Tawi la Chadema Marekani

NI KWELI KABISA MKUU, LAKINI PIA WATANZANIA WALIOPO NJE WAMEKUTANA NA MAMBO MENGI IKIWA NI PAMOJA NA YALE WALIYOKWISHA YAONA TANZANIA WANAPOKUWA NYUMBANI, THIS IS GOOD RECIPES katika mchakato wa kujenga taifa
kwangu mimi nikiwa mtanzania nayethamini uhuru wa kutoa mawazo na kuanzisha vikundi, sioni ubaya wa suala hili, naikiwezekana watanzania wote walio nje jiungeni kwa pamoja kuweza kutoa mawazo yenu hasa ya mabadiliko, ili tutokomeze ufisadi kabisa. Naamini wote kwa mamoja tukiungana tutaweza, na kila mmoja akitimiza ajibu wa kutetea raslimali za tanganyika ambazo ndizo zinaliwa na mchwa hawa
 
Mag3 wazo lako ndilo tunapaswa kuwalitekeleza, lakini kwa watu tuliolishwa itikadi za kiajabu, watu wachache sana wanoifikiria tanzania badala ya vyama, kwamba kama aliyeunda wazo anakufa na anachokianzisha hufa mara nyingi, isipokuwa mawazo na ardhi hubaki. Lakini kila jambo lina wakati wake. Ningekuwa mimi ndio naweza kuwabadili watu mmawazo na fikra zao cha kwanza ilikuwa ni kuiondoa ccm nambo yake yote,kisha wazalendo wakaipa mwelekeo. Nahisi watu ukiwaambia Tanzania kwanza watakushangaa. Lakini ukiwaambia kidumu chama fulani, na mbaya zaidi siasa za vyama imekuwa kama dini.
Kuhusu mzee mtei nami nimpe pongezi, ila upande wa fidia nadhani Mungu atakupa fidia endapo tutapata mabadiliko ya kweli na ambayo yatamfanya kila raia kufaidi matunda ya kuwa huru.
Kuhusu kiwalo cha wakubwa, mimi nakihusudu sana. Mimi ni ishara ya kuwa ni watu wa kazi, suti hizi una raha gani acha wachina wavae, kama uliangalia congress yao mwaka huu ni watu serious, wanajadili mwelekeo wa nchi bila mapambio wala taarabu. Mi nadhani hawa wakubwa waendelee mimi japo si mwanachama nalipenda sana na hasa likivaliwa na wale akina mama, wanaoneka si watu wa mzaha ni wanawake wanaoweza kukombo nchi. Hii ndio trademark yao. Na inaonyesha wanapambana na mafisadi, wakimaliza kazi basi mazingira yatajieleza.
 
WAKUU WATAIMALISHA UTAIFA KWA KUTIA NJIA GANI SASA?, MAANS CHADEMA NI CHAMA CHA SIASA
,INA MAANA WAFUNGUE BALOZI KAMA ZA SERIKALI? AU WAWATELEKEZE HAO WATANZANIA?
kwa vyoyote vile CHADEMA ni chama cha siasa na hakitaweza kutenganishwa na itikadi zake, hii ni sawa na kujinyosha damu mwenyewe,
kwa kupitia itikadi za chama bado umoja wa kitaifa unawezekana, hayo mengine uliyosema nadhani ni kazi ya serikali
tatizo ni pale ccm inapoitumia serikali kufanya mambo yake,
na kamwe chama cha CHADEMA hakiwezi kuhachana na siasa la sivyo kitaitwa jina jingine. "
wahenga walisema mtoto umleavyo ndivyo hakuwavyo, kama chama hakitafanya mkakati wa kuwafikia watu wote kwa karibu kuna hatari ya kupata wanachama walio na msimamo wa chama " .
ZINGATI ( ninaposema mtoto umleavyo nina maana wanachama ni watu wana background tofauti kuna hana ya kukomaza watu kisiasa kwa mtazamo wa chadema, REGEA waziri mkuu wa UNITED KINGDOM kakuvya ndani ya chama, )
UTAIFA na mitazamo ya kisiasa ni vitu viwili tofauti, ni katiba pekee inayoweza kulinda utaita kwa kuheshimu haki ya kila mtu na uwajibikaji ndani ya TAIFA.
hayo mengine yoyote tumevurugwa akili na watawala, wanajua nguvu ya vyama vingi katika kuleta mabadiliko, ndio maana siku hizi utasikia habari za udini , ukanda na mambo binafsi ya mtu. haya yote ni mkakati wa wao kutufanya kulale usingizi wa pono,
kikwazo kikubwa cha utaifa ni wizi wa mali za umma, unaofumbiwa macho na serikali na sio itikadi za kivyama?
Mzee Mtei kwa hili naomba kutokukubaliana nawe kabisa. Lingekuwa la maana zaidi kama Chadema, tofauti na CCM, ingejikita katika kuimarisha umoja wa Watanzania waliopo ughaibuni kwa kutanguliza utaifa badala ya itikadi. Naamini kwa dhati kuwa kufungua matawi ya vyama nje ya nchi ni upofu uliosababishwa na mfumo mfu chini ya utawala wa chama kimoja.

Kama tulivyoweza kupiga marufuku matawi ya chama makazini, yafaa tuendelee hadi kwa vijana, wazazi na wengineo. Tunashabikia mambo yasiyo na manufaa yoyote kwa jamii katika kujenga utaifa kwani kuna siku tutaanzisha umoja wa wanasoka wa Chadema au umoja wa walaji wa Chadema ! Hizo ni mbinu za kibaguzi za CCM na hazina nafasi Chadema.

Ni mawazo kama hayo yanayowafanya hata wabunge wasahau jukumu lao la kutetea maslahi ya taifa na badala yake kulinda ubinafsi. Tanzania kuna mambo tunayafumbia macho lakini madhara yake huko mbele ya safari ni makubwa mno. CCM inabidi ifanye hivyo kwa sababu hawana nia madhubuti ya kuachia madaraka kwa njia ya amani hivyo silaha yao kubwa ni uchonganishi na ubaguzi.

Natamani CCM wangeturudisha huko huko kuliko kudai walitutoa mbali kumbe tumeganda pale pale kama viwete huku wenzetu wakikata mbuga. Badala ya vijana kujiendeleza kwa bidii katika masomo huko kwa wenzetu, wamekaa kufungua matawi ya CCM, ujinga mtupu. Haya matawi sana sana yanatoa tu hifadhi kwa watoto, wajukuu na washikaji wa mafisadi.

Lile ni vazi linalotumika sana na farmers, hata mimi nilikuwa nalo, nyerere alikuwa nalo. Unaboa:lalala:
 
Nashukuru kuna WanaJF wanaunga mkono wazo la kuwa na matawi ya CHADEMA nje ya Tanzania. Of course, matawi hayo ni lazima yafunguliwe kulingana na sheria za nchi husika na uongozi uchaguliwe kufuata masharti,maadili na miiko yetu.

Sasa nijibu maswali yasiyohusika na matawi ya CDM niliyoona nikisoma michango ktk thread hii hapo juu:-

Katika picha ya avatar ya "lifeofmshaba" mtu aliyekaa kati ya Kawawa na jamaa aliyeshika kichwa ni Edward Moringe Sokoine.

Kuhusu mimi kulipwa fidia kwa kuanzisha CHADEMA kama "Superfisadi" anavyokumbusha kuwa kuna thread iliyopendekeza hivyo, kwanza nikiri kwamba sijasoma hiyo thread.

Pili ningetaka kusema kwamba kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa najisikia ninafurahi sana kwamba Chama nilichoshiriki kuasisi kinapiga hatua mbele kuelekea katika malengo yake. Kila siku namshukuru Mwenyezi Mungu kwamba ameniwezesha kuona baadhi ya matunda ya juhudi hizi: ambayo ni kuingiza na kusimika nchini Tanzania, demokrasia ya kweli. Najua bado hatujaweza kuonyesha mafanikio ktk maendeleo ya kweli kiuchumi na kijamii, lakini naamini mchango wa CDM unaanza kudhihirika, na endapo Watanzania wataamua tuchukue dola, basi mambo yatanoga.

Tatu kuhusu kulipwa fidia, nieleze ni kweli kwamba katika miaka yangu sita niliyotumikia CHADEMA kama mwenyekiti taifa, sikulipwa mshahara wowote na sikusaidiwa kodi ya nyumba nilipokuwa naishi Dar es Salaam. Pia nilitoa magari yangu kwa shughuli za chama pale mwanzoni, na wakati chama kilipomudu kunipa gari kwa safari za chama, nililiacha Dar es Salaam kwa mashughuli ya chama ilipokuwa ni lazima nirudi nyumbani kwa mashughuli ya kifamilia.

Nne nieleze kwamba katika utumishi wangu kwa umma (mfano Gavana BoT, Katibu Mkuu, EAC na Waziri wa Fedha nililipwa kiinua mgongo, yaani gratuity) na sasa nalipwa pensheni kidogo kwa kuwa civil servant kwa miaka 7 kabla ya uGavana na Mkurugenzi Mtendaji wa IMF kwa miaka 4. Kwa hiyo huyo mwanaJF aliye pendekeza Chadema inifidie, labda alielezwa juu ya kujitolea kwangu kwa umma na mafao yangu yaliyo kiduchu.

Nilivyoeleza hapo mwanzo, ni furaha kwangu iliyoje kwamba tumeweza kuifikisha CHADEMA hapa ilipo. Itambuliwe pia kwamba, the supreme effort and sacrifice is still to come kama tunavyoelekea 2015. Hata hivyo, endapo uongozi wake utakuwa na uwezo wa kufidia waliowezesha CDM kufika hapo ilipo, bila kuathiri malengo yetu matakatifu, makuu na muhimu, basi iwe hivyo.

Mzee Mtei Nashukuru sana kwa ufafanuzi wa hiyo picha ya avatar ya 'lifeofmshaba' Ebu nisaidie na hili la Balali na Nyakyi; ili kuwa waje? D. Balali ambaye ndie alikuwa M/kiti wa tawi la Chadema USA kuhukwaha U-Gavana ndani ya serikali ya CCM na Barozi Anthony Myakyi ambaye hata hakuwa mwana Chadema kuvuliwa uteuzi kwa kukukarika nyumbani kwakwe kupata Chakula tu!

Best Regards.
 
Mzee mtei naunga hoja yako kwa CDM kuwa na tawi nje ya nchi. Bt nakiri umenistua sana, SIKUWAHI KUHISI KUA DAUDI BALALI ALIKUA MWANA CDM!
 
Nashukuru sana Mzee wetu Mtei, binafsi nimefarijika kwa kupata maelezo yako lakini pia nimegundua unahazima ya mambo kadhaa ambayo naamini kama siku ukipata muda ukayaweka hapa basi humu jamvini tutajifunza mengi toka kwako.

Naunga mkono uwanzishwaji wa matawi nje ya nchi na kama ulivyosema kuwe na taratibu kwa kuzingatia maadili na malengo ya chama na si vinginevyo kama wenzetu CCM kuweka mbele maslahi yao zaidi, kwani naamini haya matawi yataeneza malengo na mikakati ya kukiimarisha chama kuwa na taswira ya kitaifa zaidi.
 
Historia yao hao waarabu ni ndefu mkubwa....mbona nyie mpaka leo hamjaonyesha makeke yoyote kuhusu katiba??au mauaji ya arusha??ni strengthen zipi ambazo mtazipata na kuzionyesha kuhusu njiii yetu hii...ufisadi still destroys us harshly and not softly...thats why nyie mmekimbilia ughaibuni!!
Hater!!
 
WanaJF Arafat na Gagurito wame fanya comments ambazo niingetaka kufafanua.

Daudi Ballali na mimi tulifahamiana tangu mwanzo wa 1966 nilipoteuliwa Gavana, yeye akiwa anamalizia masomo yake Chuo Kikuu huko Washington DC, na mimi nikihudhuria semina maalum ya magavana na deputies wao iliyoandaliwa na IMF. Nilimwajiri alipokamilisha masomo yake, na alijiunga na Benki Kuu ya Tanzania kama Economist mwishoni mwa 1966.

Nilipoachia kiti cha uGavana 1974, naye Ballali aliomba na kupata kazi IMF, akahamia Washington DC kama mfanyakazi. Hatimaye mimi mwenyewe nilijiunga na IMF kama Executive Director 1982, na tulishirikiana sana na Ballali na familia yake kwa miaka ile minne niliyoishi Washington DC. Kwa hiyo nilipozuru Washington DC 1993/4, nikiwa Mwenyekiti Taifa haikuwa vigumu kumpata Ballali kama mwanachama mpya wa CHADEMA. Ballali aliongoza tawi la Chadema Washington, kama nilivyoeleza hapo awali.

Rais Mkapa alipomteuwa Ballali kama Mshauri wake wa kiuchumi, of course, hangeweza kuendelea hadharani na ushabiki wake katika chama cha upinzani. MwanaJF mmoja anasema haku'hisi' Ballali ni MwanaCDM! Hili sio jambo la kuhisi, aidha sasa sio jambo muhimu la kujadili kwa kirefu.

Kuhusu Anthony Nyakyi kuitwa nyumbani na ajira yake ya Ubalozi UN kusitishwa, ni jambo lililodhihirisha Serikali ya CCM kutokumbatia multi-party politics kwa dhati, na pia kuchanganyikiwa kwa wengi wa maofisa waandamizi wake. Kituko hiki kilitangazwa sana na vyombo vya habari wakati huo na singetaka kuchukua muda zaidi kufafanua.

Ningesema hata dalili za sasa za viongozi na maafisa waandamizi wa CCM kuona maandamano ya amani ya CDM, kwamba ni uchochezi na uhaini, zinadhihirisha uhafidhina mkongwe na kutokukubali mabadiliko.

Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
 
Ndugu Zangu Wana JF Wote,

Ni muhimu sana kuwa na umoja wa wanachadema wanaoishi nje ya nchi kwa kuwa na matawi yanayoratibiwa moja kwa moja na katibu mkuu wa chadema makao makuu, Lazima tuwe open minded people, kuna faida nyingi sana Chadema inazoweza kuzipata kama tutaweza kuratibu matawi ya chama nje ya nchi.

.Kuwa na matawi ya wanachadema yanayoratibiwa na makao makuu ya chama:

1. kutawezesha chama kupata michango ya fedha na vifaa vya kuendesha shughuli za chama, kwa mfano matawi mengi ya chama mikoani hayana vifaa muhimu vya kiutendaji kama vile, fax, computer, copying machine, nyenzo za usafiri kama magari, pikipiki na baiskeri ili kurahisisha mawasiliano kwenye matawi yote vijijini kufikisha ujumbe wa ukombozi kwa watanzania. tukiwa na matawi itakuwa rahisi kuratibu na kuwasilisha michango hiyo huko nyumbani kuliko kuwasiliana na mtu mmojammoja. Watanzania waishio nje ya nchi wana haki sawa na wajibu sawa na mtanzania alie nyumbani, tubadilishe fikra na kuona mtu alie nje hana mchango wala tija kwa taifa, anaweza asipige kura lakini akasaidia kupatikana kwa wapiga kura wengi zaidi.

