Tatizo sugu la foleni Nairobi kuwa historia

Wakati wenzetu wa Kenya wanatarajia kuzindua barabara mpya yaani flyovers mwishoni mwa mwaka huu na itakuwa ndio mwisho wa foleni ya magari jijini Nairobi sisi hapa Dar tunapigania kujenga barabara zisizorasmi yaani (feeder roads) ili kumaliza tatizo la msangamano wa magari .Nadiriki kusema ya kuwa ni lazima tujiulize inakuaje wenzetu wanaweza sisi tunashindwa?

Hata mimi nilikuwa Nairobi nimeliona hilo, huku kwetu tutasubiri sana tukiwa na serikali legelege, hata Magufuli simwamini tena kutokana na kauli zake alizotoa Igunga, hana tofauti na baba yake. Hivi ni nani asiyejua kuwa Rais wa mwisho Tz aliondoka madarakani 2005? Mema yatafanyika iwapo tutaondoa hiki chama cha maslahi madarakani, kama sivyo tukubali kuwa twamhitaji Lowassa! Hawa wengine hawatufikishi mahali. Mabadiliko lazima jamani
 
Back
Top Bottom