Tawi Jipya La CCM DC Washington: Hongera Sana CCM's Diaspora!!

Ngoja nikujibu swali hamna mtu alikuwa anataka kuwa kiongozi wa jumuiya bali ilitokea kuwa kiongozi aliyegombania ni ccm na haikatazwi mtu kuwa kwenye chama kuwa kwenye jumuiya... Sasa wewe uliemchagua sandali mbona ni ccm na mwenyekiti wa tamco na hamkumyima kugombania kwa sababu tuu mamuya ni ccm damu ndiyo maana mkamtupa chini fyi mbinu zenu zilikuwa za kijinga sasa mnajuwa kuwa sandali ni ccm na hamtaweza kumtoa ni mwenyekiti wenu labda mumchaguwe mwingine midomo yenu wanatanzania ndiyo maana hamna jumuiya hata siku moja sababu kuna wazee hapa dmv kazi yao kuaribu amani sababu ya njaa ya maisha na uvivu uliyowatawala .watanzania wa dmv inabidi tuwe wakweli tusibishane bila sababu mtu anaweza kufanya kazi muachiani afanye kazi mtu anapenda chama cha ccm muachieni apende chama kila mtu anachaguwa cham achake anachokiamini bila matusi wala malumbano kwani matusi hayajengi au kukichukia chama sio kujenga nchi .watanzania wenzangu nchi yetu hatabadilishwa na chama chochote bali ni wewe mwananchi wa tanzania uliye mvivu , mjinga , mbishi , mlalamikaji , usiyependa maendeleo na roho yenye chuki jitahidi sana mbadilike kwanza ndiyo nchi yetu itabadilika wacheni majungu na uzushi huu mda mnakaa kubishana ujinga ungekaa mfundishe mwanao , kaka yako , dada yako jinsi gani ya kuepuka na madadhi ya ukimwi na njaa badala ya kuituka serikali yako wewe mtanzania jiulize mchango wako ni nini ?? Katika nchi umefanya nini tangu uamke??
Naomba msaada kutoka kwa yeyote yule ambaye ameweza kuelewa kilichoandikwa hapo juu...duh, kaazi kweli kweli!
 
Ni okay mnafungua tawi, lakini wasemaji wenu wanaonekana walopokaji na hawajajipanga. Jitahidini kutumia watu wenye public speaking knowledge. Mmejiabisha sana na hiyo clip.
 
user-online.png
Indume Yene Unakata maini kweli. Hii Ze-Utamu nilifikiri imekwisha sahaulika kumbe bado inakumbukwa kwa sana tu. Labda kwa sababu wamiliki wanajulikana?
Sasa
user-online.png
Indume Yene unapoiingiza Ze-Utamu kwenye topic inayohusu kuanzishwa CCM tawi lake huko DC ina maana waliokuwa wanamiliki hiyo blog ni wafuasi wa CCM?

Ze-Utamukama ingekuwa mmiliki wake ni mwana_CCM ingewezekanaje wamtukane na kumchafua kipenzi cha wa pale Magogoni kwa kumvua nguo?

Kama ni hivyo kuna kazi nzito ya kujisafisha la sivyo laani ya kumtukana Mwenyekiti wetu na kumvua nguo hadharani katu haiondoki bila kutolea swadaka ya njiwa mweupe kafara.

- Ndio maana tumewaasa wana-CCM DC, kujiepusha na majungu, fitina, na uzushi, migomo, matusi, maana haya sio mambo yetu CCM ni mabo ya wenzetu huko upande wa pili, na mifano ipo wazi kama huu wako!!

William.
 
W. J. Malecela Hakuna CCM hapo acha kuidanganya nafsi yako, hapo kuna kundi la watu amabo Maisha ya USA yameshawashinda sasa wanatafuta plan B ya kuweza japo kupora pesa ya walipa kodi ya Watanzania kama wenzao wa UK walivyofanikiwa kudhulumu mamilioni ya shilling.

Nimekuuliza swali huyo katibu mwenezi wenu Benjamin Mwaipajah unamfahamu? kama haumfahamu muulize Makongoro Mahanga au Kalanje watawaeleza, labda kama ni uenezi wa jambo lingine sawa, au muulize Mr II Sugu kuhusu huyo mtu.
Mimi nilikuwepo.
 
Last edited by a moderator:
- Yaani kwa kweli Kidumu CCM, pongezi sana Makada wetu huko DC kwa hatua kubwa na nzito inayohitaji maamuzi magumu sana, wana CCM huku nuymbani tumefarijika kwamba baada ya sarakasi za huku na kule, sasa tumeweza kuwa na Tawi jipya linalokidhi kanuni za Chama, CCM.

- CCM ni chama cha hoja, sio magomvi, matusi, migomo, ngumi, wala uuaji, hapana sisi ni chama cha amani na maendeleo na hoja nzito, sasa fanyeni kazi ya kuimarisha chama huko ili muwese kuhamasihsa majimbo mengine yafungue matawi ya CCM, na pia kuwashawishi wananchi wa huko kujiunga na chama chetu, yaani Chama Tawala CCM.

- Mheshimiwa MWenyekiti Mamuya, I have a trust in you kwamba mtajiepusha na majungu yanayotuletea matatizo makubwa matawi yetu huko nje, simamieni kwenye katiba, ukiona pahali popote kwenye chama CCM kuna mgogoro, ujue katiba imekiukwa, simamieni katiba badala ya perosnalities, ondokaneni na dhan ya kwamba kuongoza chama nje ni tiketi ya kuja kuwa mbunge Tanzania, au kuyatumia hayo matawi kuja kutafuta uwakilishi wa Diaspora katika bunge letu, fanyeni kazi za chama kwanza kwa uadilifu.

KIDUMU CCM!!

William John Samwel Malecela: MJUMBE WA WAZAZI MKOA WA DAR & MJUMBE WA CCM WILAYA YA ILALA.

ungekuwa na akili kidogo kama mjumbe mmoja hapo juu huenda hii nchi ingetokana na umasikini lakini huna target yeyote mkuu zaidi ya ushabiki wa chama cha baba yako!
 
Chama,
Kiongozi wa DMV Sandaly si mwana CCM. Na hiyo ilikuwa mojawapo ya sababu baadhi yetu tumesafiri maili 60 plus kumpigia kura. Yeye alikuwa ni kiongozi wa jumuiya ya Waislamu hapa DMV na kazi nzuri aliyoifanya ndiyo ilitufanya baadhi yetu tushabikie na kukubali uongozi wake.

Kulikuwa na njama za CCM kuteka jumuiya ya DMV kuwa kama jumuiya ya CCM zikihimizwa na afisa mmoja ubalozini ambaye kwa sasa jina lake nitalihifadhi. Lakini wajanja tuling'amua njama hizi na kwa sababu hatujawa na jumuiya kwa zaidi ya miaka 5 kutokana na sababu mbalimbali, tulikuwa tumepania tuwe na jumuiya chini ya kiongozi atakayeaminika, siyo CCM na wala si Chadema. Wagombea wote wa CCM tuliwatema chini. Wote.

Lakini la ajabu, alipokuja Kikwete hapa mwezi Juni, tulishangaa kuwaona viongozi tuliowatema wakiwa mstari wa mbele kutambulishwa kuwa ni viongozi wa CCM/DMV wakati hatukuwa na habari kuwa kuna tawi la CCM hapa. Hata kiongozi wetu Sandaly, aliwekwa pembeni, ukiona zile picha za viongozi waliokutana na Kikwete, Sandaly yuko kando kabisa.

Huo ndio uwongo ambao nimeuzungumzia awali na ndio uwongo ambao nitaendelea kuukemea. Sina shida na CCM kuanzisha tawi lao, lakini wasijifanye mapandikizi kwa jumuiya ya DMV. Unanipata? Tukutane pikiniki.

Jasusi,
Hilo unalosema linajulikana wazi, tatizo kubwa ni ubalozi ndio chanzo kikubwa cha kuvuruga jumuiya yetu, huyu afisa usalama kama anavyojinadi amekuwa mstari wa mbele sana kuvuruga jumuiya; jumiya haijiendeshi kwa kujiegesha na ubalozi; ni kitu kinachotuunganisha watanzania wa DMV bila kujali dini; kabila wala itikadi zetu kisiasa, hili la wanachama wa jumiuya kutumiwa kama ndio wanachama waccm sina uhakika nalo; ila kama walifanya hivyo haikuwa sahihi. Mimi ni mwanaccm lakini bado sijachukua kadi ya tawi, kadi yangu ya Gongo la mboto bado ipo hai na nailipia kila mwaka, hizi siasa za maji taka zivunje umoja wetu wa DMV, watanzania wa DMV wanahitaji jumiya kuliko haya matawi ya vyama yaliyojaa wasanii.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Ni vizuri sasa hivi mwende kwenye cities, manake M4C inakwenda kwenye villages!
 
Jasusi,
Hilo unalosema linajulikana wazi, tatizo kubwa ni ubalozi ndio chanzo kikubwa cha kuvuruga jumuiya yetu, huyu afisa usalama kama anavyojinadi amekuwa mstari wa mbele sana kuvuruga jumuiya; jumiya haijiendeshi kwa kujiegesha na ubalozi; ni kitu kinachotuunganisha watanzania wa DMV bila kujali dini; kabila wala itikadi zetu kisiasa, hili la wanachama wa jumiuya kutumiwa kama ndio wanachama waccm sina uhakika nalo; ila kama walifanya hivyo haikuwa sahihi. Mimi ni mwanaccm lakini bado sijachukua kadi ya tawi, kadi yangu ya Gongo la mboto bado ipo hai na nailipia kila mwaka, hizi siasa za maji taka zivunje umoja wetu wa DMV, watanzania wa DMV wanahitaji jumiya kuliko haya matawi ya vyama yaliyojaa wasanii.