2.Watanzania wengi waishio nje ya nchi baadhi yao ni proffessionals na wenye exposure ya hali ya juu, hivyo ni hazina kubwa kwa chadema kupata mawazo na hazina ya viongozi wenye experience kubwa na connections zinazoweza kutumika kuwaletea wananchi maendeleo

3.Kuwa na matawi ya chadema abroad ni nyenzo muhimu ya kukuza image ya chama kwenye international forums, kama vile international media, ni rahisi kwa tawi la chadema kuandaa maandamano kupinga maauji ya Arusha pindi JK anapohudhuria ziara za kimataifa, na ni platform inayoweza kutoa publicity of true picture ya ukandamizaji wa demokrasia unaofanywa na serikari ya ccm, actualy watanzania waishio nje ni sauti yetu muhimu kwa jumuiya za kimataifa pindi watawala wanapoamua kuzima vuguvugu la mabadiliko, wanachadema waishio china, Russia, USA, South AFrica, spain, Uk, Hong Kong, Japan na sweeden wakiandamana kupinga ubazazi wa ccm ni ujumbe ambao utakuwa loud and clear kwa jumuiya ya kimataifa, hivyo all what we need ni matawi kuwa regulated ili yasiende rogue kama matawi ya ccm, nadhani ni muhimu Dr. Slaa akatuwekea utaratibu mzuri wa kuweka matawi haya.

4.Ni nguvu kubwa ya CHADEMA BLOGSPHERE, Na majadiliano ya kwenye mitandao kama facebook, twitter, jamiiforums, wanasaidia sana kutufungua macho na kujadili maswala mengi yanayohusu mustakabali wa nchi yetu, hivyo tuwaache wawekewe utaratibu unaoleweka ili waweze kushiriki kikamilifu kwenye ujenzi wa chama imara na maendeleo ya taifa letu,

Watanzania wengi wana steriotype ya kuogopa watu wanaishi nje ya nchi au wageni nadhani inabidi tubadilike sasa, sote tunahitajika kwenye ujenzi wa chama na taifa letu na kuwa nje ya nchi hakuzui kushiriki kwa njia moja au nyingine.

Aksanteni sana ndugu zangu hasa Sinzaga na QUININE
 
Mzee Mtei,

Tunashukuru sana kwa kutoa ufafanuzi wa maswala mbali mbali ambayo wengi wetu hatukuweza kuyafahamu kwa undani, nadhani hii inatoa changamoto kwa vijana wengi ambao hawafahamu vyema harakati za mapambano ya mfumo wa vyama vingi Tanzania, vikwazo na mafanikio na athari walizopata wapambanaji mbali mbali kama marehemu Joseph Kasellabantu, Kasanga Tumbo, James Mapalala, marehemu Oscar Kambona, Abduhaman Babu na wengine wengi, historia ya nchi hii iko kimya kwani tunafahamu mateso na dhiki walizopata wapambanaji, au kuhujumiwa na serikari ya ccm, mimi nadhani ni hazina kubwa kuwa na mzee kama wewe ndani ya chadema na tunaweza kujifunza historia iliyo sahihi juu ya manyanyaso ya ccm enzi za kuanzisha mapambano ya harakati za ukombozi ndani ya mfumo wa chama kimoja.

Mzee Mtei, tutashukuru sana kama utapata nafasi ya kujadili nasi hiyo sehemu ya historia ambapo itakuwa msaada mkubwa kwa vijana wengi kufahamu ukweli ulivyokuwa na jinsi mlivyopambana, kwani ccm hawawezi kuweka historia hiyo hadharani.
 
CDM kwa umakini ule ule hebu kapitieni kwanza michango ya huyu VP hapa jukwaani. Kama ninazo kumbukumbu ambazo zinabainisha kinyume kabisa n haya anayoyzungumza hapa. Kama haya ninayoyafikiria si kweli ... huko ma-mtoni CDM naona kama vile bado kidogo hiv sijui wenyewe mnaona nini hapo?.

Mimi ninaona ni vizuri V.P. akapewa njia y kufungua tawi ili atimize azma yake aliyonayo moyoni kama mpenzi wa CDM
 
Well si wewe ulieandika OPEN LETTER TO SHYROSE BHANJI sasa ni nini kinakutaka kujua kuhusu Chadema?

Mmeona Matawi yenu ya CCM pesa zinavyoibiwa? Chadema haina muda huo...

Tunakuogopa, Umeingia Jamii Forum pia kutuchafua kama ulivyomwandikia barua ShyRose Bhanji???
 
Back
Top Bottom