TBC hawana aibu!

Kituo cha TV cha kutazama ni Mlimani TV tu kwa sasa, kutazama TBC ni kama tusikiliza radio uhuru!
 
Nawewe umeshindwa tambua kuwa TBC ni idara ya habari ya CCM, sasa unataka waende kinyume na sera na muongozo wa chama? unataka mshana aachishwe kazi alafu, wewe hujui yaliyo mpata Mhando alipotaka kuifanya TBC kuwa isiyofungamana na upande wowote?
 
TBC ni CCM B, ukipata muda muda msikilize God Monyo wa ITV anavyoripoti pale Dodoma mjengoni. Anakupigia majumlisho kwamba wote waliochangia hawajikiti kwenye mswada bali CDM na Tundu Lisu. Lakini TBC wanazipamba zile ngonjera, mipasho, taarabu, makirikiri wa wabunge wa CCM na CUF. Eti mtu anadiriki kusema anawafundisha watanzania nini kipo kwenye mswada. Hii ni dharau kubwa kuwafanya WaTZ ni wajinga. Hawa jamaa wanajidai wakishaingia mjengoni basi tayari wameshapata akili kumbe ukilaza uko palepale. Achana na TBC ili usipate kichefuchefu. Wadhani kwa nini walimtimua Tido si alikataa kuipendelea CCM na kpindi chake cha MCHAKATO MAJIMBONI. Wale vijana pale TBC nawaonea huruma maana wanatangaza vitu ambavyo hawaamini. Yule Elisha Elia na kipindi chake cha Jambo ni aibu tupu anawaita pale akina Sendeka, Mod Rashid, na blabla zao. Namhurumia sana unakuwa msomi halafu vilaza wanakuelekeza cha kusema. Poleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Wana JF roho inaniuma sana kwa yanayotendeka nchini, nimeacha kuangalia taarifa za habari wala vipindi vinavyoongelea mabo ya siasa. Nitakuwa napata taarifa toka kwenu wadau.
 
Mlimani tv!!!!!!!!,sisi wanaudsm wenyewe hata hatuipendi.Huwezi kukuta mwanachuo anaangalia hyo channel.Tbccm imeisha kwanza inatuaibisha hata kuwa kwenye dstv coz haijakizi viwango,toka tido aondoke nayo ndo ubora unashuka.
Nafikiri nyie wanachuo mngekazana na kusoma muanchane na ushabiki.
 
Mkuu mwezi uliopita nilitangaza humu rasmi kuacha kutaza TBC1, wanajamii walinishangaa kwa jinsi nilivyokuwa nimechelewa kufanya hivyo, mimi leo naona wewe ndio umechelewa zaidi.
Kimsingi kituo hiki kimeishapoteza uhalali wa kuitwa televisheni ya taifa.
Kwa nini unahangaika kupoteza muda wako huko, tulia humu kila kitu kinapatikana humu JF.
 
Kule Dodoma Kuna M-ripota wa TBC anaitwa Victoria Patrick, (Television winner of the Excellency in Journalism Awards (EJAT) 2010).


SIna hakika uwezo wake kitaaluma katika kulipoti matukio yanayohitaji taaluma kama siasa, sheria, na uchumi!!!.

[h=2]kikosi kazi cha TBC1 kikiwa kazini kurusha matangazo ya toka bungeni dodoma[/h]
by Dar es salaam , Tanzania on Monday, 22 August 2011 at 22:51



Banda la wanahabari wa TBC1 bungeni Dodoma


<
Wanahabari wa TBC1 wakiwa kazini kwenye kibanda chao nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma ambako wanarusha matangazo moja kwa moja ya kikao cha Bunge kila siku toka saa 12 asubuhi. Toka kushoto ni msimamizi wa matangazo hayo Bi Jane Mosha, Mhariri Selemani Mzee na watangazaji Elisha Elia na Bi Victoria Patrick
Mpiga picha wa TBC1 Humphrey Mwesigwa akiwa kazini ndani ya ukumbi wa Bunge
 
Back
Top Bottom