Chama
Gongo la mboto DSM

Nadhani ndugu zetu mlioko huko ughaibuni ni watu wazima na akili nzuri. Sasa kwanini umoja na mshikamano wenu unavurugwa na watu wachache?
 
W. J. Malecela Hakuna CCM hapo acha kuidanganya nafsi yako, hapo kuna kundi la watu amabo Maisha ya USA yameshawashinda sasa wanatafuta plan B ya kuweza japo kupora pesa ya walipa kodi ya Watanzania kama wenzao wa UK walivyofanikiwa kudhulumu mamilioni ya shilling.

Nimekuuliza swali huyo katibu mwenezi wenu Benjamin Mwaipajah unamfahamu? kama haumfahamu muulize Makongoro Mahanga au Kalanje watawaeleza, labda kama ni uenezi wa jambo lingine sawa, au muulize Mr II Sugu kuhusu huyo mtu.
Mimi nilikuwepo.

- Kuna mbunge mmoja wa Chadema aliwahi kuniambia kwamba wewe umewahi kuhusika na kumuuzia Mh. Mahanga, kata moja ya Chadema wakati wa uchaguzi uiopita, vipi hizo tuhuma mkuu ni kweli au mbunge alikupkazia tu?

Es!
 
Nadhani ndugu zetu mlioko huko ughaibuni ni watu wazima na akili nzuri. Sasa kwanini umoja na mshikamano wenu unavurugwa na watu wachache?

- Ukiona makelele kelele na majungu maana yake kuna tatizo, sasa watu wapo majuu ungetegemea wawe wastaarbu maana wapo ustarabuni, lakini ni vigumu sana kuutoa uswahiili in wabongo, ndio tabia zetu hizi!!

Es!
 
ungekuwa na akili kidogo kama mjumbe mmoja hapo juu huenda hii nchi ingetokana na umasikini lakini huna target yeyote mkuu zaidi ya ushabiki wa chama cha baba yako!

- Badala ya Great Thinker naona unaanza kuwa mganga wa kienyeji mpaka kujua mambo ya kwenye fikra za wengine! duh!

Es!
 
Nadhani ndugu zetu mlioko huko ughaibuni ni watu wazima na akili nzuri. Sasa kwanini umoja na mshikamano wenu unavurugwa na watu wachache?
Timbilimu,
Sisi huku bado ni wamoja. Juhudi za kutuvuruga hazitafanikiwa. Kama anavyoeleza Chama jumuiya yetu isiruhusu na nina hakika haitaruhusu siasa zitugawe, eti mimi CCM mimi Chadema.
 
user-online.png
Indume Yene Unakata maini kweli. Hii Ze-Utamu nilifikiri imekwisha sahaulika kumbe bado inakumbukwa kwa sana tu. Labda kwa sababu wamiliki wanajulikana?
Sasa
user-online.png
Indume Yene unapoiingiza Ze-Utamu kwenye topic inayohusu kuanzishwa CCM tawi lake huko DC ina maana waliokuwa wanamiliki hiyo blog ni wafuasi wa CCM?

Ze-Utamukama ingekuwa mmiliki wake ni mwana_CCM ingewezekanaje wamtukane na kumchafua kipenzi cha wa pale Magogoni kwa kumvua nguo?

Kama ni hivyo kuna kazi nzito ya kujisafisha la sivyo laani ya kumtukana Mwenyekiti wetu na kumvua nguo hadharani katu haiondoki bila kutolea swadaka ya njiwa mweupe kafara.

CS.
Ingekuwa vyema kama ungeweka ujumbe wake ambao uliambatana na majibu yangu kwa kaka yangu Ze Mutuz. Mimi sijamtusi wala kumvua nguo, naomba uwe sahihi. Yeye aliongelea kuwa chama chake kimefungua blog hivi majuzi akihesabu kuwa hiyo ni maendeleo. Nilichosema au kujibu ilikuwa ni kwamba chama kilikuwa kimechelewa kufungua hiyo blog kuliko wengine ili kwenda na wakati.

Nikaongeza kuwa ni kweli kufungua blog ni vyema ili kuharakisha mawasiliano kwa wanachama au mashabiki wa chama. lakini maendeleo hayo yatapimwa iwapo goals zitakuwa zimefikiwa. Nikatoa mfano kuwa kuna mtu alifungua blog iitwayo Ze Utamu, kwa watu wengi wanajua impact ya hiyo blog. Sasa kwa mfano ule hatuwezi kusema hiyo blog ilikuwa na maendeleo kwa jamii ya kitanzania.

Kwa mara nyingine, naomba husipotoshe ukweli, ninamheshimu Kaka William na mtu yeyote yule. Sina classes, heshima ni kwa wote ila changamoto ni vyema tuka-share ili kuleta faida kwa Taifa letu.
 
nyie watt wa kishua babazen wana wasomesha kwa kodi ze2, ajui shida na maisha wanayo ishi watz....naamin mtalaaniwa..
 
Nadhani ndugu zetu mlioko huko ughaibuni ni watu wazima na akili nzuri. Sasa kwanini umoja na mshikamano wenu unavurugwa na watu wachache?

timbilimu,
Tatizo lilijitokeza kubwa tuliwahi kuchagua viongozi ambao tulidhani nia na lengo lao ni kuiongoza jumuiya kumbe walikuwa wasaliti walitumiwa na ubalozi ili kuifanya jumuiya kama kitengo cha ubalozi; katiba ya jumiya inajieleza wazi ni chombo huru kinachowaunganisha watanzania; matatizo mengi yalipandikizwa na huyu ofisa wa ubalozi, watanzania wengi hawakujua njama za huyu ofisa mpaka uchaguzi wa juzi alijaribu kupandikiza viongozi; ila ninachokuhahakishia viongozi waliopo madarakani hivi sasa wanaaminika na watu wenye nia kuiongoza jumuiya; bado tunaendelea kujiuliza ofisa huyu anayejidai ni usalama wa taifa anaiingilia jumuiya hii kwa maslahi ya nani? Jumuiya hii si ya kisiasa na hakuna hata siku moja ambayo kama jumuiya tumewahi kuivunjia heshima serikali yetu wala ubalozi, hiki ni chombo chetu sisi watanzania tuliopo huku ili tusaidiane, tuelemishane na kudumisha ukaribu wetu na ikibidi tuchangie maendeleo ya taifa letu hiki hakiwajahi kuwa chombo cha kisiasa Jumuiya ilikuwa karibu sana na ubalozi wakati Mzee Nyang`anyi baada ya kuondoka waliokuja hawakutaka kujishughulisha na jumuiya ila walipoalikwa walihudhuria shughuli za jumuiya matatizo mengi yanaletwa na huyu ofisa amekuwa akipandikiza usaliti ila mwaka huu amekwama na wala hatafanikiwa.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
CS.
Ingekuwa vyema kama ungeweka ujumbe wake ambao uliambatana na majibu yangu kwa kaka yangu Ze Mutuz. Mimi sijamtusi wala kumvua nguo, naomba uwe sahihi. Yeye aliongelea kuwa chama chake kimefungua blog hivi majuzi akihesabu kuwa hiyo ni maendeleo. Nilichosema au kujibu ilikuwa ni kwamba chama kilikuwa kimechelewa kufungua hiyo blog kuliko wengine ili kwenda na wakati.

Nikaongeza kuwa ni kweli kufungua blog ni vyema ili kuharakisha mawasiliano kwa wanachama au mashabiki wa chama. lakini maendeleo hayo yatapimwa iwapo goals zitakuwa zimefikiwa. Nikatoa mfano kuwa kuna mtu alifungua blog iitwayo Ze Utamu, kwa watu wengi wanajua impact ya hiyo blog. Sasa kwa mfano ule hatuwezi kusema hiyo blog ilikuwa na maendeleo kwa jamii ya kitanzania.

Kwa mara nyingine, naomba husipotoshe ukweli, ninamheshimu Kaka William na mtu yeyote yule. Sina classes, heshima ni kwa wote ila changamoto ni vyema tuka-share ili kuleta faida kwa Taifa letu.

Indume Yene Kaka, nilikuwa najaribu kukuchokoza tu kuhusu Ze-utamu uliyoitamka, maana ni wimbo ambao ulizua wacheza ngoma za Ze-Utamu ambazo zilikuwa zinakesha sana na kisha kusitishwa kwa kukiuka maadili. Ni namna ya kuzungumza tu kwangu labda hukunipata vizuri maana wakati mwingine kutoka Dodoma niendapo Singida huwa napendelea kupitia njia ya Kwamtoro badala ya ila ya Manyoni lakini safari ni ile ile ya kufika Singida uendako Indume Yene na mimi tunakutana huko huko Singida. Huenda ni mimi niliyekuwa mtengenezaji wa blog ile Ze-Utamu na sasa najaribu kwa nguvu zangu zote siri hii isisambae kwa kujisafisha maana home kutamu na ikitoka siri haya matamu yataota mbawa, kwani nimeshaanza kuweka mizizi kwa matamanio makubwa niliyonayo hapa sweet home.
 
Back
Top Bottom