Elections 2010 TBC Live TARIME leo

Kama vile mlogwa vile!!! yaani...

Kasheshe, aliyerogwa hapa ni yule anayeng'ang'ania kile kile. Hata kama mambo yanabadilika na anaona na kutambua yanabadilika lakini yeye bado anang'ang'ania kilekile, bila kujali athari zake kwake na kwa wenzake. Almradi tu amedhihirisha mapenzi yake kwa hicho kitu na kuonekana machoni pa watu amefanya hivyo.
 
Naona kipindi kimeisha but thats my contirbution kwa leo kwa wale ambao hawajaweza kuona kipindi hiki live leo. nadhani wapo walioweza kurekodi huenda wakatuwekea zome clips hapa kuweza kupata ile feeling hasa ilikuwaje

CCM kutoweka wagombea wao wanafanya kosa kubwakwa maoni yangu maana hapa ndio ingekuwa nafasi nzuri ya kuzidiana kisera,

Ila pia sijapenda uulizaji huu wa maswali wa TBC nadhani ile issue ya ubungo bado inawatafuna tafuna nod wamebadili strategy... maswali ingebidi yawe specific kwa kila mgombea bana..
Mkuu TBC hawajakosea kitu kwa sababu kero za wananchi zinavihusu vyama vyote hivyo ni muhimu kila mgombea ajielezee kuhusiana na kero hiyo na ndio maana umeona wagombea wote wamezungumzia zaidi sera za chama badala ya wao wenyewe kuelezea wanachokiona bora zaidi kufanyika kuondoa kero hizo.. Kwa hiyo kinachokuwepo ni Ahadi tupu.

Labda tuseme makosa yao yanakuja pale waliposhindwa kugawa maswali ktk safu mbili. Ya kwanza ni mahitaji ya wananchi ambayo wagombea wote wanawajibika kujibu swali moja (Sera na Ilani za chama), kisha nyingine ni maswali ambayo yanayowahusu wagombea in question.. hapo kila swali lingemlenga mgombea kulingana na CV, record yake na ahadi zake (ilani za Mgombea)..

Mara nyingi utaratibu mzuri wa midahalo huwa na watu maalum waliochaguliwa kuuliza maswali yaliyokwisha tayarishwa bila chama chochote wala mgombea kujua wataulizwa nini, ukisha mzunguko huo wa maswali inakuja maswali ya wananchi ambapo muulizaji anaweza kuelekeza swali lake kwa mgombea mmoja au kwa wagombea wote..

Hata hivyo, huu ndio mwanzo tunajifunza tutafika tu kuwa makini na wenye kuelewa kwa nini midahalo ni muhimu na maswali ya aina gani huulizwa.
 
Mara nyingi utaratibu mzuri wa midahalo huwa na watu maalum waliochaguliwa kuuliza maswali yaliyokwsiha tayarishwa bila chama chochote kujua wataulizwa nini, ikisha mzunguko huo inakuja maswali ya wananchi ambapo muulizaji anaweza kuelekeza swali lake kwa mgombea mmoja au kwa wagombea wote..

Hata hivyo, huu ndio mwanzo tunajifunza tutafika tu kuwa makini na wenye kuelewa kwa nini midahalo ni muhimu na maswali ya aina gani huulizwa.

Ndio I support your idea na nimeona inatumika baadhi ya nchi
 
Kama vile mlogwa vile!!! yaani...

Mkuu, wanikumbusha yule Wariri wa Habari wa Iraq ambaye tarehe 7 Aprili, 2003 aliutangazia Ulimwengu kuwa hakuna mwanajeshi wa Marekani aliyeingia Bagdad na kwamba waliojaribu waliteketezwa kwenye lango la jiji. Muhammad Saeed al-Sahhaf alikataa kata kata kuamini kuwa hatari ilikuwa inawanyemelea pamoja na milio ya mabomu kusikika hatua chache kutoka aliposimama. Naam Kasheshe habari ndiyo hiyo, endelea kuwadanganya wakereketwa wa CCM kuwa majeshi ya Chadema bado yako mbali !
 
Huyu jamaa Mwita namkumbu kipindi akiwa pale udsm, 2005 katika siasa za udsm alikuwa akimuunga mkono Sumaye, kutokana na Sumaye kuchezea mchezo mchafu ndio namuona yupo CHADEMA, baada ya hapo alikuwa amefulia kweli
 
Inawezekana kunaweza kuwa na connection kati ya ushiriki wake kwenye Kambi ya Sumaye vs Mtandao. Zama za Nchimbi akiwa Mwenyekiti wa UVCCM, Mwita alikuwa Katibu wa UVCCM mkoa wa Tanga. Baada ya JK kuingia madarakani, Nchimbi alimwandikia Mwita Waitara barua ya kumhamisha kutoka kutoka Tanga kwenda Makao Makuu. Hapo ndipo lilipotokea zogo, jamaa alisema yeye hawezi kwenda kuwa mpika chai pale Makao Makuu na yeye [Mwita] aliona hicho kitendo ilikuwa ni kama demotion, kutoka Katibu wa UVCCM mkoa mpaka kuwa nobody pale Makao Makuu. Kwenye barua aliambiwa kwamba angepangia kazi nyingine Makao Makuu ya UVCCM.

Probably alisha-sense kwamba sasa mtandao wanaanza kumshughulikia na ndio maana aliamua kutimkia CHADEMA baada ya hilo zogo la kuhamishwa kutoka Tanga kwenda Makao Makuu ya UVCCM. I guess atawapelekesha puta kwenye hilo jimbo maana hata kwenye uchaguzi mdogo baada ya Chacha Wangwe (RIP) kufariki, alishiriki kwa kiasi kikubwa kutetea hilo jimbo lisiende CCM.
 
Kichekesho ni Mwera alikuwa amevaa kombati za Chadema! Halafu alikuwa akikosea kosea badala ya kusema CUF anasema Chadema!
 
Nimeangalia kipindi jana ucku.

CHADEMA watachukua jimbo kwa mahesabu ya haraka na namna mgombea wao alivyokuwa akijibu hoja na mikakati ya chama chake kwa Wanatarime. CHADEMA wako juu kila mahali.

CCM wamekimbia midahalo kwa kuogopa kuhojiwa kuhusu maovu wanayoyafanya ndani ya jamii ya Watanzania. CCM safari hii lazima muibe kura sana vinginevyo CHADEMA watachukua nchi. Watanzania tumechoswa na longo longo zenu za kila kukicha.

Wasalaamu.
 
Midahalo hii inawatafuna sana CCM kwa kuisusia kwao. Kwa kuwa TBC ni ya serikali "yao" nasikia kila jitihada zinafanyika TBC1 waifunge. Yule jamaa aliyekuwa mbunge wa Tarime ni MTUPU kwelikweli hata sijui CHADEMA walimteuaje kugombea wakati ule.
 
hawa viongozi wa ccm hawana issue za msingi kabisa, huwezi kuwakataza wagombea wasishiriki kwenye midahalo huo ni ujuha mkubwa sana kwenye zama hizi za sayansi na teknolojia hasa hasa ukizingatia kuwa midahalo hiyo inarushwa kwenye runinga na redio na hizo ndio njia nzuri za kutangaza sera kwa wananchi ambao wengi wao sio wahudhuriaji wa mikutano ya kampeni.
sasa ccm wao hawataki maswali kwa kuwa hawna hoja za msingi na hawana majibu ya msingi ya maswali mengi ambayo wananchi wanaweza kuwauliza.
 
Mkuu TBC hawajakosea kitu kwa sababu kero za wananchi zinavihusu vyama vyote hivyo ni muhimu kila mgombea ajielezee kuhusiana na kero hiyo na ndio maana umeona wagombea wote wamezungumzia zaidi sera za chama badala ya wao wenyewe kuelezea wanachokiona bora zaidi kufanyika kuondoa kero hizo.. Kwa hiyo kinachokuwepo ni Ahadi tupu.

Labda tuseme makosa yao yanakuja pale waliposhindwa kugawa maswali ktk safu mbili. Ya kwanza ni mahitaji ya wananchi ambayo wagombea wote wanawajibika kujibu swali moja (Sera na Ilani za chama), kisha nyingine ni maswali ambayo yanayowahusu wagombea in question.. hapo kila swali lingemlenga mgombea kulingana na CV, record yake na ahadi zake (ilani za Mgombea)..

Mara nyingi utaratibu mzuri wa midahalo huwa na watu maalum waliochaguliwa kuuliza maswali yaliyokwisha tayarishwa bila chama chochote wala mgombea kujua wataulizwa nini, ukisha mzunguko huo wa maswali inakuja maswali ya wananchi ambapo muulizaji anaweza kuelekeza swali lake kwa mgombea mmoja au kwa wagombea wote..

Hata hivyo, huu ndio mwanzo tunajifunza tutafika tu kuwa makini na wenye kuelewa kwa nini midahalo ni muhimu na maswali ya aina gani huulizwa.

sawa kabisa mkuu Mkandara...hapo kwenye bold ndio exactly my point,, sasa wao jana wameng'ang'ania kwamba kila swali lijibiwe na kila mgombea...maswali specific hayakuruhusiwa lakini wana TARIME bado walikuwa wajanja kuyatwist ili ujumbe ufike....
 
Midahalo hii inawatafuna sana CCM kwa kuisusia kwao. Kwa kuwa TBC ni ya serikali "yao" nasikia kila jitihada zinafanyika TBC1 waifunge. Yule jamaa aliyekuwa mbunge wa Tarime ni MTUPU kwelikweli hata sijui CHADEMA walimteuaje kugombea wakati ule.

mkulu hilo likifanyika itabidi tuaccept hypothesis kwamba TBC ipo pale kwa maslahi ya CCM na sio maslahi ya umma....
 
Midahalo hii inawatafuna sana CCM kwa kuisusia kwao. Kwa kuwa TBC ni ya serikali "yao" nasikia kila jitihada zinafanyika TBC1 waifunge. Yule jamaa aliyekuwa mbunge wa Tarime ni MTUPU kwelikweli hata sijui CHADEMA walimteuaje kugombea wakati ule.
Kwa taarifa yako midahalo hii imeshalipiwa na UNDP ili ifanyike na si utashi wa TBC. Bila hivy itabidi waziteme pesa zote mamilioni kwa mamilioni ya dola waliyopewa TBC. Hivyo hawana utashi lazima waonyeshe vipindi hivyo ku justify malipo waliyopewa na ni lazima warushe na hata kidogo vionjo vya mikutano inayoendelea nchi nzima.
 
Back
Top Bottom