau Star tv, Itv na Channel ten kidogo. TBC ni Magamba.com.

gud but kulikimbia tatizo si kutatua tatizo bali ni kuliongeza tatizo, so cha msingi kwa sisi wanamageuzi ni kufanya harakati kwa kulipigia kelele swala hili kuanzia humu mtandaoni na ku-inspire wanamageuzi wote na viongoz wa CDM ktk kulitafutia soln swala hili so as tuweze kuipata TBC tunayoitaka ambayo haina chembe za kibaguzi kutokana na political interest za magamba. Jamani wanamageuzi na CDM lioneni hili swala kwani linarudisha nyuma harakati za mageuzi kuliko hata jinsi mnavyodhani.
 
Ni kweli TBC ina upendelo wa wazi wa coverage ya habari kwa kuwapendelea Magamba, lakini boss wao Mshana anapaswa kufahamu kuwa chombo hicho kinarndeshwa kwa kodi zawa-TZ bila kujali itikadi zao, tunajua kitu kilichomfukuzisha kazi Tido Mhando, ni kutimiza wajibu wake wa mwanahabari wa kuzibalance habari bila kuwapendelea CCM, jambo lililowakera wafadhihina wa magamba hadi wakashinikiza akafukuzwa kazi!
 
kamera za Station ya Taifa ya hovyo kabisa ,kabisa hata wakati wa mwalimu akina Ben Kiko walikuwa na uwezo wa kutetea maslahi ya nchi si hawa wa leo makanjanja
TBC Makanjanja, wataleta njaa na janga. Tusiwapuuze! Mauaji ya Rwanda 1993 yalianza hivihivi! Hatua za kisheria zichukuliwe. Tunaomba kuwapa jukumu hili WIZARA KIVULI!
 
Katika kutangaza uzinduzi wa Kampeni za CHADEMA mtangazaji wa TBC (Amina Moleli) anamalizia taarifa yake kwa kusema "uzinduzi huo ulihudhuriwa na mamia ya wakazi wa jiji Arusha" Hii maana yake nini. Ina maana si wakazi wa Arumeru waliohudhuria uzinduzi wa Kampeni za CHADEMA bali ni wakazi wa jiji la Arusha??
TBC mna bifu gani na CHADEMA?
 
usimlaumu licha ya kwamba yeye ni mmasai lakini inawezekana haijui arusha vizuri anadhani arumeru iko arusha.
 
Msimlaumu amina,taarifa ile imerushwa kwa basi 2 kwani kitaaluma hawajarusha penye hot newz,basi 2 wamerusha ili isionekane hawajarusha kabisa.shme on them
 
Seriously wanaboa,.yan wamekaa ki-green kwel! Politix everywhere
 
ni mchanganyiko wa mrangi na mmasai na anatoka huko huko meru east,kama amesema hivyo basi amekusudia
Najua kwamba script hakuandika yeye, lakini kwanini yeye hakutumia "umbayuwayu" angalau kusema ukweli kidogo kuhusu tofauti kati ya Arusha na Arumeru. Na pia badala ya kusema "mamia" angesema "maelfu" maana mamia yanaishia kwenye 999.
 
TBC ishakuwa ya magamba so ni wakati wa sisi wanamageuzi kuidai tv yetu inayoendeshwa kwa kodi ze2 alafu ikiwanufaiisha wachache. TBC P.U.M.B.A.F.U sanaaaaaaaaaaa
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom