Tawi la chadema chuo kikuu mwenge-moshi laazimia kufanya harakati nchini kuimarisha chama vijijini.

MWANAKASULU

Senior Member
Nov 18, 2011
195
67
HOTUBA YA M/KITI CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO CHADEMA TAWI LA CHUO KIKUU MWENGE-MOSHI BAADA YA KUSIKILIZA MAONI,MAPENDEKEZO NA USHAURI JUU YA AGENDA KADHAA ZILIZOJADILIWA NA WANACHAMA.KATIKA MKUTANO MKUU WA WANACHAMA WOTE ULIOFANYIKA TAR.22/12/2011 ENEO LA OFISI YA TAWI.
Ndugu wanachama wenzangu awali ya yote naomba nimshukuru Mungu mwenye wingi wa Rehema tumeweza kukusanyika hapa kwa uweza wake wote tukiwa wazima Sambamba na hilo kwa niamba ya wanachama wote wa tawi letu kwa masikitiko makubwa natoa pole kwa Wakazi wote wa jiji la Dar es salaam walioathirika kwa namna yoyote kwa garika/janga ambalo halikuwahi kutokea tangia Tanganyika imepata uhuru.Hivyo mwenyezi Mungu awatie nguvu na Ujasiri ktk kipindi hiki kigumu kwa ndugu na jamaa waliokumbwa na jinamizi hili.
Kabla sijajielekeza kujibu hoja zilizotoka kwa wanachama kwa moyo wa dhati nawashukuru sana Makamanda wenzangu kwa mahudhurio yenu na kwa michango yenu yenye tija na kuimarisha chama chetu.Kwa kuwa hoja nyingi zimefanana zingine zimejibiwa na wachangiaji lakini nitajihadi kupitia kila hoja.
Kwanza kabisa makamanda wenzangu napenda niwajurishe kwamba Mwanachadema popote pale alipo yuko vitani yatupasa tukae kikamanda zaidi kwani sasa hivi Serikali ya CCM kwa kupoteza mvuto na ushawishi wake wa awali serikali inatumia nguvu kubwa ya dola mfano police kutupiga mabomu na viongozi wetu kufunguliwa mashitaka ya ajabu malengo yao ikiwa kudhoofisha Mvuto uliopo wa CHADEMA kwa Wananchi wa Tanzania, Majuzi tu tumeshuhudia mwandishi wa Gazeti la Mwananchi alivyofunguliwa mashitaka ya ajabu,mwandishi wa Tanzania Daima alivyoonewa na kupelekwa rumande ,tunakumbuka hata gazeti la Mwanahalisi limeshafungiwa miezi mitatu kisa imeandika ukweli dhidi ya ufisadi ambao unaibuliwa au ulioibuliwa na CHADEMA.Kwa hili nawadhibitishia kwamba CCM watachemka wamekumbuka shuka kukiwa tayari kumekucha na CCM imebaki inalala ambapo CHADEMA tumeamuka.Hivyo hata wajipange kwa vikao vipi hawataweza kufifiza Mvuto wa chama chetu kwa sababu Serikali ya CCM imeshindwa kutatua matatizo ya watanzania hivyo watanzania wanahitaji sasa serikali ibadilishwe na si vinginevyo.
Pili serikali imekuwa ikishinikiza baadhi ya wakuu wa Vyuo ili wanafunzi wafukuzwe kwa sababu tu eti wanafunzi hao wameonekana wakishabikia siasa.Tumeshuhudia UDOM,tumeona wanafunzi 43 UDSM,na 66 Mhimbili.Sisi kama CHADEMA kupitia M/kiti wetu wa BARAZA LA VIJANA CHADEMA Bw.John Heche tumelaani ukiukwaji huu wa haki za Wanafunzi uliofanywa na wakuu hao wa Vyuo.Nadhani serikali haina kumbukumbu sahihi juu ya Hayati baba wa Taifa kwamba harakati za Mwl .J.K.Nyerere kukomboa Tanganyika yetu alizianzia akiwa Mwanafunzi wa chuo kikuu cha OXFORD UINGEREZA akisaidizana na Waafrika wengine waliokutana na kutengeneza umoja wenye nguvu ili kuipigania Afrika Je! Mwl angefukuzwa masomoni huko Oxford Tanganyika ingekombolewa? Pia ni vyema tumukumbuke Bw.V.I.Lenin 1917 alivyopigania USSR bado akiwa mwanafunzi nchini Ujerumani baada ya kusoma kitabu cha mwanaharakati Bw.Karlmax.Je huyo Lenin angefukuzwa huko Ujerumani masomoni je USSR ingekombolewa?
Baada ya kusema hayo naomaba niwatoe wasiawasi Makamanda wangu na wanafunzi wenzangu Naomba tusisahau hotuba ya katibu mkuu Dr.Willibroad P.Slaa aliyoisema alifyokuja kufungua tawi letu.Kwamba tuwe mbele kusimamia haki,na kwamba haitokuwa na maana ya kupeperusha bendera ya CHADEMA kama watu wataonewa harafu sisi kwa kuogopa tukae kimya akasema hakuna aliyeko juu ya sheria hivyo chama kitashughurikia yeyote anayekiuka Sheria.Hivyo basi kukwepa ukiritimba wa Serikali na kutambua kilichotuleta hapa chuoni basi nawaombeni na nakuwasihi sana kwamba tukiwa ndani ya chuo tusiwe na harakati yoyote ile ya chama lakini tukitoka nje ya chuo hususani tukiwa hapa ofisini kwetu hakuna atakaye weza kututishia chochote kwani tutakuwa sehemu yetu hata sheria itatulinda.
Tatu nawaombeni sana kwamba sisi wasomi tunajua kabisa hatuko CHADEMA kwa ajili ya Ushabiki ni kwa sababu tu sisi wasomi tunaweza kuutumia usomi wetu kuikomboa jamii kwa mstakabali wa Nchi yetu bila kujali tofauti za Itikadi,rangi,Dini na Kabila.Kwa kutambua hivyo basi naomba niwatangazie Waraka na.1 wa Katibu Mkuu CHADEMA unaotaja kwamba uchaguzi mkuu wa chama ngazi zote utafanyika 2012 na kumalizika 2013 hivyo basi nawasihi na kuwashauri kuna haja ya nyie kugombea nafasi yoyote na ngazi yoyote katika eneo utokapo.2015 CHADEMA tunachukua nchi hivyo Viongozi wetu wameona ni vyema Uchaguzi ufanyike mapema ili makovu yatakayojitokeza yafutike kabla ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa2014 na Uchaguzi Mkuu 2015.Na chama kiko makini kwa hili ili tupate viongozi makini watakaosimia ukweli,uwazi na maadili kwa mjibu wa katiba ya chama.
Nne makamanda mmechangia mawazo mazuri juu ya chama chetu kinavyosimamia mpaka nchi yetu ipate katiba mpya kiukweli swala la katiba mpya lilikuwa kwenye ILANI ya chama chetu tu katika uchaguzi wa 2010.Bahati mbaya kwenye ilani ya CCM hawakuwa na wazo la katiba na wala hata Rais alivyozindua bunge baada ya Uchaguzi hakugusia swala la Kupata katiba mpya lakini Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametoa wazo la kupata katiba tar.31/12/2012.Tena huku wakitofautiana kauli na mwanasheria mkuu wa Serikali pamoja na Waziri wa sheria na Katiba.Mbali na wabunge wa CCM kupitisha mswaada ambao mpaka sasa Rais ameshasaini CHADEMA tunasema tutasimama kidete mpaka tupate katiba inayokidhi watanzania, 1.Wabunge wetu walitoka bungeni kupinga huo mswaada ampapo wabunge wa CCM walishindwa kujadilii mswaada wakajadili CHADEMA na Tundu Lissu,2. Kamati kuu ikatuma kamati ndogo kufikisha mapendekezo ya chama wakaweka makubaliano ambapo serikali ilikubali kuendelea kupokea maoni na mapendekezo ya wadau,3.Tar.7/12/2011 chama kimetoa semina kwa wanachama mikoa yote nchini na kupata maoni kwa maboresho zaidi hatua zote hizi tumezifanya kwa njia ya mazungumuzo tena kwa amani ila tahadhari kwa Serikali ni kwamba kwa kuwa Rais mwenyewe alikili kufanya Marekebisho hivyo naendeleza kumuomba atekeleze alichokubaliana na kamati yetu iliyofika ikulu.Kama bunge lijaro litashindwa kupokea maboresho ya CHADEMA basi tunaenda kwa wananchi bahati nzuri wananchi tumeshawaweka mkao wa kupigania katiba yetu mpaka kieleweke.
