Tatoo za mbunge huyu mhhhhh!

343t4ww.jpg


Wakuu hivi tatoo za namna hii zinaruhusiwa bungeni?
Mkuu mambo ya pwani hayo
 
Ni kweli dada Tina

Hee hapo ndiyo munachekesha kweli kweli, wahindi ndiyo wanapaka hina mpaka basi wakati wa harusi. Na wala haibagui muhindu, bohora au nani. Nyinyi bado munakomalia mashetani na majini hamwachi nyie! Kama hamuelewi si muulize tu mueleweshwe?

Na yule aliyeulizia kama mbunge anapata muda wa kusikiliza matatizo jimboni kwake, kupaka hina ya aina hiyo inachukuwa kama saa moja hivi, lakinni tunawaona akina mama na wabunge wanaweka vichwa vyao kwa wamasai kusukwa rasta kwa masaa kumi au zaidi, sasa ipi inakula muda?
 
Mhh! Nimekusoma mkuu but the so called mambo ya pwani yanafanya nini bungeni? kila mtu akipeleka utamaduni wake mjengoni itakuwaje?

Mzee Kimburu wewe kwanza ulikuwa hata hujui tafauti baina ya hina na tattoo, halafu unaulizia mambo ya pwani yanafanya nini bungeni - hebu nikuulize wale akina mama wanaovaa mapete ya dhahabu na vidani ni utamaduni wa wapi? Au hayo masuti ya huko bungeni ni utamaduni wa akina nani hapo bungeni?

Ni dhahiri kwamba wewe umefika hivi karibuni kutoka Tanganyika, tulia kwanza ujifunze mambo ya watu.
 
Shekhe mropokaji alishasema kwamba michoro mwilini inawa-please majini. Kwa watu wa Pwani, majini ni wao na wao ni majini. Takbriiii!!!
 
Jamani those are not tatoos! Ni piko ati.. And haivuti majini ni urembo tu!!
 
$hehe huyu bado mwali kaolewa juzi juzi tu, na imani za kiislamu siunajua lazima mwanamke aonekane alivyo au lazima arembwe kwa kupakwa hina, so sidhani kama mama kakosea.

Kweli Mkuu hio ni hina lakini Uislamu hauna uhusiano na mapambo hayo. Ukweli Uislam unakataza tabia hio ya kuonyesha mapambo hadharani. Anatakiwa mume wake tu ndio aone.

Issue hapa ni kanubi za Bunge na sio Uislamu na heena.
 
hizi hata mke wa mkubwa bona hua anajichora! yule lady wa kwanza(kwa kiingereza).
ila kwa me siszipendi mnolakini ni kma aaina ya pambo haswa la tamaduni za watu wa pwani.
 
343t4ww.jpg


Wakuu hivi tatoo za namna hii zinaruhusiwa bungeni?

mkuu nenda kaombe wale wabunge waliohamia mjengoni wakufungulie sehemu zao karibia ukimbie hiyo mbona sio hapo juu kuna waliosheheni picha za wah kwenye miili yao tatizo kuziona garama mpaka uhamie
 
Ni urembo na kiashiria tosha kwamba kulikuwa na shughuli hivi karibuni
 
Mheshimiwa Suupwika .. mi ndo nawasilisha eti! Vijana wa zenji waajiriwe jeshini kwa usawa… si tulimpiga mtu kule mpaka kakimbia nchi…

Alikimbizwa na mganda T. Okelo, wazenji walivyo kunguru kazi yao kulalamika tu!
 
Hina nzuri sana kwa siye watu wa pwani ni chachu ya mambo flani kunako bedi
Aha! mambo ya "Bedi", mahaba, na sherehe mpaka kwenye Bunge? Hiyo kali kweli kweli. Labda ndiyo maana wanasinzia na kulipuka na Ndiyoooo au "naunga mkono hoja mia kwa mia" wakati hata lililozungumzwa hakulisikia!
 
kama sura zilivyo tofauti, mawazo tofauti na fikra pia basi hata huyu naye ni tofauti na wengine. Halafu si wajua wenzetu walivyo kwa mapambo? Ukizingatia na posho za vihela vya migawo ya nauli nje ya bunge zipo sasa azifanyie nini kama hakuwakuta wananchi wake nje ya mjengo?
NI HALALI ACHA TU AJIREMBE.
 
Back
Top Bottom