Tbc dhambi inawala....

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
Hivi karibu TBC1 imeanzisha kipindi kinachorushwa kila Jumamosi saa 1 usiku chenye jina 'Huku ndio Kwetu',ambacho kinawatembelea na kuwahoji watu hasa wanaoishi maeneo ya uswahilini kama Mbagala,Gongo la mboto nk kwa hakika hiki kipindi ni aibu kwa kituo kikubwa kama hiki...kipindi kinafanana kwa kila kitu na kipindi cha uswazi kinachorushwa na EATV...najiuliza

  • Huyo mhariri wa vipindi hakujua kuwa ni photocopy ya EATV
  • Au ni dhambi ya kumchakachua TIDO ndio inawala
 
[Huyo mhariri wa vipindi hakujua kuwa ni photocopy ya EATV

Hata kile kipindi cha saa mbili kamili sijui kinaitwa habari ni photocopy kabisa na taarifa ya habari ya ITV..kama vipi kesho tuandamane.
 
Hivi karibu TBC1 imeanzisha kipindi kinachorushwa kila Jumamosi saa 1 usiku chenye jina 'Huku ndio Kwetu',ambacho kinawatembelea na kuwahoji watu hasa wanaoishi maeneo ya uswahilini kama Mbagala,Gongo la mboto nk kwa hakika hiki kipindi ni aibu kwa kituo kikubwa kama hiki...kipindi kinafanana kwa kila kitu na kipindi cha uswazi kinachorushwa na EATV...najiuliza

  • Huyo mhariri wa vipindi hakujua kuwa ni photocopy ya EATV
  • Au ni dhambi ya kumchakachua TIDO ndio inawala

Hao wamepoteza mwelekeo. Sasa wanatoa vipindi vya ajabu ajabu, sasa wapo kwe Babu Samunge, wanatoa vipndi vya wakulima wa Marekani badala ya kuangaliwa wakulima wetu kule Namanyele nk.
Hata wanatangazaji lugha haipo njema, siku moja nilimsikia mtangazaji akilonga eti" treni hiyo ilijikuta ikiacha njia na kugonga ukuta....!!!
 
tumewazoea copy and paste toka Tido aondoke wamepoteza mwelekeo ukiangalia watangazaji wa vipindi vya tv nyingine wamewachukua nawanaenda fanya vipindi vilevile
 
Tbc fm nako upuuzi mtupu..! Juzi wakapiga wimbo wa Juma Nature - ugali, mwiso mtangazaji akasema '' mlikuwa mnasikiliza kibao cha Ugali kilichoimbwa na msanii Juma na-tu-re (natule ugali au wimbo)..!!??
 
TBC1 kwa sasa inajiendesha kwa uzoefy na siku watu wakishituka itarudi enzi zile za TvT
 
Nimeona hivyo vipindi kama cha uswazi na juke box , mzimu wa Tido utaendelea kuwatafuna . Wanahitaji mabadiliko .
 
Back
Top Bottom