Tano Makamanda nakubaliana na maoni yenu juu ya kuimarisha uchumi na kupata vitendea kazi vya ofisi ya tawi letu kwani natambua hatuna chanzo cha mapato kwa ajili ya kulipia ada ya pango la ofisi yetu na hatuna fanicha.Hivyo kama wajumbe mlivyosema kwamba kamati tendaji ibuni mradi,proposal ya vitu vinavyotakiwa na kiasi cha pesa ili tupange siku ya kufanya harambee na kualika wadau mbalimbali wakiwamo viongozi wa chama madiwani pamoja na wabunge.Lakini baada ya harambe tawi letu lina Mpango kabambe wa kutengeneza project maalumu ya chama kwa makamanda wote wa tawi letu ili tukaimarishe chama Vijijini nchi nzima tawi letu tumeamua kwa kutambua kwamba kweli wasomi wamekikubali chama chetu lakini ni wasomi wachache wanaofika vijijini kwa ajili ya kuelimisha jamii walio Wengi michango yao mizuri inaishia kwenye mitandao tu mfano Facebook,Mwenge forum na Jamii forum wakati watanzania takribani asilimia 90 na ambao ndo wapiga kura hawajawa na uwezo wa kupitia habari kwenye mitandao Hivyo tusibweteke kabisa twende vijijini mijini hakuna kazi tena.Uongozi wa tawi letu utapanga majina ya watu tutakaowatuma kwenda vijijini vilivyopo katika majimbo yote nchini mkoa kwa mkoa kikubwa tutaendelea kuwasiliana na viongozi wetu kwa Ushauri na utekelezaji Zaidi Ila kwa hili naombeni sana tusitangulize masilahi mbele.Hivyo ninawaahidi tutakaa kama kamati tupendekeze vitu kadhaa na kuwaalika wabunge ili waje kweye harambee hii tuweze kufanikisha miradi itakayo tuwezesha kuwafikia wananchi Vijijini
Sita kuhusiana na wazo la vyeti vya CHASO{CERTIFICATE FOR CHADEMA STUDENTS ORGANIZATION} hili ombi nitalipeleka ngazi za juu kwa maamuzi ili wanao graduate degree wawe wanapatiwa Cheti kitakachoonesha mchango wako katika chama ukiwa masomoni na hili naona ni la msingi kwani cheti kitakutambulisha kwa viongozi na tutaweka sifa za watu wanaofaa kuvipata endapo uongozi ngazi ya juu utakubaliana na hili wazo.Lakini kikubwa zaidi makamanda nawaombeni sana kila muendapo hubirini elimu ya Uraia tena mkisisitiza Vijana kwamba siku serikali itakapotangaza tar. Ya kuboresha daftari la wapiga kura basi kila mmoja ashike vijana kumi aende nao wakajiandikishe.kweli tunajua kabisa chama chetu kimependwa na rika zote lakini wapo vijana wengi wanakosa sifa za kuchagua Diwani,Mbunge na Rais kwa sababu ya kukosa kitambulisho cha mpiga kura CHADEMA tutapita nyumba kwa nyumba kuwasihi vijana wakajiandikishe.
Saba napenda kuwashukuru wanoendelea kujitolea kufanya kazi ya chama na nawapongeza wazee waliojitokeza kuongeza nguvu kwenye tawi letu pia nampongeza mzee Samwel Ndauka kunikabidhi kadi ya CCM kwa hiali yake na nikampa kadi ya CHADEMA na ameturuhusu kutumia gari yake tutakapokuwa tunataka kufanya shughuli za CHAMA tukiwa maeneo ya hapa Moshi.Na tayari tawi letu lina Uongozi Baraza la Wazee pamoja na Baraza la Wanawake lakini sijalidhika na Idadi hii ya Wanawake najua hapa Chuoni wanawake ni wengi Hivyo naombeni Muwahamasishe kwani baraza la Wanawake mkishaniridhisha nitamuomba Kiongozi BAWACHA taifa aje kutupa mawili matatu.Hivyo nawakaribisha sana wazee wenye mawazo kama ya Ndauka kwani CCM imepoteza mvuto tayari CCM imeshawasiliti na kuwatelekeza wazee Wastaafu wa Afrika Mshariki.
Mwisho nawatakieni masomo mema tusome kwa bidii kwani hili ndilo jukumu kubwa lililotukutanisha hapa chuoni na tutambue hautakuwa Mbunge makini au kiongozi makini kama kitabu kitakupiga Chenga.Pia nawatakia Viongozi wangu na wana CHADEMA wote nchini Krisimas njema na heri ya Mwaka Mpya.Mungu awe pamoja nanyi katika sherehe hizi.

NI MIMI M/KITI CHADEMA TAWI LA CHUO KIKUU MWENGE{SAUNT BRANCH}
……………………………..
ABEL DENDWA NDIMANYI.
MUNGU IBARIKI CHADEMA NA MUNGU IBARIKI TANZANIA TUNAYOITAKA. AMENI.
 
Back
Top Bottom