TBC hawana aibu!

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
925
Ndugu zangu,Nimeangalia TBC1 usiku huu. Nilikuwa na kiu ya kufuatilia kilichoendelea bungeni leo kwenye suala la Katiba. Maana, kuna wengi miongoni mwetu, kutokana na majukumu mengine, tunashindwa kufuatilia ' live' kinachoendelea bungeni.Na hakika, TBC1 bado ni chombo cha habari cha umma kinachoheshimika. Naandika kuwaatadharisha TBC1, kuwa heshima yao inaweza kushuka kama hawataonyesha umakini kwenye mambo ya msingi ya kitaifa. Ona leo, kuhusu mjadala wa Muswaada wa Katiba, wabunge waliounga mkono hoja walipata coverage kubwa, mfano, tuliwasikia kwa sauti zao Ole Sendeka wa CCM na Hamad Rashid wa CUF.Ilipofika zamu ya Mbunge Machali wa NCCR Mageuzi, basi, mtangazaji wa TBC1 ndiye aliyetwambia kwa ufupi sana alichosema mbunge huyo. Umma haukupewa nafasi ya kumsikia Mbunge Machali kwa sauti yake mwenyewe!Tuwe wakweli kwa nchi yetu, kuwa ni mambo kama hayo ndiyo yenye kuchangia kupungua kwa imani ya umma kwa mchakato mzima wa kuratibu Katiba. Hapa kuna mawili, ama TBC1 wanashindwa kufanya kazi yao vema ya kuhabarisha umma au wanafanya kazi kwa maelekezo rasmi.Ona, iweje habari ya ' abrakadabra' ya misukule ya Iringa ipate nafasi kubwa kuliko sauti ya Mbunge wa NCCR Mageuzi anayetoa maoni yake kuhusu Muswaada wa marekebisho ya Katiba? Jambo muhimu kabisa kwa nchi yetu kwa wakati huu. Tujisahihishe ili tusonge mbele kama taifa moja.Maggid,
Iringa,mjengwablogspot.com: The Best Search Links on the Net
 
Mkuu,,heshima ya tbc ilishashuka kitambo tu! kuhusu maelekezo ndiyo haswaaaaa hali ilivo,wanafanya kazi kwa maelekezo ya kunufaisha/kukibeba ccm na c kwa utashi wa habari. Achana nao wale mkuu
 
angalia saa sita usiku startv wanarudi mambo yote bila chenga.mimi siku hizi siangalii tbc kwa sababu wananiharibia siku.mia
 
Ndugu zangu,Nimeangalia TBC1 usiku huu. Nilikuwa na kiu ya kufuatilia kilichoendelea bungeni leo kwenye suala la Katiba. Maana, kuna wengi miongoni mwetu, kutokana na majukumu mengine, tunashindwa kufuatilia ' live' kinachoendelea bungeni.Na hakika, TBC1 bado ni chombo cha habari cha umma kinachoheshimika. Naandika kuwaatadharisha TBC1, kuwa heshima yao inaweza kushuka kama hawataonyesha umakini kwenye mambo ya msingi ya kitaifa. Ona leo, kuhusu mjadala wa Muswaada wa Katiba, wabunge waliounga mkono hoja walipata coverage kubwa, mfano, tuliwasikia kwa sauti zao Ole Sendeka wa CCM na Hamad Rashid wa CUF.Ilipofika zamu ya Mbunge Machali wa NCCR Mageuzi, basi, mtangazaji wa TBC1 ndiye aliyetwambia kwa ufupi sana alichosema mbunge huyo. Umma haukupewa nafasi ya kumsikia Mbunge Machali kwa sauti yake mwenyewe!Tuwe wakweli kwa nchi yetu, kuwa ni mambo kama hayo ndiyo yenye kuchangia kupungua kwa imani ya umma kwa mchakato mzima wa kuratibu Katiba. Hapa kuna mawili, ama TBC1 wanashindwa kufanya kazi yao vema ya kuhabarisha umma au wanafanya kazi kwa maelekezo rasmi.Ona, iweje habari ya ' abrakadabra' ya misukule ya Iringa ipate nafasi kubwa kuliko sauti ya Mbunge wa NCCR Mageuzi anayetoa maoni yake kuhusu Muswaada wa marekebisho ya Katiba? Jambo muhimu kabisa kwa nchi yetu kwa wakati huu. Tujisahihishe ili tusonge mbele kama taifa moja.Maggid,
Iringa,
mjengwablogspot.com: The Best Search Links on the Net

endelea kuumiza nafsi yako kwa kuangalia hiyo tv channel
 
TBC1 ilikufa toka siku ile alipoondoka Tido Mhando. Wakaacha weledi na kukimbilia ushabiki na vimemo.
 
Mnahangaika nao waniniii......AH lakini NO wale si ndo kodi zetu zinaendesha TBC,naona kuna haja ya kuwajadili kwa kina humu jukwaani,nadhani walioamua kama mimi kutokuangalia kabisa tutakuwa tumekubali TBC ambacho ni chombo cha umma kitumike kwa manufaa ya CCM na CCM B na ni kweli kimekuwa kituo cha propaganda cha CCM.Itabidi tujadili hili kwa kina na tupate solution.
 
Ili kumalizia siku vema angalia taarifa ya habari ya Mlimani TV saamoja na nusu jioni/usiku. Hii ni kwa walio Dar au wenye ving'amuzi starmedia.
 
JF bwana POLICCM, TBCCM, TISSM, BUNGECCM, COURTCCM, hahaha raha utamu.....mabadiliko ni lazima.
 
Mlimani tv!!!!!!!!,sisi wanaudsm wenyewe hata hatuipendi.Huwezi kukuta mwanachuo anaangalia hyo channel.Tbccm imeisha kwanza inatuaibisha hata kuwa kwenye dstv coz haijakizi viwango,toka tido aondoke nayo ndo ubora unashuka.
 
Kweli kabisa, aibu tupu. Kuna cku nilikua naperuz channels za dstv nakaona sio mbaya kuicheck tbc...weeee...hio quality ya picha na sauti..O.M.G. it's a shame for sure. Vipindi vyenyewe havivutii..grrrrrrrrr..TBC be creative and provide quality service bana, munatuaibisha wajameni.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom