Elections 2010 TBC Live TARIME leo

Kaizer

Platinum Member
Sep 16, 2008
25,320
17,822
Wadau, sasa hivi kuna kipindi kinaendelea cha mdahalo wa wagombea tarime huko

Mgombea wa Chadema anaonekana kushangiliwa sana na wahudhuriaji (Mwita Mwikabe)

Aliyemtangulia (Mwera) amemung'unya tu maneno of course na wa NCCR na UDP


Kama kawaida CCM hawapo ila kwa Tarime, hakuna CCM ninavoona,

wahudhuriaji wengi wamevaa nguo za Chadema
 
Anasema hahitaji kuwa na kanda maalum ya kipolisi Tarime (kukomesha vita)

Elimu bure hadi form six

Anasema mgodi umenywesha watu maji ya sumu, wamenyang'anya watu ardhi bila fidia

Ataanzisha academic competition kwa vile ni mwalimu

Kila kata kuwa na timu ya mpira, wanawake na wanaume,

Atatembelea wagonjwa hospitalini na magerezani kuona kama wanahudumiwa,

Polisi walioletwa wamevunja katiba (ibara ya 13) na ya 14.......kutendewa kwa mujibu wa sheria, na kuishi sehemu anayopenda,
 
maswali sasa:
Charles mwera anaulizwa, je, atasimamiaje maendeleo iwapo atakuwa na madiwani achache wakati CUF wamesimamisha 5 tu (mtangazaji anasema sio valid lol)
anauliza tena....haki za binadamu na uonevu, atasaidja wakati mwaka mmoja na nusu akiwa bungeni alishindwa kusimami (mtangazaji anapotezea tena anadai eti wanatakiwa wajibu wote....duh!)
 
sasa huyu mgombea wa NCCR sijui atajibuje manake naona anabwabwaja tu hana majiu ya maana.....
 
Dag hivi hawa TBC waliambiwa wabadilishe namna ya uulizaji maswali? manake kama swali linaulizwa kisha wajibu kila mmoja sasa sioni maana ya huu mdahalo wakuu....au ninamiss something hapa...
 
mgombea wa Chadema anasema kuwa wana kurugenzi ya siasa na haki za binadamu...na ofisi ya mbunge itakuwa na mwanasheria, na wanaharakati wa haki za binadamu waliletwa Nyamongo kuangalia hali halisi...


Mgombea wa CUF sasa anasema alivyokuwa mbunge alisimamia SANA mambo ya haki za binadamu migodi, ardhi, mbuga za wanyama,,,
 
wanalalamika wananchi kwamba uulizaji wa maswali sio mzuri.....

swali limekuwa twisted kwa walioahidi elimu ya bure wakati haipo kwenye ilani ya chama chao.....chama chenye ilani ya elimu ya bure ni chadema tu, watasimamiaje wakati hawana hata madiwani (mtangazaji Shaaban Kisu kalichakachua tayari)
 
Makamba katuharibia chama. Yaani hapa angekuwepo Nyang'wine, pangechimbika kati yake na Waitara wa Chadema. Na hii midahalo ina effect kwenye campign hizi, sijui nani katuroga jamani!
 
Makamba katuharibia chama. Yaani hapa angekuwepo Nyang'wine, pangechimbika kati yake na Waitara wa Chadema. Na hii midahalo ina effect kwenye campign hizi, sijui nani katuroga jamani!

Hapa aliharibu sana tu, kwa nini hawa waamini wagombea wao?
 
Hapa aliharibu sana tu, kwa nini hawa waamini wagombea wao?
========

Wagombea wanajiamini lakini viongozi wanaogopa na hawatoi uhuru kwa wagombea wanaopenda kwenda kudahala waende. Leo hapo Lumumba nusura ngumi zipigwe kwenye simu.
 
Haya swali la sekta ya Afya sasa....mambo ya vitanda na magonjwa ya mlipuko....

Huyu wa CUF anasema kuwa watasimamia.watahakikisha na mambo ya kupata hati safi

Wa NCCR mageuzi...(ha halafu jamaa ana kifimbo kama cha mwalimu) anasema watazindua zahanati mpya na kupanua hospitali

Wa Chadema....anazungumzia yaliyo kwenye ilani..anazungumzia mattaizo ya hosp ya wilaya (dawa hakuna, manesi) madiwani wamepewa ultimatum ya kwamba waonyeshe zahanati kila kijiji kama wangependa kuendela baada ya miaka 5,

Wa UDP anasema magonjwa mlipuko ni aibu wakati jimbo ni tajiri...wakati kuna mirahaba...anadai majiya tarime ni machafu, mji hauna miundo mbinu...akichaguliwa kuwa mbunge atatumia fedha za mrahaba kwa maji safi, (LOL anadai UTI inasababishwa na Amoeba) atajenga hospitali mpya
 
========

Wagombea wanajiamini lakini viongozi wanaogopa na hawatoi uhuru kwa wagombea wanaopenda kwenda kudahala waende. Leo hapo Lumumba nusura ngumi zipigwe kwenye simu.


ilikuwaje mpanga nusura ngumi zipigwe ,tujuze tafadhali
 
Swali kwamba bodi ya mikopo kwa wanafunzi, (kwamba mbunge aliyekuwepo hakuweza kwuasaidia wanafunzi kwa kudai hajui hata ofisi zilipo za bodi pamoja na wizara)

UDP anasema ni tatizo la kitaifa...kwamba atazungumza na serikali...badala ya kupata mikopo, wanaosaidia tarime (wachimba amdini) wawasaidie moja kwa moja ili wawasaidie wana Tarime...anazungumzia kuanzisha chuo kikuu tarime kwa vile UDSM ilianza Lumumba na wanafunzi 23:becky:

NCCR anadai kubadilisha sheria....kusiwe na vigezo akishachaguliwa kuingia chuo kikuu....kama mwanasheria atapeleka hoja sheria ibadilishwe

CHADEMA...ananukuu ilani uk 16, kwamba wakati bodi inaanzishwa aliipinga bodi ya mikopo akiwa rais wa wanafunzi wa UDSM..kwa vile inabaguwa wa div one na two pekee, na kwamba wanawakopesha kwa kutumia ile mean test...Chadema watavunja bodi ya mikopo na kusomesha kukopesha kwa 100,
 
Back
Top Bottom